Tanzania ni kilaza

Enzymes

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2013
Posts
4,332
Reaction score
3,013
The Africa Competitive Report 2013 (Pg 194) inaonesha Tanzania ni nchi ya 80, Uganda ni ya 69 na Kenya ni ya 37 katika UBORA WA ELIMU kati ya nchi 144. Mm kama mtanzania mwenzenu naskitika sana kuona JK akiendelea kuteua Mawaziri wasio kuwa na vyeti halisi katika sekta hii nyeti. Na mpangilio mbovu wa madaraja unao letwa ili kuficha udhaifu kwa lengo la kujijenga kisiasa huenda kujisafisha kwa lengo la uchaguzi ujao mwaka 2015.

Pia natumia mwanya huu kuondoa ukungu ulio tanda machoni mwa watu wakidhani elimu yetu (Tanzania) ni bora kuliko ya Uganda.

Utafiti pia unaonesha Tanzania ni kinara wa Matatizo kama : Rusha 16.3%, ukosefu wa mitaji au fedha za kuanzisha biashara 15.6% , Ukosefu wa miundombinu bora 10.8%, mfumko wa bei 10.7%, Urasimu wa vyombo vya serikali 8.0%, nk.
 
^^
Sijaelewa..Walipima Ubora wa elimu kwa kulizingatia vyeti vya Mawaziri?
^^
 

"utafiti" na "ripoti" yake unapofanywa na kuandikwa na Mnyarwanda unategemea nini?
 
Mkuu unaweza kusema wametumia kigezo gani
 
mKOLONI ALIPO ONDOKA NCHINI ALIACHA SHERIA YA KUWA . kILA MWALIMU LAZIMA APITIE CHUO CHA UALIMU NA KUPATA CHETI NDIPO AFUNDISHE. sasa hapa Tanzania Nyerer alifuta hilo mwaka 1977 ambapo alianzisha ualimu wa UPE kila dalasa la saba lazima afundishe bila kupitia chuoni, sasa hapo wewe unategemea nini? tena baada ya kugundua kuna uhaba wa vyuo vya ualimu na walimu nchi nzima, yeye alikwenda jenga jumba la mikutani Chimwaga kwa ajili ya mikutano ya chama la ghalama ya zaidi ya bilion za mabilion, wewe hapo unategemea nn?

Idadi ya wakuu wa wilaya wakati wa nyerere, karibia wote walikuwa darasa la saba waliohitimu Hombolo, chuo cha propaganda, sasa hapo wewe unategemea nn?

leo hii hakuna marekebisho yyte ktk elimu: shule zote za kata hazina zahanati, Libraly wala maabala, wewe unategemea nn?

Meya wa jiji la DSM anashindwa hata kupanda michikichi njia ya sama nujoma, nyerer rd, na kati kati ya posta mpya, wewe unategemea nn?

Polisi na usalama wa taifa wameshindwa kabisaa kutueleza wezi wa fedha zilizofichwa Uswiss mpaka leo, wewe unategemea nn?

shule za misisngi nchi nzima zinanuka vyoo, wala havina vyoo vya kuvuta mpaka leo, wewe unatgmea nn?
 
Tatizo siyo vyeti vya mawaziri but mfumo mzima wa elimu umeoza, na hizi sera chakavu za CCM ndo kwanza tunazidi kudidimia loh!
 

Sina uhakika sana unaposema elimu yetu (Tanzania) inazidiwa ubora na Uganda, ninavyojua mtu akifeli Tanzania anaenda Uganda kuendelea na masomo. Marafiki zangu walipata zero (currently Division 5) mwaka 2004 wakaenda Uganda wakaendelea na Form V kama kawaida. Pia nikiwa chuo (SUA) kuna washikaji kibao walikimbilia Uganda kumalizia Degree zao baada ya Ku-disco, Pia hata sasa hivi ukitaka kupata uhakika uliza mtu yoyote ambaye yupo hapo chuoni atakwambia watu wanavyokimbilia Uganda kumalizia course zao.

Inawezekana report hiyo ilijikita kwenye suala la mazingira ya usomaji kama kuwa na library, walimu wa kutosha, etc.. Lakini kwenye kumeza wa Tz bado tupo juu sema miaka ya hivi karibuni hawa ma-waziri wamekuja kutushusha kielimu kabsa.
 




Tatzo wabongo mmekariri bila kuwa na facts. Download Global or Africa Competitive report na ucheki kama Tanzania imewahi kuipita Uganda Kielimu. Ukumbuke hii report ina andaliwa na world Bank na sio kiasa tu ni nyanja zote hata za kiuchumi.
 




Tatzo wabongo mmekariri bila kuwa na facts. Download Global or Africa Competitive report na ucheki kama Tanzania imewahi kuipita Uganda Kielimu. Ukumbuke hii report ina andaliwa na world Bank na sio kisiasa tu ni nyanja zote hata za kiuchumi.
 

Yawezekana kuna mengine ya kweli katika maneno yako ila la mfumuko wa bei si tumeambiwa jana tu kuwa ni about 6%? Hiyo ya kwako si imepitwa na wakati jamaa? Halafu hakuna kitu kinaudhi kama hiyo headline yako!! Nina wasiwasi kama we kweli ni Mtanzania!!!
 


Mkuu hawa jamaa (BoT) huwa wana monthly report au Quarterly report ila wanavyo wasilisha, ni mfumko wa bei ya mazao ya vyakula, viwandani, nk ni wagumu sana kuwa wazi na General Inflation level. Kumbuka pia hawa majamaa wameajiriwa na JK , hivyo ku Cook figure ni kawaida ili kumfurahisha. Ukweli ni kwamba Tanzania haitafikia one digit Inflation ktk utawala wa JK, hii ilitokea tu wakati wa JKN na kaka Ben (hadi 5%) kwani kwa sasa soko ni la biashara holera holera na si biashara huria!!

Kuhusu Uraia wala usiwe na shaka ila ukweli lazima usemwe na Uongo uwekwe pembeni. Cheki mali asili tulizonazo na maendeleo tulio nayo kama si ukilaza ni nini?Cha mhimu base on facts and Ignore Porojo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…