Tanzania ni kubwa,ishi mahali popote ulipokuwa ukifanyia kazi kuliko kwenda kuishi kwenu,utadharirika!

TUKANA UONE

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2018
Posts
2,345
Reaction score
6,970
Je Wajua ya Kuwa Bugger Kwa Kiswahili fasaha uitwa "SANGWEJI ?"

Ndiyo,chukua hiyo kama ulikuwa haujui!

Kumekuwa na tatizo la waastafu wengi kupata shida kurudi mikoani,wilaya kwao kuanza maisha upya pindi wanapostaafu!

Tanzania yetu ni kubwa mno na hamna haja wastaafu kurudi mkoani kwenu kuanza upya!

Unakuta mtu kazaliwa mkoa wa Mbeya,na amekuwa mwalimu mkuu wa shule tofauti tofauti mkoani Kigoma,muda wote wa miaka 45 au 50 ya miaka yote Kigoma hakutaka kujenga mkoani Kigoma anaamua kurudi kujenga Mkoani Mbeya akiwa tayari umri umemtupa na hafahamiani na mtu yeyote Mbeya isipokuwa huko Kigoma,unajiuliza sababu ya yeye kupakimbia Kigoma ni ipi?,yaani uishi Kigoma miaka 40 halafu utegemee utapata Raha Mbeya Kwa miaka 10?,nani alikudanganya?

Unakuta hata hapo Mbeya hafahimiki na majirani zake,kila kitu Kibaya kikitokea watamuhisi yeye kwakuwa ni mpya kwenye hilo eneo!

Unakuta ni mtumishi kapangiwa kazi pale Wilayani Magu na yeye ni mzaliwa wa Lindi,kwanini usijenge Nyumba hapo Magu uishi na familia yako kuliko kutangatanga na uzee wote huo!,Unalazimisha ukajenge kwenu nani anayekufahamu huko Lindi?,mwisho wa siku unaenda kwenu Lindi kila mtu anakushangaa,huna mwenyeji Wala rafiki wa kupiga naye soga unaishia kujifungia ndani kwako kama mwanga!

Jengeni huko huko mnakopangiwa kazi kwasababu mnakutana na watu na wafanyakazi wenzenu Kwa muda mwingi,hivyo mnajua wapi pa kuanzia hata kama mkipata tatizo!

Hapa nazungumzia Kwa wafanyakazi wote ambao wanapangiwa Kituo Cha kazi Kwa miaka 3 na kuendelea kama wewe ni mfanyakazi wa serikali ambaye unafanya kazi Kwa kuhama hama,let's say kila baada ya miezi 3 au 4 unahama hii hoja haikuhusu,wewe angalia panapokufaa Jenga huko na anzisha familia!
 
Na hii si kwa wafanyakazi tu. Hata kwa wapambanaji. Ukitoka kwenu kwenda kupambana baada ya kipita miaka 20 watu waliopo kule kwenu 90% watakuwa hawakujui. Ni watoto waliozaliwa wakati unaondoka na wamekuwa wakubwa. Watakaokuwa wanakujua ni wale tu mliokuwa wote.... na wewe ni mtu wa kwenda na kukaa siku chache kisha kuondoka kurudi kupambana.
Mleta mada una point.
 
Wanatupunguzia gharama za kusafirisha maiti,ujue nini ,ukistaafu kuna nguvu ya uvutano zinakuvuta kwenu kwa asili,ili ukazikwe karibu na ancestors wako,sio kwamba wanapenda,tuwasamehe kwa hilo,hata wewe mtoa mada ukizeeka utajikuta nafsi inakuvuta kwenda kwenu
 
Mtu kwao na mwenda kwao si mtoro, nyumbani kuna raha hata kama ni kubaya, Mila na desturi hutofautiana kati ya jamii moja na nyingine, kuna baadhi ya mila zinaweza kua kero kwa mtu wa jamii nyingine, usukumani kwa mfano unaweza gongewa kengere saa 4 usiku kuna mkutano chini ya mbuyu, au umejichanganya umemega mpaka wa shamba wa jirani yako adhabu yake ni kuchapwa viboko, unaweza vumilia miaka 40 sababu ya kazi lakini huwezi vumilia miaka 10 kwakua upo huru,hayo na mambo mengine hufanya watu kukumbuka walikotoka, mtumishi anaweza kurudi kwao kwa kujenga taratibu taratibu na kurudi likizo angalaua mara moja kwa mwaka, wenyeweji ni walio karibu yako wewe, kusema unarudi kwenu ili kuwatafuta marafiki zako wa mliosoma nao shule ya msingi? waliorika lako ndio watakua marafiki zako na ulijenga nao ndio watakua majirani zako,
 
Wanatupunguzia gharama za kusafirisha maiti,ujue nini ,ukistaafu kuna nguvu ya uvutano zinakuvuta kwenu kwa asili,ili ukazikwe karibu na ancestors wako,sio kwamba wanapenda,tuwasamehe kwa hilo,hata wewe mtoa mada ukizeeka utajikuta nafsi inakuvuta kwenda kwenu
Kweli watu weusi tunasafari ndefu sana,utasikia nikifa nikazikwe kwetu...
 
Dk Livingstone alifia Africa akazikwa kwao ulaya sioni shida kuwa na makaburi ya ukoo,subiri uingie kwenye siasa uambiwe we mrundi tuonyeshe kaburi ka babu yako,ila kikubwa ni mambo ya spiritual ,nafsi inakuvuta kwenu
 
Hata nikae utawani miaka buku nikirudi nyumbani shangwe kama kawa tu

Naenjoy kilugha chetu, vyakula na matunda ya kwetu n.k aisee tujenge nyumbani kwetu huu utafutaji una mwisho wakati mwingine zari linatokea umezikwaa pesa mapema tu unastaafu unaenda kula mafyoksi na matoroja nyumbani kwa raha kabisa
 
Back
Top Bottom