Nebuchadinezzer
JF-Expert Member
- Oct 1, 2018
- 1,403
- 2,546
Nimefika Tabora ndugu zangu, nimelia sana baada ya kukumbuka kuwa JPM hayupo tena duniani.
Magufuli, Magufuli, Magufuli, nimekuita mara tatu, najua hunisikii, ila Mungu atakulipa siku ya ufufuo. Ni miaka 60 tangu tupate uhuru, mkoa wa Tabora ulisahaulika sana...hasahasa kwenye huduma muhimu za kijamii.
Awamu zote kabla ya JPM zilipita,bila kuwaletea wana Tabora maji safi na salama. JPM aliwahi kusema, ukiomba mkopo ili upeleke huduma ya maji Tabora, wahisani wanakataa.... JPM aliamua kutumia hela anayokusanya (Kodi) kupeleka maji katika mkoa mkubwa wenye historia iliyotukuka.
Kilichoniliza sio JPM kufa, wala kuleta maji Tabora. Kilichoniliza, kuna bibi mmoja, aliniomba hela 2,000...nikasita kumpatia maana anaonekana ni mlevi. Mimi msabato, ni makosa kumpatia mtu hela akanunue kitu kitakachomuangamiza.
Nikamuuliza ya nini 2000, akanambia "Mjukuu wangu, hii naenda kulipia mkopo wa bomba la maji" Nilishituka, ikabidi nimuite dogo mmoja, alikuwa anapita, nikamuuliza kama kuna mikopo ya hivyo.
Dogo akanambia baada ya maji kufika wilaya ya nzega kipindi cha JPM, changamoto ilikuwa wananchi wengi hawakuwa na uwezo wa kuvuta mabomba ya maji kutoka ziwa Viktoria. Serikali ya wanyonge, kupitia rais Magufuli akatoa order, kila asiyenauwezo wa kuvuta bomba la maji, atakopeshwa, atakuwa analipa 2000 kila wiki mpaka itakapo timia 40,000.
Bibi yule nilimpa 2000. Sasa leo Napita zangu mitaa ile yule bibi ananiletea risti inayodhibitisha kalipia maji. Nilishangaa sana. Nilimpa 20,000 ili akalipe deni lote. Baada ya kufika, napolalaga, nilianza kulia baada ya kukumbuka kuwa JPM hayupo tena duniani.
Tabora nayoifahamu mimi, leo ndoo mbili shilingi 50? Miaka 60 bila maji, Magufuli akaleta maji.
AsanteMagufuli- Kweli vizuri havidumu