Tanzania nzima inaweza msahau Hayati Magufuli ila sio Tabora

Sasa wewe hujui maendeleo hatua?
Kama Magulfuli alipeleka maji Tabora kuna walioyafikisha shinyanga.
Ina maana mikoa yote nchi hii ilikuwa haina maji katika tawala zilizopita?

Lia rais kuna mahali anaposogeza maji, umeme, barabara, etc
 
Tuondolee upumbavu wako hapa!!!

 
Mkuu Nebuchadinezzer, kila Rais ailyepata kuiongoza nchi yetu ana mazuri yake kutokana na fursa na changamoto za wakati alizokutana nazo. Nyerere hakuwa na wataalamu wa kutosha wala hakuchimba madini mengi isipokuwa almasi lakini aliweza kufanya mazuri yake.

Baada ya uchumi kuvurugwa na vita vya Kagera na anguko la ukomonisti duniani, Mzee Mwinyi bado aliweza kusimama imara kwa nafasi yake kwa kukubaliana na sera za uchumi huria.

Mzee Mkapa na Mzee Kikwete walinufaika sana na sera za uchumi huria. Mbali ya kubinafsishwa na kuuzwa kwa makampuni ya umma, bado marais hawa ndio waliweza kunufaika na fursa na faida zitokanazo na uchimbaji wa gesi na madini. Hapa ndipo nchi ilipoanza kupata uwezo wa kuendeleza miundombinu mingi iliyokuwa katika "blue prints" za awamu zilizopita.

Magufuli amekuta kila kitu kipo sawa, alikuta nchi ina fedha na pia inakopesheka na kwa kweli alikopa na kukomba kila kitu [emoji849][emoji51] Aliendeleza tu yale yaliyokuwa yamepangwa kufanyika. Tatizo lake kubwa alitaka kwa makusudi kufunika yaliyofanywa na wenzake, na alifanya hivyo kwa ajili kiki na kupenda sifa ambazo hakustahili kuzipata.

Nchi yetu nikiifananisha na nyumba, ujenzi wake ulianza hata kabla ya Tanganyika na Zanzibar kuwa nchi huru. Nathubutu kusema wale machifu wa awali ndiyo walianza kujenga msingi wa nyumba yetu ijapokuwa historia haiwasemi kwa uwazi.

Kwa upande wa Nyerere aliifikisha katika lenta na kupandisha kozi kadhaa juu yake. Mzee Mwinyi aliweka mbao za kupaua, Mzee Mkapa alipaua nyumba, Kikwete alianza kazi ya "finishing" ambayo iliendelezwa na Magufuli na hata sasa inaendelezwa na Mama SSH.

Je! Sasa ni kwa nini Magufuli pekee atambulike ndiye aliyeijenga nyumba Tanzania na wala si mtu mwingine!? Lazima kuna tatizo kubwa sehemu fulani.
 
Unadhani Ujinga wako Umetoa Msaada gani Mkubwa zaidi?

Note;
Ignorance= Ujinga
 
Mbona huo mladi hulizinduliwa na JK na waziri wa maji kipindi hicho Jumanne maghembe pale uwanja wa Chipukizi pale duka la vitabu TMP,

Au mleta post ulikuwa bado tumboni hujazaliwa?
Acha kututanganya,Sisi watu wazima na wenye akili timamu tuna kumbukumbu.
 
Tofautisha kati ya NHIF ya JPM na ile ya JK na watangulizi wake, leo jitu linaongezewa kalaki tu linapiga kelele kama zuzu linasahau kila kitu. Wabongo ni bongolala kweli
 
Ishukuru CCM kwa kukufanya Masikini, na kukupa Elimu ndogo, ikakunyima exposure basi unaridhika na mambo madogo
 
Ujinga ni kipaji chako! Uchumi wa kati umefikiwa kwa Magufuli kupora fedha za watu benki, fedha ambazo serikali inashindwa kuzirejesha kwa wenyewe baada ya Samia kubaini uporaji mkubwa uliofanywa na mtangulizi wake.

Sasa nioneshe uchumi wa kati!
 
Hata Sepp Blatter alipendwa sana huku afrika lakini wazungu wakamla kichwa, sasa utaona wazungu wanatumia vigezo tofauti kupima performance ya mtu ukilinganisha na mtu meusi, mtu mweusi ukimpa mlo atakuimbia mapambio hadi unaingia kaburini hata kama huko kwingine utafanya ukatili usiomithilika.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…