Tanzania Nchi 1 ya JMT, Zanzibar Kujiita Nchi, Sio Uhaini?. Zanzibar Iadabishwe Kuondoa Ubatili wa Katiba Yake ili Tuitambue au Tumchelee Mwana Kulia?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
Makala yangu ya leo kwenye gazeti la Mwananchi.
Screen Shot 2024-12-11 at 6.10.52 PM.png

Kuna msemo wa Kiswahili usemao, mchelea mwana kulia , hulia yeye!. Makala hii ni swali "Tanzania ni nchi moja ya JMT, Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT, kitendo cha Zanzibar kujiita nchi, huku imenyamaziwa, huu sio uhaini?, kitendo cha hali hii kuachwa bila kukemewa, huku sio kumchelea mwana kulia?, Je Zanzibar Iadabishwe kwa kulazimishwa kuondoa ubatili wa Katiba yake unaokwenda kinyume na katiba ya JMT, ili katiba ya JMT, iitambue katiba ya Zanzibar, au kwa vile tunaiogopa sana, bora tuu tuendelea kumchelea huyu mwana kulia?

Japo kimataifa Tanzania ni nchi moja ya JMT, chini ya serikali moja ya JMT, inayoongozwa na rais mmoja, rais wa JMT ambaye ni mkuu wa nchi, mkuu wa serikali na Amiri Jeshi Mkuu, lakini kitaifa Tanzania ni nchi moja yenye katiba mbili, katiba ya JMT na Katiba ya Zanzibar, yenye marais wawili, rais wa JMT na Rais wa Zanzibar, yenye mabunge mawili, Bunge la JMT na Baraza la Wawawakilishi, yenye mahakama mbili, Mahakama Kuu ya JMT, na Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Japo Muungano wetu adhimu na adimu, ni muungano wenye nchi mbili zenye haki sawa na hadhi sawa ndani ya muungani licha ya ukubwa wa eneo la mshirika mmoja Tanzania Bara na udogo wa eneo la mshirika mwingine, Zanzibar, Katiba ya JMT, ndio katiba mama, na inaitambua katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Katiba hiyo ya Zanzibar, ilifanyiwa marekebisho makubwa na kutoa toleo la mwaka 2010, lakini mpaka hivi leo ninapoandika hapa, Katiba ya JMT, imegoma kata kata kuyatambua marekebisho hayo ya Katiba ya Zanzibar na mpaka hii leo, bado katiba yetu hailitambui toleo la mwaka 2010 la ya Zanzibar iliyounda Serikali ya Umoja wa Kitaifa SUK, kutokana na baadhi ya vipengele vya katiba ya Zanzibar kukinzana na Katiba ya JMT.

Ibara ya kwanza ya Katiba ya JMT inasema “1. Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano.
Ibara ya pili ya katiba ya JMT inasema

2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.

Ibara kwanza ya katiba ya Zanzibar inasema

1. Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Ibara ya Pili ya katiba ya Zanzibar inasema

2. Zanzibar ni miongoni mwa Nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hizi ibara mbili tuu za kwanza, ni sio tuu zimevunja katiba ya JMT, bali zimefanya kosa kubwa la uhaini kuivunja JMT ndani ya nchi mbili.

Kabla ya muungano wetu adhimu, tulikuwa nan chi mbili za Tanganyika na Zanzibar, muungano wetu ni muungano wa union, kwa nchi mbili kuungana na kuwa nchi moja. Nchi ya Zanzibar na nchi ya Tanganyika, zote zilikufa na kuunda nchi moja ya JMT. Kitendo cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 inatamka kwamba Zanzibar ni Nchi na inatamka mipaka ya eneo lake katika Ibara ya 1 inayosema "Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar." Wakati Katiba ya JMT imeitangaza Tanzania ni nchi moja ya JMT na kutaja eneo la JMT ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.
Huu ni mkanganyiko.

Hapa Zanzibar imejitangaza kama nchi, tangazo hili ni kama kuvunja muungano.

Wakati haya yakifanyika, nchi ilikuwa chini ya Rais Jakaya Kikwete, mtu rahimu sana, aliamua kunyamaza kimya bila kuingilia kwa hoja kuwa hayo ni mambo ya ndani ya Zanzibar, kilichofanyika ni kwa Katiba ya JMT, ku ignore (kuyapuuza) mabadiliko hayo ya Katiba ya Zanzibar kwa katiba ya JMT kutofanyiwa mabadiliko hivyo mpaka leo, katiba ya Zanzibar haitambuliwi na katiba ya JMT, huku katiba ya JMT, ikiendelea kuitambua katiba ambayo imeishafutwa.

Katiba hiyo ya Zanzibar katika Ibara ya 26 inatamka kwamba Rais wa Zanzibar ni Mkuu wa Nchi ya Zanzibar Katiba ya Jamhuri ya Muungano katika Ibara ya 33(2) inatamka "Rais wa Jamhuri ya Muungano ndiye Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu". Hapa ni muendelezo wa Zanzibar kujitangaza kuwa ni nchi, na kumtangaza Rais wa Zanzibar kama mkuu wa nchi, wakati ukweli ni Tanzania ni nchi moja ya JMT, Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT, yenye utawala wake wa ndani.

Katiba ya Zanzibar haikuishia hapo, katika Ibara ya 2A inatamka kwamba "Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali, Rais aweza kuigawa Zanzibar katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi."

Masharti haya ni kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano Ibara ya 2(2) ambayo inatamka "Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Rais aweza kuigawa Jamhuri ya Muungano katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge: Isipokuwa kwamba Rais atashauriana kwanza na Rais wa Zanzibar kabla ya kuigawa Tanzania Zanzibar katika Mikoa,Wilaya au maeneo mengineyo."

Ibara hiyo inapoka madaraka ya rais wa JMT, kupoka madaraka ya rais ni kosa la uhaini!.

Katika Ibara ya 132 ya katiba ya Zanzibar, inatamka kwamba "Hakuna Sheria yoyote itakayopitishwa na Bunge la Muungano ambayo itatumika Zanzibar mpaka Sheria hiyo iwe ni kwa ajili ya mambo ya Muungano tu na ipitishwe kulingana na maelekezo yaliyo chini ya vifungu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Sheria kama hiyo lazima ipelekwe mbele ya Baraza la Wawakilishi na Waziri anayehusika.Ibara hii inaeleza zaidi, pale Sheria ndogo inapoundwa kwa mujibu wa uwezo uliowekwa chini ya kijifungu cha 132(1) na (2) itatumika tu pale itakapotimiza shuruti zote zilizowekwa kwa matumizi ya Sheria Mama kama ilivyoainishwa katika kifungu hiki"

Masharti haya ni kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano Ibara ya 64 ambayo inatamka kwamba Bunge la Jamhuri ya Muungano ndilo lenye mamlaka ya kutunga sheria kwa mambo ya Muungano (Bara na Zanzibar) na yasiyo ya Muungano ya Tanzania Bara. Ibara hiyo imepoka madaraka ya Bunge la JMT kutunga sheria za mambo ya muungano na kulifanya BLW ndilo lenye mamlaya ya kuu kuhusu muungano.

Katika Ibara ya 24(3) ya Katiba ya Zanzibar, "Rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu (Zanzibar) katika shauri lililofunguliwa dhidi ya masharti ya Sura hii ya Katiba yatasikilizwa na Mahakama Kuu (Zanzibar) mbele ya Majaji watatu, na uamuzi wao utakuwa ni wa mwisho na hautokatiwa rufaa kwenye Mahakama ya Rufaa ya Tanzania." Ibara hii ni kinyume cha Ibara ya 117(1) na (4) ambayo inatamka kwamba Mahakama ya Rufani ndiyo yenye Mamlaka ya juu ya kutoa haki nchini na uamuzi wake ni wa mwisho hivyo Mahakama Kuu ya Zanzibar, kupoka mamlaka ya Mahakama ya Rufani ya JMT na Jaji Mkuu wa Zanzibar kuwa ndie mkubwa kuliko Jaji Mkuu wa Tanzania.

Ukiondoa hiyo mikanganyiko ya katiba ya Zanzibar na katiba ya JMT, mabadiliko hayo ya katiba ya Zanzibar pia yameleta mambo mazuri, Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), kwa jina maarufu la GNU (Government og National Unity), hili ni jambo jema, kubwa, zuri na la kheri, japo ki protokali, serikali ya JMT inaitambua SUK na viongozi wake wanapewa protokali stahiki kitaifa na kimataifa, sasa ni muda muafaka kwa Katiba ya JMT, ama iitambue rasmi katiba ya Zanzibar, kwa kuifanyia marekebisho katiba ya JMT na kuuingiza SUK, au Zanzibar ilazimishwe kuuondoa huo utata wa Katiba ya Zanzibar kupoka mamlaka ya JMT, Rais, Bunge na Mahakama ili itambuliwe rasmi.

Hitimisho
Je Zanzibar Iadabishwe kwa kulazimishwa kuondoa ubatili wa Katiba yake unaokwenda kinyume na katiba ya JMT, ili katiba ya JMT, iitambue katiba ya Zanzibar, au kwa vile tunaiogopa sana, bora tuu tuendelea kumchelea huyu mwana kulia?

Kuna mambo mengi tuu ya Zanzibar, JMT inayachelea mwana kulia, moja la mfano ni lile la umeme, Wazanzibari wamekuwa wakitumia umeme wa Tanesco bila kulipia kwa muda mrefu, hali iliyopelekea kulimbikiza deni likawa kubwa la muda mrefu hadi kuwa halihimiliki, Tanesco wakatangaza kuikatia umeme Zanzibar, isipolipa!, rais wa Zanzibar akatangaza hatulipi, kama ni kutukatia umeme waache wakate, tutawasha vibatari na koroboi ndipo serikali ya JMT ikaingilia kati, ikawasamehe deni lote likafutwa. Hii maana yake wenzetu wametumia umeme wa bure!, sijawahi kusikia hata maramoja familia masikini za huku bara wanaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, wakisamehewa deni la umeme!, lakini wenzetu wamesamehewa!. huku ndiko ninakukuita kumchelea mwana kulia. Sasa kwenye hili la Katiba, je Zanzibar aadabishwe kwa kulazimishwa kuondoa huu ubatili wa katiba yake unaokwenda kinyume na katiba ya JMT, ili katiba ya JMT, iitambue rasmi katiba ya Zanzibar, au kwa vile tunaiogopa sana, Zanzibar kuiambia ukweli, ni bora tuu tuendelea kumchelea huyu mwana kulia?

Paskali
 
Mimi nadhani Kwa njia za kidiplomasia, Zanzibar anazidi kua Nchi Huru.

Hilo ndio Kosa ambalo Tanganyika inalifanya, uhuru anaoendelea kupewa Zanzibar na kuzidi kujitanua na kujulikana Kimataifa... Amini amini nawaambia, Kuna Siku wataidai Zanzibar, na wataidai hata Kwa Bunduki na wataidai katika wakati ambao nyuma yao kutakua na mataifa mengi ya Kiislam na yale ya wamagharibi .

Kwa namna yoyote Ile, Zanzibar inapaswa kua sehem ya Tanganyika , suala la Zanzibar kujiita Nchi ni Uhaini.

Kama kuilinda Tanzània haiwezekan, basi tuwaache wawe Nchi kamili Sasa.
 
Waziri mkuu mstafu Mizengo alishaliambia bunge kuwa Zanzibar si nchi.
Katiba ya Zanzibar inaishia hapo Zanzibar. Utambulisho wa uzanzibar na utanganyika upon ndani ya mipaka tu. Dunia yote yatambua Tanzania 🇹🇿
Zanzibar ni Jimbo la Tanzania kama Dubai katika UAE
 
Utaratibu uliokuwepo kipindi cha utawala wa Kikwete ilikuwa iandikwe kwanza katiba ya Zanzibar ifuate katiba ya jmtz ambayo ndani yake ingekuwa na serekali tatu,serekali ya mapinduzi,serekali ya muungano na serekali ya Tanganyika.

Ndani ya katiba hiyo Tanganyika ingetambuliwa kama nchi kama ilivyo upande wa Zanzibar,wakati mchakato wa kuandaa katiba unaendelea upande wa Zanzibar ndio waliofanikiwa kuandika katiba mpya kwa kuwa ili kuwa wao ndio watangulie kuandika katiba yao kwanza ndio ije ya jmtz ambayo ingekuwa na serekali 3 na nchi mbili ambazo zimeungana.

Mambo yalipo hamia upande wa katiba ya jmtz CCM waliharibu mchakato wa katiba mwishoni kabisa wakati katiba ya Zanzibar ilishakamilika zamani na isingekuwa rahisi kurudia tena.

Mkanganyiko uliopo kwenye katiba ya Zanzibar na jmtz ulitokea kutokana na wazanzibar kuamini kuwa watanganyika nao wanakwenda kupata serekali yao na nchi yao ya Tanganyika inakwenda kurudi hivyo walitaka kuweka mambo sawa wakati katiba ya jmtz inaitambua Tanganyika kama nchi yenye serekali yake kutokana na katiba ya Tanganyika ambayo ingekuja kuandikwa mbeleni wazanzibar nao wawe wameitambua Zanzibar kama nchi yenye serekali yake.

Kwa hiyo wazanzibar hawapaswi kulaumiwa kwenye mkanganyiko huu,wakulaumiwa ni CCM kwa kuingilia na kuharibu mchakato mzima wa katiba iliotokana na wananchi wakiongozwa na Waryoba.
 
Uhaini wa wapi ? Huna akili.

Hivi unajua hata Tanganyika ni nini ? Na Zanzibar ni nini ? Au unajiandikia tu
 
Waziri mkuu mstafu Mizengo alishaliambia bunge kuwa Zanzibar si nchi.
Katiba ya Zanzibar inaishia hapo Zanzibar. Utambulisho wa uzanzibar na utanganyika upon ndani ya mipaka tu. Dunia yote yatambua Tanzania 🇹🇿
Zanzibar ni Jimbo la Tanzania kama Dubai katika UAE
Wewe na yeye wote akili hamna
 
Utaratibu uliokuwepo kipindi cha utawala wa Kikwete ilikuwa iandikwe kwanza katiba ya Zanzibar ifuate katiba ya jmtz ambayo ndani yake ingekuwa na serekali tatu,serekali ya mapinduzi,serekali ya muungano na serekali ya Tanganyika.

Ndani ya katiba hiyo Tanganyika ingetambuliwa kama nchi kama ilivyo upande wa Zanzibar,wakati mchakato wa kuandaa katiba unaendelea upande wa Zanzibar ndio waliofanikiwa kuandika katiba mpya kwa kuwa ili kuwa wao ndio watangulie kuandika katiba yao kwanza ndio ije ya jmtz ambayo ingekuwa na serekali 3 na nchi mbili ambazo zimeungana.

Mambo yalipo hamia upande wa katiba ya jmtz CCM waliharibu mchakato wa katiba mwishoni kabisa wakati katiba ya Zanzibar ilishakamilika zamani na isingekuwa rahisi kurudia tena.

Mkanganyiko uliopo kwenye katiba ya Zanzibar na jmtz ulitokea kutokana na wazanzibar kuamini kuwa watanganyika nao wanakwenda kupata serekali yao na nchi yao ya Tanganyika inakwenda kurudi hivyo walitaka kuweka mambo sawa wakati katiba ya jmtz inaitambua Tanganyika kama nchi yenye serekali yake kutokana na katiba ya Tanganyika ambayo ingekuja kuandikwa mbeleni wazanzibar nao wawe wameitambua Zanzibar kama nchi yenye serekali yake.

Kwa hiyo wazanzibar hawapaswi kulaumiwa kwenye mkanganyiko huu,wakulaumiwa ni CCM kwa kuingilia na kuharibu mchakato mzima wa katiba iliotokana na wananchi wakiongozwa na Waryoba.
Kikwete ndiye aliyharibu mchakato
 
Wanabodi,
Makala yangu ya leo kwenye gazeti la Mwananchi.
View attachment 3174619

Kuna msemo wa Kiswahili usemao, mchelea mwana kulia , hulia yeye!. Makala hii ni swali "Tanzania ni nchi moja ya JMT, Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT, kitendo cha Zanzibar kujiita nchi, huku imenyamaziwa, huu sio uhaini?, kitendo cha hali hii kuachwa bila kukemewa, huku sio kumchelea mwana kulia?, Je Zanzibar Iadabishwe kwa kulazimishwa kuondoa ubatili wa Katiba yake unaokwenda kinyume na katiba ya JMT, ili katiba ya JMT, iitambue katiba ya Zanzibar, au kwa vile tunaiogopa sana, bora tuu tuendelea kumchelea huyu mwana kulia?

Japo kimataifa Tanzania ni nchi moja ya JMT, chini ya serikali moja ya JMT, inayoongozwa na rais mmoja, rais wa JMT ambaye ni mkuu wa nchi, mkuu wa serikali na Amiri Jeshi Mkuu, lakini kitaifa Tanzania ni nchi moja yenye katiba mbili, katiba ya JMT na Katiba ya Zanzibar, yenye marais wawili, rais wa JMT na Rais wa Zanzibar, yenye mabunge mawili, Bunge la JMT na Baraza la Wawawakilishi, yenye mahakama mbili, Mahakama Kuu ya JMT, na Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Japo Muungano wetu adhimu na adimu, ni muungano wenye nchi mbili zenye haki sawa na hadhi sawa ndani ya muungani licha ya ukubwa wa eneo la mshirika mmoja Tanzania Bara na udogo wa eneo la mshirika mwingine, Zanzibar, Katiba ya JMT, ndio katiba mama, na inaitambua katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Katiba hiyo ya Zanzibar, ilifanyiwa marekebisho makubwa na kutoa toleo la mwaka 2010, lakini mpaka hivi leo ninapoandika hapa, Katiba ya JMT, imegoma kata kata kuyatambua marekebisho hayo ya Katiba ya Zanzibar na mpaka hii leo, bado katiba yetu hailitambui toleo la mwaka 2010 la ya Zanzibar iliyounda Serikali ya Umoja wa Kitaifa SUK, kutokana na baadhi ya vipengele vya katiba ya Zanzibar kukinzana na Katiba ya JMT.

Ibara ya kwanza ya Katiba ya JMT inasema “1. Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano.
Ibara ya pili ya katiba ya JMT inasema

2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.

Ibara kwanza ya katiba ya Zanzibar inasema

1. Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Ibara ya Pili ya katiba ya Zanzibar inasema

2. Zanzibar ni miongoni mwa Nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hizi ibara mbili tuu za kwanza, ni sio tuu zimevunja katiba ya JMT, bali zimefanya kosa kubwa la uhaini kuivunja JMT ndani ya nchi mbili.

Kabla ya muungano wetu adhimu, tulikuwa nan chi mbili za Tanganyika na Zanzibar, muungano wetu ni muungano wa union, kwa nchi mbili kuungana na kuwa nchi moja. Nchi ya Zanzibar na nchi ya Tanganyika, zote zilikufa na kuunda nchi moja ya JMT. Kitendo cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 inatamka kwamba Zanzibar ni Nchi na inatamka mipaka ya eneo lake katika Ibara ya 1 inayosema "Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar." Wakati Katiba ya JMT imeitangaza Tanzania ni nchi moja ya JMT na kutaja eneo la JMT ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.
Huu ni mkanganyiko.

Hapa Zanzibar imejitangaza kama nchi, tangazo hili ni kama kuvunja muungano.

Wakati haya yakifanyika, nchi ilikuwa chini ya Rais Jakaya Kikwete, mtu rahimu sana, aliamua kunyamaza kimya bila kuingilia kwa hoja kuwa hayo ni mambo ya ndani ya Zanzibar, kilichofanyika ni kwa Katiba ya JMT, ku ignore (kuyapuuza) mabadiliko hayo ya Katiba ya Zanzibar kwa katiba ya JMT kutofanyiwa mabadiliko hivyo mpaka leo, katiba ya Zanzibar haitambuliwi na katiba ya JMT, huku katiba ya JMT, ikiendelea kuitambua katiba ambayo imeishafutwa.

Katiba hiyo ya Zanzibar katika Ibara ya 26 inatamka kwamba Rais wa Zanzibar ni Mkuu wa Nchi ya Zanzibar Katiba ya Jamhuri ya Muungano katika Ibara ya 33(2) inatamka "Rais wa Jamhuri ya Muungano ndiye Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu". Hapa ni muendelezo wa Zanzibar kujitangaza kuwa ni nchi, na kumtangaza Rais wa Zanzibar kama mkuu wa nchi, wakati ukweli ni Tanzania ni nchi moja ya JMT, Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT, yenye utawala wake wa ndani.

Katiba ya Zanzibar haikuishia hapo, katika Ibara ya 2A inatamka kwamba "Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali, Rais aweza kuigawa Zanzibar katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi."

Masharti haya ni kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano Ibara ya 2(2) ambayo inatamka "Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Rais aweza kuigawa Jamhuri ya Muungano katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge: Isipokuwa kwamba Rais atashauriana kwanza na Rais wa Zanzibar kabla ya kuigawa Tanzania Zanzibar katika Mikoa,Wilaya au maeneo mengineyo."

Ibara hiyo inapoka madaraka ya rais wa JMT, kupoka madaraka ya rais ni kosa la uhaini!.

Katika Ibara ya 132 ya katiba ya Zanzibar, inatamka kwamba "Hakuna Sheria yoyote itakayopitishwa na Bunge la Muungano ambayo itatumika Zanzibar mpaka Sheria hiyo iwe ni kwa ajili ya mambo ya Muungano tu na ipitishwe kulingana na maelekezo yaliyo chini ya vifungu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Sheria kama hiyo lazima ipelekwe mbele ya Baraza la Wawakilishi na Waziri anayehusika.Ibara hii inaeleza zaidi, pale Sheria ndogo inapoundwa kwa mujibu wa uwezo uliowekwa chini ya kijifungu cha 132(1) na (2) itatumika tu pale itakapotimiza shuruti zote zilizowekwa kwa matumizi ya Sheria Mama kama ilivyoainishwa katika kifungu hiki"

Masharti haya ni kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano Ibara ya 64 ambayo inatamka kwamba Bunge la Jamhuri ya Muungano ndilo lenye mamlaka ya kutunga sheria kwa mambo ya Muungano (Bara na Zanzibar) na yasiyo ya Muungano ya Tanzania Bara. Ibara hiyo imepoka madaraka ya Bunge la JMT kutunga sheria za mambo ya muungano na kulifanya BLW ndilo lenye mamlaya ya kuu kuhusu muungano.

Katika Ibara ya 24(3) ya Katiba ya Zanzibar, "Rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu (Zanzibar) katika shauri lililofunguliwa dhidi ya masharti ya Sura hii ya Katiba yatasikilizwa na Mahakama Kuu (Zanzibar) mbele ya Majaji watatu, na uamuzi wao utakuwa ni wa mwisho na hautokatiwa rufaa kwenye Mahakama ya Rufaa ya Tanzania." Ibara hii ni kinyume cha Ibara ya 117(1) na (4) ambayo inatamka kwamba Mahakama ya Rufani ndiyo yenye Mamlaka ya juu ya kutoa haki nchini na uamuzi wake ni wa mwisho hivyo Mahakama Kuu ya Zanzibar, kupoka mamlaka ya Mahakama ya Rufani ya JMT na Jaji Mkuu wa Zanzibar kuwa ndie mkubwa kuliko Jaji Mkuu wa Tanzania.

Ukiondoa hiyo mikanganyiko ya katiba ya Zanzibar na katiba ya JMT, mabadiliko hayo ya katiba ya Zanzibar pia yameleta mambo mazuri, Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), kwa jina maarufu la GNU (Government og National Unity), hili ni jambo jema, kubwa, zuri na la kheri, japo ki protokali, serikali ya JMT inaitambua SUK na viongozi wake wanapewa protokali stahiki kitaifa na kimataifa, sasa ni muda muafaka kwa Katiba ya JMT, ama iitambue rasmi katiba ya Zanzibar, kwa kuifanyia marekebisho katiba ya JMT na kuuingiza SUK, au Zanzibar ilazimishwe kuuondoa huo utata wa Katiba ya Zanzibar kupoka mamlaka ya JMT, Rais, Bunge na Mahakama ili itambuliwe rasmi.

Hitimisho
Je Zanzibar Iadabishwe kwa kulazimishwa kuondoa ubatili wa Katiba yake unaokwenda kinyume na katiba ya JMT, ili katiba ya JMT, iitambue katiba ya Zanzibar, au kwa vile tunaiogopa sana, bora tuu tuendelea kumchelea huyu mwana kulia?

Kuna mambo mengi tuu ya Zanzibar, JMT inayachelea mwana kulia, moja la mfano ni lile la umeme, Wazanzibari wamekuwa wakitumia umeme wa Tanesco bila kulipia kwa muda mrefu, hali iliyopelekea kulimbikiza deni likawa kubwa la muda mrefu hadi kuwa halihimiliki, Tanesco wakatangaza kuikatia umeme Zanzibar, isipolipa!, rais wa Zanzibar akatangaza hatulipi, kama ni kutukatia umeme waache wakate, tutawasha vibatari na koroboi ndipo serikali ya JMT ikaingilia kati, ikawasamehe deni lote likafutwa. Hii maana yake wenzetu wametumia umeme wa bure!, sijawahi kusikia hata maramoja familia masikini za huku bara wanaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, wakisamehewa deni la umeme!, lakini wenzetu wamesamehewa!. huku ndiko ninakukuita kumchelea mwana kulia. Sasa kwenye hili la Katiba, je Zanzibar aadabishwe kwa kulazimishwa kuondoa huu ubatili wa katiba yake unaokwenda kinyume na katiba ya JMT, ili katiba ya JMT, iitambue rasmi katiba ya Zanzibar, au kwa vile tunaiogopa sana, Zanzibar kuiambia ukweli, ni bora tuu tuendelea kumchelea huyu mwana kulia?

Paskali
Mayala huu mjadala mbona ulishapita...au umesahau maelezo ya Kikwete Bungeni?
 
Back
Top Bottom