John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Tanzania imeshika nafasi ya Pili kati ya nchi 43 za Barani Afrika zilizoshiriki kwenye dodoso kuhusu Usalama Mtandaoni, lililoandaliwa na Global Cybersecurity Index (GCI).
Pia, kati ya Nchi 155 Ulimwenguni, Tanzania inashika nafasi ya 21 kwa unafuu wa gharama za kununua GB 1.
Aidha, Tanzania inashika nafasi ya 6 kwa unafuu zaidi wa gharama ya data kati ya Nchi 55 Barani Afrika.
Takwimu hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabiri K. Bakari wakati akizungumza kwenye mjadala kuhusu Maendeleo katika Sekta ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, katika kipindi cha Mwaka mmoja wa utendaji wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.