Tanzania nchi ya maajabu: Mjue Mtanzania wa kwanza kucheza kombe la Dunia Urusi 2018

Shukrani kwa hiyo Interview ...wabongo hatukeep time ndo la msingi hapo anasema ...Huku Ujeruman anakochezea mpira ukichelewa mazoezini unapigwa fine na uongozi wa club anasema......sasa hapa kuna Yanga na Simba mafaza......
 
ni mdanish huyo kaka tusidanganyane.
 
Asante Sana CCM kwa kutuonyesha Watanzania wanaocheza mpira Nje ya nchi! Ipo kwenye ilani ya uchaguzi
Kweli Tanzania nchi ya ajabu, sasa CCM imeingiaje hapa.
 
Sasa mtu anacheza timu ya taifa ya Denmark ila bado unasema ni mtanzania wakati.mwenzio alishajilipua uraia.

Usikute hata bongo mavumbini hapajui
huyo kazaliwa sio kujilipua...kila Mara anakuja Bongo especially Tanga anampenda sana bibi yake mzaa baba..mbona magazeti yalimuhoji alivyotua bongo
 
Kama kawaida Wabongo tusione kitu tunaanza dickriding!

The nigga donated sperm

The kid hadaiwi kitu na TZ!
 
Sijasoma Civics mimi sisi tulikuwa na soma linaitwa Siasa.......Huyo ni Mtanzania halisi udenimark wake ni kwenye taratibu za kwenye makaratasi
You are right and i was wrong mkuu, ni kweli kutokana na taratibu za nchi yetu the guy anasifa za kuwa mtanzania na ni mtanzania the rest ni siasa za kwenye makaratasi as you said mkuu.
Baada ya kupitia maandiko ya nchi yetu na haya ndio niliyoyapata.

URAIA WA TANZANIA

Masuala ya uraia nchini Tanzania yanasimamiwa na Sheria ya Uraia ya Tanzania ya mwaka 1995 Sura 357 kama ilivyorejewa mwaka 2002, pamoja na kanuni zake za mwaka 1997. Sheria hii imeanisha aina tatu za uraia wa Tanzania ambazo ni;
1. Uraia wa Tanzania kwa kuzaliwa
2. Uraia wa Tanzania kwa kurithi
3. Uraia wa Tanzania kwa Tajnisi au kujiandikisha.

URAIA WA TANZANIA KWA KURITHI.
Mtu aliyezaliwa nje ya Tanzania siku na baada ya Muungano atakuwa raia wa Tanzania kwa
kurithi endapo mzazi wake mmoja ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa au kuandikishwa/tajnisi. Ni vyema ieleweke kuwa mtu aliyezaliwa nje ya Tanzania hawezi kuwa raia wa Tanzania kwa kurithi iwapo baba/mama yake ni raia wa Tanzania kwa kurithi.
 
kwao hyo jamaa anaijua Handeni ya Tanga?
 
Watanzania kwa kulazimisha undugu. Hadi mnatia aibu.

Huyo sio Mtanzania.
 
Hata Rashford tuliambiwa Ni Mtanzania anaeitwa Rashidi. Watanzania Kwa Kupenda Vya Watu Hatuzidiwi.

Sasa Kama Baba Yake Mzazi Kaukana Utanzania akajibadilisha Mpaka Jina ili awe Na Jina la Kidenish la Paulsen na Kujivalisha Uraia Wa Denmark Yeye Mtoto atapataje Utanzania?
 
Obama ni Mmarekani Mwenye asili ya Africa kutoka nchi ya Kenya Lakini si mkenya same applied to Yusof Manji ni mtanzania mwenye asili ya Asia. Walance Karia ni mtanzania mwenye asili ya Somali. Ili uwe mtanzania lazima uwe na urai wa nchi moja. Yusuf Poulsen Angekuwa mtanzania asingecheza Timu ya taifa lingine Tanzania bado hatujawa na huo uraia wa nchi mbili. He is not totally TANZANIAN
 
Huyo dogo ni Mtanzania kwa asili na kamwe haitabadilika....hayo mengine na mautaratibu tu ya kwenye karatasi....huo ndo msingi wa mada yangu
 
Atakuwa na uraia wa nchi mbili labda.
Kwa Denmark hiyo inawezekana
Kali Ongala baba yake mtanzania mama yake MZUNGU mwingereza. alikuwa na uraia wa Tanzania na England alishindwa kucheza timu ya taifa kwa sababu sheria haikuruhusu uraia wa nchi mbili
Kally ni mwingereza
 
Sane na mane ni Senegal , Rinaldo ureno , pogba ni Guinea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…