DAR si LAMU
JF-Expert Member
- Mar 31, 2007
- 2,928
- 551
Najaribu kupata nakala niisome vizuri, kwani kuna mambo yanahitaji kutafakari kidogo.
Hotuba hii imejaa data nyingi za kiuchumi ambazo ni economic indicaters muhimu, naimani approach hii ni nzuri na viongozi wengine wataiga, mfano aliposema dept/gdp ratio yetu sasa ni 25% ukilinganisha na 90% mwaka 2005 hii nidata muhimu kwa mwanauchumi makini.
Nimefurahishwa na approach ya kuanza kuukataa umaskini kwa kukataa kurudi HIPC, jambo hili jamani hebu tulipongeze.
Kuna hili la Imported inflation nadhani hapa anahitaki kwenda deep kidogo, mfano kitasa cha yale/union kimeuzwa shs 17,000/= tangu 2005 hadi leo bei ni hiyo hiyo. kigae cha spain 1' x 1' kimeuzwa shs 1200/= hadi leo. sealing board ya SA imepanda kutoka 9500/= hadi 12000/= ongezeko hili inawezekana nikutokana na kupanda kwa gharama za usafirishaji.
Hebu tuangalie locally produced goods katika soko la kamachumu, mchele umepanda kutoka shs 180/= mwaka 2005 hadi 1400/= todate, saruji imepanda kutoka 9800/= hadi 25,000/=, sukari kutoka 380/= hadi 1800/= vyote hivi has nothing to do with imported inflation.
Suala la diesel; iweje diesel kigali iuzwe franc 770 (= tshs 1400) na dar diesel iuzwe tshs2000! wakati rwanda wanapitishia diesel bandari ya dar!
Amesema alipofika Dodoma university alishangaa kweli, naimani alishangazwa na ujenzi uliomahili na sio uzuri wa students wanaosoma pale.
..ni kweli kwamba hizo data zinavutia. lakini, unafikiri zina maana yeyote kwa mwananchi wa kawaida, ambaye anapata tabu ya kula mlo wa kutosha kwa sababu bei za bidhaa zimepanda sana?
..hizo data kama unawahutubia wataalamu au wasomi zinakuwa zimefika kwa walengwa. lakini, kama unahutubia wananchi utakuwa kama unapigia mbuzi gitaa. wananchi wanataka majibu ya shija zao na si takwimu. ukisema uchumi umekuwa, basi na useme umesambaza maji vijijini, umejenga barabara,na zahanati vijijini zimepata dawa na hii iwe kweli na si iwe imepikwa kwenye data za wizara.
..pia, ajira za kweli ziwe zimetengenezwa vijijini na mijini. wakulima wawe wamepata mbolea na mbegu.
..hayo mambo ya hipc yana kazi kubwa. kwani tunakusanya kiasi gani cha mapato na tunatumia kiasi gani?. halafu, kama ndio tuko kwenye mkao wa kukopeka, je hiyo haiwezi kuturudisha kule kwenye madeni makubwa?. kumbuka, watu wa magharibi wanapenda tuwe tunadaiwa daima.