Kweli JMushi, ila hofu yangu ni kwamba tunakuwa vipofu wa makusudi kuhusu how change really occurs. inachukua muda. sisemi kwamba serikali yake kikwete is on point kwa kila kitu, kwa mfano hizo sekondari za kata za vodafasta kweli ni dangaya toto: bila waalimu wazuri tutavuna kizazi cha watanzania wasioajirika huko mbele ya safari kwasababu ya uduni wa elimu. Ila nadhani leo hotuba ya rais imeashiria kwamba tupende tusipende Kikwete anafanya kazi kwa mantiki, anayo system yake, na anapenda kutoa majibu kamili ya utendaji baada ya kufanya kazi badala ya kuropoka ovyo.
wapinzani wa ndani na nje ya bunge wametuzoeza hizi sera na politics za kugrand-stand. hata ninavyo wapenda wapiganaji akina chadema crew na baadhi ya wabunge wa CCM, ninawaamini zaidi watendaji ambao wanafanya mambo yao kimya na kutoa majibu kwa kufikiria kama akina Pinda (and perhaps Kikwete to some extent). Sasa nitapenda kuwaona wapinzani watakavyompaka matope knowing that it is always far easier to criticize someone who is making an attempt- kwani wao hawajapata nafasi ya kupambana na changamoto za kuendesha nchi (siyo majimba na halmashauri tu) huku wakitukanwa hadharani kila siku. tusizoee ku-underestimate kazi za serikali.