Tanzania na Visiwa vya Comoro zimesaini Hati nne za Makubaliano kwenye kilele cha Mkutano wa Kwanza wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC)

Tanzania na Visiwa vya Comoro zimesaini Hati nne za Makubaliano kwenye kilele cha Mkutano wa Kwanza wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC)

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Tanzania na Visiwa vya Comoro zimesaini Hati nne za Makubaliano kwenye kilele cha Mkutano wa Kwanza wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Comoro uliofanyika tarehe 24 Julai, 2024 jijini Dar es Salaam.

Hati zilizosainiwa katika kikao hicho zinazojumuisha nyanja za; Ushirikiano wa Kidiplomasia, Afya, Biashara na Viwanda na Teknolojia ya Habari. Utiaji saini hati hizo umeshuhudiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro anayeshughulikia Nchi za Kiarabu, Nchi zinazozungumza Kifaransa, Diaspora na Mtangamano wa Afrika Mhe. Mohamed Mbae.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo wa kihistoria, Waziri Tax ameelezea umuhimu wa kusainiwa kwa hati hizo kuwa itawezesha pande hizo mbili kuwa na ushirikiano ulio katika mpangilio mzuri katika nyanja husika na hivyo kuleta tija zaidi.

“Pamoja na kutia saini Hati za Makubaliano pia tumekubaliana kuendelea kushirikiana katika maeneo mengine ya miundombinu, nishati, ulinzi” alisema.

FB_IMG_1721874650771.jpg
FB_IMG_1721874660973.jpg
FB_IMG_1721874664204.jpg
FB_IMG_1721874667215.jpg
FB_IMG_1721874670083.jpg
FB_IMG_1721874672790.jpg
 
Yes Comoros nchi maskini Sana kama Zanzibar hakuna faida na mashiko ni hasara Tu kwa Tanganyika
 
Kila nikiwaza muungano wa Tanganyika na zanziba huwa najiuliza ilikuwaje nyerere alizidiwa vipi ujanja na viongozi wa zanzibar? Angalia alichoifanyia nchi yake mwenyewe na matokeo yake. Na hawa wacomoro nao nina wasi wasi wanufaika wakubwa watakuwa ni wao kuliko sisi.
 
Back
Top Bottom