Nilivyo kuwa nasikia kuwa ukiona vyaelea ujue vimeundwa, nimeamini! au usilolijua ni kama usiku wa giza, nimeamini!
Wadau hali inayoendea ya kundi moja kujihakikishia kuendelea kuwepo madarakani na kundi lingine kujihakikishia linashika madaraka na kuongeza nchi sio lelemama aisee!
Makundi haya yako tayari umoja, mshikamano na amani yetu kuiweka kando ili ndoto zao zifikiwe!
Yanayoendelea awamu hii siambiwi na mtu ila naona kwa macho yangu kupitia nafasi yangu, maana chaguzi zilizopita nilikuwa nasimuliwa!
Wahusika kwa nafasi zenu naomba tukumbushane, Tanzania ni yetu sote hakuna mgeni kutoka nje tunayepambana naye. Mdogo mtu yupo upande mwingine na kaka mtu mtu pia yupo upande mwingine pia, vivyo hiyo kwa wajomba, baba na watoto wao!
Tukumbuke pia kuwa hatuna Tanzania nyingine zaidi ya Tanzania iliyoasisiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwl J. K. Nyerere itasambaratishwa kwa tamaa ya madaraka, ubinafisi na makundi ya watu wenyewe malengo maovu wasio itakia mema nchi yetu na vizazi vilivyopo na vijavyo.
Kwakuwa wanaotaka kuendelea kushika dola na kwakuwa wanaotaka kushika dola wote ni watanzania wenzangu, kwa kuwa pia ndugu zangu mkae mkijua kuwa kura yangu kati yao au yenu nitaitoa tu kwa yule atakae nishawishi kwa sera zake za maendeleo, amani, mshikamano, n.k, na si kwa sababu nyingine yoyote.