MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,565
- 843
- Thread starter
- #181
Nina maswali kuhusu Dr.Salim:Hivi amesha deliver nini hasa kwa taifa hili mpaka kuonekana anafaa sana kuwa Rais,mpaka Nyerere kumbembeleza mara kibao as if hakuna wengine capable kumshinda?
Kama Dr.Salim angeukwaa huo Urais tuseme 1985 au 1995 ama 2005,je bongo sasa tungekuwa tunacheza na GDP per capita ya Botswana,Namibia au hata Kenya ama tungekuwa kama Wasomali tu?
Inaelekea Dr.Salim ni arrogant na alijihisi kuwa yuko overqualified kwa nafasi ya Urais wa Tanzania au alikuwa hataki au hana nia hasa ya kuwa Rais wa Tanzania.
Kama alikuwa anajua kuwa Wazanzibari wenzake hawamtaki,iweje akatae Urais wa 'kupewa mezani' na Nyerere,kisha ghafla tu autake Urais huohuo 2005,wakati Nyerere ambaye angeweza kumbeba hakuwepo?
Naweza nikasahihishwa kwenye hili ila kwangu mimi naona CY ya Dr. Salim Ahmed Salim imeng'arishwa zaidi na vyeo alivyo shika badala ya nini alifanya katika hivyo vyeo.
Mfano Sokoine anakubwa kwa yale aliyo yafanya akiwa waziri mkuu nk. ila kwa Salim sioni hili. Pia kutokana na uelewa wangu Salim amelaumiwa sana na Watanzania wengi pale OAU kwa kuto kusaidia Watanzania kupata nafasi za kazi mbali mbali.
Nikisema kusaidia simaanishi kuwafanyia upendeleo bali inasemekana alikwenda a step ahead na kama kuhakikisha ana wazibia oppportunity Watanzania. Naomba nisahihishwe ikibidi.