Tanzania ni nchi ya kidikteta

Tony254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2017
Posts
16,017
Reaction score
16,431
Mimi kama Mkenya nahuzunika sana kuona kwamba tumezungukwa na nchi za kidikteta. Kenya is the only democracy in East Africa. Mkubwa wa Upinzani Freeman Mbowe na wafuaswi wake wamekamatwa usiku wa kuamkia jana na wanashikiliwa na polisi. Inakisiwa kwamba watashtakiwa kwa madai ya ugaidi. Yaani mnarudi nyuma ndugu zetu. Kushtaki Freeman Mbowe kwa shtaka la kigaidi inadhihirisha kwamba huko kwenu kuna udikteta wa hali ya juu hata kushinda Uganda.

 
Nonsense kwenye ranking ya democrasia Tanzania ipo mbele yenu hamna democrasia nyie mna ukabila na rushwa .
 
Noma sana na inahuzunisha kwa kweli, kuanzia Somalia kupitia Ethiopia, Uganda, Sudan Kusini mpaka Tanzania tumezungukwa na mataifa ya ajabu sana, hamna uvumilivu wowote.
Poleni sana, sidhani kama mama ameridhia haya yote.

Lakini mpaka polisi watumie neno "ugaidi" labda kunalo wanalolijua au wamegundua.....
 
Sasa kama chunguzi znaonesha kunamasuala anatakiwa kujibu au ametenda kosa asikamatwe ?
Au unafikiri wanasiasa wao hawafanyi makosa?
 
Sasa kama chunguzi znaonesha kunamasuala anatakiwa kujibu au ametenda kosa asikamatwe ?
Au unafikiri wanasiasa wao hawafanyi makosa?

Kama kweli kafanya kosa akamatwe, kila mmoja lazima awe chini ya utawala wa sheria, sipendi mambo ya umungu mtu, ila sasa hapo mumetaja kafanya ugaidi, jameni hicho sio kitu cha kutaja taja kiholela hivyo, ugaidi hukumu yake unanyongwa mazima mazima, natumai mko na sababu za msingi za kutaja tuhuma kama hizo.
 
Kunauwezekano jamaa alihsi kama anachunguzwa na siku zake znahesabika ndomana akaamua kujificha kwenye mwanvuli wa katiba mpya
Kama polisi wanamsingizia basi ukweli utajulikana lakini kitu cha kushangaza ni kauli ya makamu mwenyekiti wake ndugu Tundu znakautata kama ukizifikiria vizur
 
Samia anaweza kuwa dikteta katili zaidi kuliko wote east Africa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…