Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,892
- 16,476
Good evening jamiiforums
Mnamo mwaka 2018 mwezi wa August niliwahi kuhoji usahihi wa kisarufi katika matumizi ya maneno "Tanzania" na "National" katika kuunda jina la uwanja wa taifa kwa lugha ya kiingereza uliosomeka kama "Tanzania National Main Stadium" kwenye lango kuu.
Soma Hapa>>> Uwanja wa taifa kuandikwa "Tanzania National Main Stadium" ni sahihi katika sarufi(grammar) ya kiingereza?
Sijaenda uwanja wa taifa muda mrefu ila kulingana na maelezo ya rafiki zangu nasikia lile bango pale lango kuu limetolewa na sasa pameandikwa "Benjamin Mkapa Stadium".
Kama hii taarifa ni kweli basi wamefanya jambo la maana sana kwa maana hata Senegal wanao uwanja wa taifa unaoitwa "Léopold Sédar Senghor" jina la baba wa taifa lile.
Kulingana na maelezo ya wataalam wa lugha, maneno "Tanzania" na "National" hayapaswi kutumika pamoja kwa maana yana maana zinazoshabihiana.
Je ni sahihi kwa shirika la utangazaji la TBC kuitwa TNBC (Tanzania National Brodcasting Corporation) au lile la nyumba la NHC kuwa TNHC (Tanzania National Housing Corporation)?
Sasa wiki iliyopita nikiwa ninatazama taarifa ya habari ile ya saa moja ambayo wanaiita ARIDHIO ndio nikaja kukutana na hii ya "Tanzania National Business Council" (TNBC) ndio nikakumbuka kuwa haya ndio yale yale ya uwanja wa taifa ya kuchanganya maneno mawili yanayoshabihiana kwa maana.
Kwanini isingekuwa "Tanzania Business Council (TABC)" au "National Business Council (NABC)" kama ilivyo kwa TBC na NHC?
Mbona shirika la Utanganzaji sio TNBC na wala lile la nyumba haliitwi TNHC? Kuna nini kinaendelea hapa au mimi ndio mshamba wa lugha? Kama suala ni mfanano mbona TISS ya BOT inafanana na ile TISS ambayo ni idara ndani ya ofisi ya Rais na bank kuu hawawazi hata kubadili jina la huo mfumo ila maisha yanaendelea kama kawaida?
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.