Tanzania ni yetu sote! Tukikupa uongozi ukumbuke ni neema tu za Mungu

Tanzania ni yetu sote! Tukikupa uongozi ukumbuke ni neema tu za Mungu

Mbona umebadili gia angani? Hakuna dalili za uteuzi tena?
 
Ccm ndo wanajifanya tanzania ni yao peke yao.

Watanzania daini katiba mpya na tume huru ccm itoke vinginevyo mtapata tabu sana
 
Tanzania ni mali ya Watanzania wote pasipo kujali hali zao, itikadi za kisiasa na hata imani zao za kidini. Ni nchi ya matajiri na maskini, waliosoma na wasiosoma, wakulima na wafugaji, wafanyakazi na wafanyabiashara bila kujali rangi zao.

Kama Watanzania, tulipendelewa na Mwenyezi Mungu kuwa watanzania na kuwepo Tanzania kama ilivyo sasa. Naam! Hatupo hapa kwa bahati mbaya wala kwa hisani ya kundi fulani au jamii fulani. Kama Watanzania, hadhi yetu ya uraia ni moja; hawezi kutokea yeyote miongoni mwetu ama nje yetu kubatilisha uhalali wa Mtanzania yeyote kwa sababu iwayo yote.

Mfumo wa utawala wa nchi yetu ni lazima uwe ni ule ambao una ridhaa ya watanzania wenyewe. Hatuhitaji kuiga mfumo wa utawala wa Rwanda na Uganda kwakuwa Tanzania haikuumbwa ifanane na nchi hizo. Tanzania haijawahi kupigana vita vya ndani kama ilivyo kwa nchi hizo nilizozitaja hapo juu. Taifa halipaswi kuwa mali ya mtu mmoja au kikundi cha watu bali mali ya Watanzania wote. Utawala uliopo sasa unafanya mambo ambayo ukiyatazama ni kama vile nchi hii kimekabidhiwa kikundi cha Al-shabab kutawala. Matamko yanatolewa kila kiongozi ajisikiavyo, hakuna tathmini ya athari, mapokeo wala matokeo ya kauli hizo.

Ni wajibu wa kila raia mzalendo na mpenda amani ya nchi yetu kuyachukia mambo haya na kuyakemea! Tanzania yetu sote!
 
Unaonaje unaonewa lakini bado unakua ni mtu mwenye amani na mwenye tabasamu kuliko anaye kutesa.

Tanzania ni yetu sote, tulitoa mkoloni na tumebaki watanzania wenyewe.

Tujenge nchi, tuheshimu haki za wengine,

Hatuhitaji watawala, bali viongozi wenye maono ya kumfanya kila Mtanzania aifurahie nchi yake.

Madaraka ni kama koti la kuazima, ipo siku adui yako ataliazima pia.

Watanzania wote bila kujali vyama vyetu tuonane mahakamani.

Sura mpya ya siasa za Tanzania ni leo.

20200310_080543.jpeg
20200310_063326.jpeg
20200309_203105.jpeg
FB_IMG_1583674992342.jpeg
FB_IMG_1583673551276.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo utafiti ule ulikuwa wa kweli? Kwamba upinzani unaungwa mkono na warembo na watanashati walioelimika¡
Huku tawala wakiungwa mkono na wazee na vijana waliokimbia shule na maprofessor, maDr wenye njaa kali?
 
Ndio utafiti ulivyosema. Huwezi kupinga utafiti
 
S
Unaonaje unaonewa lakini bado unakua ni mtu mwenye amani na mwenye tabasamu kuliko anaye kutesa.

Tanzania ni yetu sote, tulitoa mkoloni na tumebaki watanzania wenyewe.

Tujenge nchi, tuheshimu haki za wengine,

Hatuhitaji watawala, bali viongozi wenye maono ya kumfanya kila Mtanzania aifurahie nchi yake.

Madaraka ni kama koti la kuazima, ipo siku adui yako ataliazima pia.

Watanzania wote bila kujali vyama vyetu tuonane mahakamani.

Sura mpya ya siasa za Tanzania ni leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa
 
Hongereni sana, CDM sasa ni taasisi kubwa. Kuna wajinga wachache wanataka kuturudisha nyuma kwa tamaa za kutaka ufalme Tanzania, msikatishwe tamaa komaeni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom