East African
JF-Expert Member
- Nov 27, 2013
- 704
- 993
Ndug wana JF mimi kama mtanzania kwa elimu niliyoipata na uchunguzi wangu wa kina nimegundua yafuatayo kuhusu vita ya Tanzania na Uganda na ningependa wale wasiojua wayafahamu haya;-
Mara baada ya rais Obote kupinduliwa alikimbilia Tanzania ili apate hifadhi kutokana na urafiki mkubwa kati ya Nyerere na Obote. Mara baada ya kupata hifadhi hapa Tanzania inasemekana kuwa Mwl hakumpenda Idd Amini na kuamua kumsaidia Obote kurudi kwenye kiti chake.
Baada ya Idd Amini kuona vile akatangaza mgogoro na nchi yetu kwa kuwa tulikuwa tunataka kumpindua naye akaamua kujihami kwa kutoleana maneno makali na Mwl. Hiyo ndiyo ikawa mwanzo wa vita ya Tanzania na Uganda.
Lakini ikumbukwe pia baada ya vita kuanza kuna wanajeshi wa Uganda walimchukia Idd Amini na wakaamua kuiasi serikali na kusaidiana na majeshi ya Tanzania ili kumuondoa Idd Amini. Kitendo cha kuasi kwa wanajeshi wa Uganda kulisaidia Tanzania kumpiga Idd Amini kwa urahisi la sivyo ingechukua muda mrefu kumuondoa Idd Amini. Ikumbukwe kuwa wananchi wa Uganda hawakufurahishwa na utawala wa Idd Amini na ndiyo maana uasi ukatokea.
Pia ikumbukwe kuwa vita hiyo isingeweza kutokea kama Mwl asingetaka kumsaidia Obote. Ikumbukwe kuwa Idd Amini alimpindua Obote mwaka 1972 hivi na yeye akaondolewa 1979. Nasikitika kwa kuwa historia ya vita hii inapindishwa sana na kuonekana kuwa eti Idd Amini alitaka kuchukua ardhi yetu. wakati chanzo ni sisi watanzania wenyewe.
Tafadhali sikusema haya kwa kuwa namchukia Mwl ila naeleza kile ninachokifahamu.
R.I.P Mwl. Nyerere