Tanzania Nchi 1 ya JMT, Zanzibar Kujiita Nchi, Sio Uhaini?. Zanzibar Iadabishwe Kuondoa Ubatili wa Katiba Yake ili Tuitambue au Tumchelee Mwana Kulia?

waliwahi kujiingiza OIC kinyemela ikagundulika, fasta wakachomolewa huko. Nchi za kiislam kama oman, UAE, yemen na misri labda zinaweza kuwa nyuma ya zanzibar kama ikiamua kujitoa kwa nguvu. mataifa ya magharibi kama marekani na uingereza wanaweza kujiingiza humo kuiondoa kwenye muungano. isingojwe ifike huko, bora ioneshwe mlango wa kutokea itoke kwa amani
 
Hayo mambo, classmate wako Tundu Lissu ameyaongea sana na kuyapigia kelele kwenye Bunge Maalumu la Katiba Mwaka 2014

Lakini akaishia kuitwa Msaliti, hana nidhamu n.k

Sio na Wazanzibar, bali na Sisi wenyewe wa Tanzania Bara ambao tumetulia wakati Nchi yetu inaliwa kimya kimya pamoja na kupotezwa

Mzanzibar ana haki ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini hakuna Mtanzania ana hiyo haki ya kugombea hata Udiwani hapo Zanzibar

Mzanzibar ana haki ya Kumiliki Ardhi Tanzania Bara, lakini Mimi ama wewe Mtanzania Bara haturuhusiwi Kumiliki hata eneo la kutosha kuchimba japo kaburi tu hapo Zanzibar

Anyways, tuwaache wenye mamlaka waendelee kutuendesha vile wapendavyo hadi Siku akili zikiturudia 🙌
 
Hongera Mayalla,
Linapokuja swala kwa maslahi ya Taifa, kweli unasismama kwa maslahi ya Taifa! Kuandika tu ulichoandika, huku sio nyuma ya keyboard, inahitaji ujasiri.

Zanzibr iwe mkoa tu kama DSM, Morogoro, Mwanza kama kweli tuna nia njema na nchi hii. Hivi unajua Mhe.SSH kuwa tu Rais wa JMT, ni hekima za hali ya juu sana. Huenda haya yasiwe hivyo, huko mbeleni, ni viongozi wa sasa yeye Mhe. Rais wa JMT na yule wa zanzibar, tena na Mwenyezi Mungu alivyowatega, ni wao waamue sasa, nchi ya Zenji ife kama Tanganyika ilivyokufa, JMT 🇹🇿 ishamiri. Kwa vizazi vyetu vya leo na vijavyo. Wasipo ngamua hitajio hilo, ipo siku haitakuwa ilivyo leo!
 
Iko vile Bandugu kwa sababu kama sio wakati huo basi ni wakati gani tena ???!!
😳🙌🤩😂😅 !
 
Tumeshachelewa, ndama kaota pembe tayari.
 
Tufanyeje ili na sisi tupate Tanganyika yetu kama Wazanzibari walivyo na Zanzibar yao?
 
Hili andiko lako lina muda mchache sana kutimia.
 
Hivi mnajua Zanzibar na tanganyika zipo kwenye muungano kwa hiyari??? Yani sio lazima kuwa na muungano!!!? Hapo kwenye zanzibar iadabishwe mnataka kuigeuza zanzibar kuwa sawa na labda arusha, gairo, au nyamagana kwamba ni kasehemu tu.

Mnasahau zanzibar nje ya muungano wanakiti chao umoja wa mataifa,
Zanzibar nje ya muungano wanatambulika kama taifa kamili kama rwanda, kenya, singapore na kadhalika.

Halafu sisi watanganyika tunaolilia utanganyika wetu adui yetu sio zanzibar wala wazanzibari, tena wala wazanzibari hawajawahi kutaka kuifuta tanganyika, ni sisi tanganyika ndio tumejifuta wenyewe.

Wezetu wazanzibari wamenyooka na wako sahihi hata kisheria kuwa kuna uzanzibari wao na kuna utanzania ni sisi huku wenyewe bila kutekenywa wala kupigwa dole ndio tumejifuta,

Hebu tuwapumzishe wazanzibari wa watu, sisi watu milioni 60 tunataka kuwabebesha zigo la lawama watu wasio fika milioni mbili, hebu na iwe aibu kwetu, tuwe na haya tujilaumu wenyewe
 

Nchi? Neno nchi kwa kimombo ni lipi?

Dubai kwa mfano wanajitambulishaje, wanajiitaje na sisi tunaitambus vp
 
Ni issue ya muda tu
 
Mleta mada na wachangiaji wote hadi sasa...kiwango chenu cha unafiki kwa hakika kinatisha. Juzi tu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, CCM inadaiwa kushinda kwa asilimia 99%!

Kwa kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania (JMT) ni ya CCM, serikali ya Zanzibar ni ya CCM na marais wa pande zote mbili wametokana na CCM, hilo dai la uhaini linakujaje hapo?

Nakiri wako binadamu wanaokula binadamu wenzao lakini...
 
Haya maswali muulize Mstaafu Kikwete yeye ndiye alibariki hicho walichofanya wazanzibari
 
Zanzibar kila siku ziendavyo inakua na kiburi juu ya Tanganyika (baba) katiba ya Warioba iludi mezani na iwe na serikali moja tu au tatu, vinginevyo ipo sababu kuu ya kufanya mahamuzi Magum kama Israel
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…