Tanzania nakupenda kwa moyo wote

Tanzania nakupenda kwa moyo wote

Lyrics[edit]​

Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote
Nchi yangu Tanzania
Jina lako ni tamu sana
Nilalapo nakuota wewe
Niamkapo ni heri mama wee
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote.

Tanzania Tanzania
Ninapokwenda safarini
Kutazama maajabu Biashara nayo makazi
Sitaweza kusahau mimi mambo mema ya kwetu kabisa
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote.

Tanzania Tanzania
Watu wako ni wema sana
Nchi nyingi zakuota nuru yako hakuna tena
Na wageni wa kukimbilia ngome yako imara kweli wee
Tanzania Tanzania
Heri yako kwa mataifa.

Tanzania Tanzania
Karibu wasio na kwao
Wenye shida na taabu
Kumbizwa na walo wezi
Tanzania yawakaribisha
Tuungane kiume chema wee
Tanzania Tanzania
Mola awe na we daima.
 
Ila MODS lazima aliyeleta hii mada huku ana matatizo na uzalendo.
Kwanza, mmeiondoa kule siasa-sawa
Pili, mmeipeleka Machanganyiko-sawa

Hili la kuileta Entertainment si suala la kulifumbia macho.
Uzalendo wa nchi si swala la kina Diamondi na Harmonize au Ali Kiba.
THIS IS NOT ENTERTAINMENT, ITS PATRIOTISM, unless mna walakin!
 
Back
Top Bottom