Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi kuna habari kama polisi iliarifiwa na kuruhusu maandamano hayo ? Maana kumekuwa na mtindo ambao si wakawaida kwa Polisi kutangaza habari za maandamano ya vyuma vya upinzani ,utawasikia wanafikiria ,wameruhusu halafu utasikia wameandika barua kuzuia mpaka itakapotolewa taarifa nyengine.
Wapinzani mupo ? mambo kama haya ni lazima muyachungue na kupata uthibitisho kuwa CCM waliandika barua kuomba kibali au kuiarifu polisi ,maana hi nchi si ya CCM peke yao wafanye watakavyo bungeni na huku mitaani mambu ni hayo hayo.
Hili ni muhimu kuliangalia kwa udnani kwa sababu kuna uwezekano maandamano haya yamefanyika kienyeji mno. Yamekuwa ya ghafla sana. Hivi watu wakiomba kuandamana kupinga hotuba ya muunwgana wanaweza kuruhusiwa haraka haraka namna
hii?
Mimi sishangazwi wala nino maana ndio demokrasia lol....mkipinga wenzenu wanaunga mkono....!! Mwendo mdundo.
Kama wanaanchi wanaandama kumpongeza JK, hiyo ni dalili tosha kwamba somo letu hapa JF halitoshi kabisa. Wakati sisi tunaenda mwezini, CCM wanaenda kwa wananchi.
Pia ni makosa kuwalaumu CCM kuaandaa hayo maandamano, wa kulaumiwa hapo ni sisi wenyewe ambao tunashindwa kufikisha hoja zetu kwa wananchi. Na pia hao wananchi ambao pamoja na hali ngumu, ufisadi na dhuluma zingine bado wanapoteza muda wao kwenda kwenye maandamano ya kumuunga mkono msanii.
Ule mpango wa kuijadili hotuba ya Kikwete Bungeni umezimwa. taarifa kutoka huko, zilizothibitishwa na Spika Sitta, zinaeleza kuwa mjadala wa hotuba hiyo hautakuwepo hivi sasa, labda katika bunge la Novemba.
Taarifa ni kuwa mjadala huo umefutwa kwa sababu hotuba ya rais hadi hivi sasa bado haijakamilika. Alisema maneno mengi wakati wa hotuba ambayo yapo nje ya hotuba yake iliyokuwa imeandikwa. Imeshindikana kuingiza hayo maneno mengine kwenye hotuba na kuwahi kutengeneza vitabu vya hotuba ambavyo vingegawiwa kwa wabunge
Ni kweli hata mimi nilimsikia Spika akisema kuwa vitabu vimepelekwa Ikulu kwa ajili ya kufanyiwa uhariri sasa uhariri wanini kama Hansard walirekodi?si hata TV walitoa live na wengine kuirudia usiku?hapa maji yamezidi unga sasa ugali utaiva? na uji haunyweki kwani watu walilala njaa......
Kwani hujawahi kusikia madai kwamba watu weusi wana akili pungufu kuliko wengine? Sijui ukweli wa madai hayo, ila inaonekana kuna matatizo fulani katika fikra za binadamu-nyani.