Tanzania: Ni yapi yaliyojiri 1995?

Tatizo kubwa ambalo linaumiza nchi yetu ni mfumo wa kuwapata wale ambao wanasimama katika nafasi mbalimbali. Tunampata raisi si kwa sababu

yeye ni bora bali kwa sababu genge la watu fulani kwa pesa walizowaibia watanzania na kwa nia yakuonekana kwamba matakwa yao yanasimama

wamemtaka awe raisi. Hii inafanya tuwe na kuchagua raisi bora kati ya wengi waliohafifu. Its like trying to make sense out of nonsense! Matokeo yake

tunapata mtu bomu ambaye kwa sera za chama analazimika kutawala kwa miaka kumi! Imagine watu chini ya kumi wanaamua hatima ya Tanzania

for the next ten years! mfumo huu ndio uliopekea Mkapa 1995, JK 2005 and who knows!? (kama hatutakuwa makini) May be EL/Mwinyi/Nahodha

/Membe or Pinda 2015! Disastor!
 
Mkuu haya ya JK pale Monduli si wengi tunayafahamu mimi nikiwa mojawapo. Nitashukuru sana ukiweza kutuelimisha mimi na wengineo. Ahsante
 
Calnde you are right. Mfumo ni kila kitu katika nchi. Ndiyo ina dictate kila kinacho endelea kwenye nchi.
 

Nimekupata mkuu, kwamba ilikuwa ni propaganda machine dhidi ya Malima. Kama ni kweli habari hizo zilikuwa za uzushi, basi nasikitika sana kwani niliziamini.

Viva JF kwa kutuweka sawa na kurekebisha baadhi ya flaws kwenye historia ya Taifa letu. JF ni muhimu sana.
 
Dah binafsi nimejifunza mengi sana. Hivi hamna videos na pictures za uchaguzi wa mwaka huo kuanzia chaguzi ndani ya chama na kwenye chaguzi kuu? Wenzetu wana mtindo wa kudocument mambo kama haya. I have been thinking of making a documentary on the office of the presidency kuanzia Nyerere mpaka JK hapo Mungu atakapo mjalia kumaliza salama 2015.
 
Mwalimu alikua anaona mbali sema sis 2005 tukawa na mawazo ya hapa kwa hapa kama kuku
 
Mwalimu alikua anaona mbali sema sis 2005 tukawa na mawazo ya hapa kwa hapa kama kuku

Maneno yakisemwa yakapingwa na yakatokea ndiyo yana nguvu ya kihistoria. Kama tungefuata maneno ya Mwl. Nyerere leo hii wala tusingeona uzito wa maneno yake. Tungechukulia tu kama jambo la kawaida. Kila taifa changa lazima lipite mabonde kwanza kabla ya kufika kileleni. Labda kipindi hiki kitakumbukwa kama kipindi muhimu sana kwenye historia ya nchi yetu maana sasa hivi historia pekee tuliyo nayo ni uhuru wa Tanganyika na mapinduzi ya Zanzibar..
 
Niamini mkuu wangu, Hata kesho Regia Mrema akija gundua system ina abuse wanawake iwe ktk ajira au elimu na akasimama kulizungumzia ataonekana Mjinsia (sijui ndio hivyo inaitwa) Au mbunge yeyote mwanamme akisimama na kupinga viti maalum muda wote lazima atapachikwa - Ujinsia kwa sababu huwezi kuzungumzia vitu hivi bila watu kuitazama kwanza jinsia yako kisha wanaunganisha utetezi wa hoja nzima.

Labda niseme tu kwamba Mar. Malima kwa kutoelewa WATU na MAZINGIRA alokuwepo alifanya kosa kubwa sana kuandika ile barua kwa rais Mwinyi akiwa muislaam na akishirikisha viongozi wote waliomtangulia kitaifa na ktk wizara hiyo. Kuwashutumu watu kwa kosa la makusudi kutowapeleka waislaam na wanawake elimu ya juu ni shtaka zito sana ambalo pengine alihitaji muda na subira ktk uwasilishaji wa hoja nzima.

Miaka ya Nyerere na Mwinyi sote tunajua ilikuwa njaa kali, nafasi za ku advance zilikuwa za kugombania na kila mzazi alitaka mwanaye aendelee mbele kimasomo. Katika utafiti nilowahi kuufanya ilikuwa kitu kama asilimi 5 tu ya wanafunzi ndio walikuwa wakiendelea na masomo.. Kwa hiyo vijana wengi wa Masaki, O'bay, Sinza, Mbezi yaani kote sehemu za fridge open (happened to be Christians) walikuwa na majibu ya mitihani ama wazazi wao wako madarakani.

Kushinda darasa la saba na form 4 was a big deal wakati ule yaani wazazi wanaweza kutokula wakisikia umeshindwa..Ukweli ni kwamba haikuwa mpango wa serikali bali serikali ilishindwa kuzuia kama tunavyoshindwa leo na Ufisadi..
 
Mkuu Mkandara au mkuu yoyote yule mwingine, mwaka huo kulikua na mgombea yoyote kutoka Zanzibar? Ukiacha of coarse Salim A. Salim aliye kataa. Na je ilifikaje mpaka Omar Ali Juma akapewa ugombea mwenza? Maana huyu kabla hajafa alikua anaonekana ana nafasi kubwa sana ya kushinda 2005 haswa kama angepush "Ni zamu ya Zanzibar".
 
Hapana. Hapa nitakataa kabisa. Mkapa mwenyewe kaniambia kwa mdomo wake kwamba alipomfuata Mwalimu kuomba ushauri kuhusu baraza la mawaziri Mwalimu alikataa katakata akimwambia "it is your government. You choose the people you want to work with." Mwalimu hakuwa na usemi wowote hata kidogo katika uchaguzi wa mawaziri ya serikali ya Mkapa. Ila nasikia alishangaa aliposikia Mkapa amempa Lowassa wizara.
 
Mkapa alikuwa "lightweight" katika siasa za Tanzania. Pia hakuwa choice ya kwanza ya Mwalimu, na hilo atakumbusha kila anapopata nafasi. Mwalimu alitaka Salim achukue forms za urais 1995, lakini Salim akikumbuka jinsi alivyodhalilishwa na Wazanzibari 1985 alikuwa anasita akitaka "ateuliwe" Mwalimu akasema kuwa Salim anataka apewe kila kitu kwenye sahani. Waliomshawishi Mwalimu kumsapoti Mkapa alikuwa ni Butiku na afisa mmoja wa Kitanzania aliyekuwa benki ya dunia ambaye alikuwa na uhusiano mzuri na Mwalimu. So Mkapa was Mwalimu's second choice.

Lakini ukiangalia cv za Mkapa na Kikwete kufikia 1995 Kikwete was a featherweight. Hakuwa na accomplishment yoyote ya kujivunia wakati Mkapa alishawahi kuwa mhariri wa magazeti ya serikali, press secretary wa Mwalimu, Balozi, Waziri wa mambo ya nje, etc. etc. Kwa hiyo ile kauli kuwa Kikwete alikuwa bado hajakomaa ililenga kuonyesha hilo. Na hata sasa ukilinganisha utawala wa Mkapa na wa Kikwete and their accomplishments, kama Mkapa asingekuwa fisadi, he would be standing tall above them all.
 

Mimi kuna kitu kimoja kina nitatiza kuhusu Mkapa. Mimi naamini Nyerere hakua mtu wa kukurupuka. Kama alimchagua Mkapa naamini kabisa Nyerere alidhani anafaa. Je Mkapa ni alikua anaficha makucha yake au kweli alikuwa "Clean" akaja kubadilika baadae?
Up to the time Mkapa anaingia Ikulu hakuwa na mali. Nakumbuka alikuwa na Mercedes moja chakavu iliyokuwa ya ubalozi wetu Ujerumani.
So at that time the "clean label" suited him. It was after he was in Ikulu that he could not overcome the temptation to get rich.
 

Kwa hiyo mkuu pamoja na kuwa "second option" Nyerere alimuamini sana Mkapa kwa sababu kwa uelewa wangu (naomba kusahihishwa), Nyerere alikua too involved na serikali ya Mwinyi in terms of kuinfluence baraza na decision making. Je ni kweli hakumuamini Mwinyi (kwenye uwezo wa kuongoza) lakini akamuamini Mkapa? Au aliona alikua too involved na serikali ya Mwinyi akajifunza na kuamua kumuachia Mkapa maamuzi yote?

Ila kuna kingine kina nitatiza mkuu. Wengi wanadai Nyerere kumpenda Mkapa ni kwa sababu ya Ukatoliki wao. Sasa hawa watu wanaelezeaje kuwa first choice ya mzee alikua SALIMA AHMED SALIM?
 
Mkuu, si kweli kuwa Kikwete alijiandaa kuwa Rais, ila ni mtu mtu anayependa makuu hodari wa kujipendekeza ili apate kitu au aonekane Mr clean/ Mr Perfect. Kuwa juu ya wengine hata kama has nothing great to deliver.

Kwenye post za miaka ya nyuma waliandika hili alipokuwa chuoni tabia yake ilikuwaje. Angalia trend yake alipokuwa Monduli nini alifanya, nini kilichomwondoa huko kwa aibu. Nini kilimfanya agombane na Mwandosya pale Nishati na madini? Alipokuwa rais wa JMT nini alifanya kwa baraza lake na nini alichofanya kimataifa including AU? What about that move towards MO Ibrahim prize? Connect all those things then you can know what a kind of man is this.

Yes! Up to now his character has not fade.
 
Mkuu haya ya JK pale Monduli si wengi tunayafahamu mimi nikiwa mojawapo. Nitashukuru sana ukiweza kutuelimisha mimi na wengineo. Ahsante
Go for the past post /archived about Kikwete include that, Kikwete in Black and White
 
Binafsi sitausahau mchango Dr AL Mrema kwenye uchaguzi huu. Isingekuwa Wachagga kuuonyesha Uchagga wao kwa Mrema nchi ingekuwa nyingine sasa hivi. Hii CCM isiyosafishika tusingekuwa nayo sasa.
 

Mkuu unaweza kutupa kisummary ya vitu alivyo fanya chuo, Monduli, Nishati na Madini, hiyo ya Mo Ibrahim price na baraza lake? Ili kidogo tuone trend?
 
Binafsi sitausahau mchango Dr AL Mrema kwenye uchaguzi huu. Isingekuwa Wachagga kuuonyesha Uchagga wao kwa Mrema nchi ingekuwa nyingine sasa hivi. Hii CCM isiyosafishika tusingekuwa nayo sasa.

Naomba utufafanulie mkuu.
 
Naomba utufafanulie mkuu.
Mrema alikubalika Nchi nzima. Wizara ya Mambo ya Ndani ilikuwa imemjenga sana kwa jinsi alivyokuwa akishughulikia kero za Watanzania. Alifahamika na kukubalika zaidi kwa WATANZANIA kuliko wagombea wote wa CCM na vyama vingine. Wakati wa kampeni ndipo yakajitokeza makundi ya ajabu ya Kichagga yakichangishana fedha kwa wingi na kufanya mikutano yao wenyewe utadhani alitakiwa kuwa Rais wao peke yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…