Ni watu wanaofikiria huru kama mimi ndio wanaoweza kuchambua kwa haki... sio wale ambao mkate wao wanapatia kutoka CCM, au wale ambao wanategemea panapo 2010 na wao... wapate fedha za walipa kodi....
Kuna mambo ya msingi kabisa JK ambayo ameongelea... Nitataja machache!
1. Mchakato wa Sheria ya Uchaguzi (Election Financing) ndani ya vyama na wakati wa uchaguzi wa vyama... (hiyo mahafidhina hawajaona kwamba ni jambo jema)... by April 2009 sheria itakuwa imefikishwa bungeni.
2. Sheria ya kumpa au kuipa taasisi ya Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali Meno.
3. Kupitishwa kwa sheria mpya ya TAKUKURU.
4. Marekebisho ya Sheria ya EWURA.
5. Ukuaji wa Demokrasia na Uhuru wa maoni!
6. Fedha za EPA, kwenda kwenye TIB kuanzisha mtaji wa Kilimo, zingine kwenda kwenye ruzuku ya Mbolea na Dawa za Mifugo...
7. Chuo Kikuu cha Dodoma, Intake expected to 8,000 students, Kitila tukitoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam tulikuwa kama 5,000/-
8. Ukuaji wa Utalii - mapato kutoka $600mi.. kwenda $1200mil and USA kuongoza kwa watalii.
9. Umeme kwa wilaya zote nchini except Nkasi at least by now... but they are working on it.
10. Amezungumzia barabara kwa undani... mwenye akili timamu anaweza kujua hilo.
11. Issue ya Zanzibar done.
12. Issue ya Richmond... out of the scope... waziri Mkuu ndiye ataipeleka Bungeni specific, hivyo hakutakiwa kuizungumzia.
13. Muafaka ni sehemu ambayo bado wako nyuma.
14. Mambo ya inflation ameongelea kwa namna ambayo hata mimi nilikuwa sikuwa fahamu adhari zinginge ukitegemea mimi nimesomea mifugo.
15. Michezo... focus tunapeleka kwenye riadha.
16. Amedumisha utawala bora... waliosikiliza alisoma mapendekezo ya CAG. na hatua alizochukua ikiwa pamoja na kuunda tume ya Mwanyika...kurudishwa kwa fedha...
My take kwenye hili... huu ndio ulikuwa mchezo wetu waTanzania wengi wa Kuiba... dawa ilikuwa baada ya fedha zetu kurudishwa.. tuachane nao tuendelee na shughuli zingine we have other priorities... mifano hii imefanyika sehemu nyingi duniani kwa watu makini...
South Africa: Baada ya ubaguzi Mandela alivyochukua nchi... hakuwapeleka wazungu magereza aliunda tume ya maridhiano mambo yakaisha.
Kenya: Baada ya mauaji... wanachofanya sio kupelekana magereza.
Zambia: walifanya tofauti... wakatimuana kila wakati... b'se of nonsense decision za Chiluba.