Tanzania nzima inaweza msahau Hayati Magufuli ila sio Tabora

Kwanini usimshukuru Lowassa ambae alienda hadi Misri kugombana na waarabu waliokuwa hawataki watanzania tusitumie maji ya ziwa Victoria. Akawaambia Tanzania haitambui mikataba ya mkoloni. Akaahidi kuyafikisha maji Dodoma... Hawa unaowasifia wanatekeleza mawazo ya watangulizi wao. Huna haja ya kulia 😂😂
 
Uchumi wa kati ambao zaidi ya asilimia 70 ya vijana hawana ajira? Wafanyakazi zaidi ya miaka 5 hawajaongezewa mishahara? Wanafunzi wanasomea chini ya miti na wanakaa chini? Uchumi unakua kwa 4%? Watu wanakula mlo mmoja kwa siku? Unajua uchumi wa kati wewe au unaropoka tu? Idiot
 
Huu ndio wimbo uliopo ,

Hao walioandaa hiyo mipango kwanini hawakuitekeleza wao??
Utekelezaji ulikuwa unaendelea, awamu ya kwanza maji yamefika Shinyanga na Kahama awamu ya pili yamefika Tabora, Nzega na Igunga awamu ya tatu yatafika Singida na Dodoma.
 
Magufuli anachukiwa na watu wachache sana hapa duniani, niamini mimi bro. Fanya research mkuu. Wanaomchukia ni kikundi cha watu wachache sana ambao wako JF, twitter na Ufipa basi.
Uko sahihi mkuu.Ukiingia hiyo mitandao ndio kuna magenge yasiyompenda Magufuli
 
Waliotumbuliwa na Magufuli pamoja na magenge ya chadema yatakupinga na kukukashfu

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 
Huu mradi uliasisiwa na kujengwa enzi za Benjamin Mkapa na sii mwendazake, yeye alikamilisha tu. Sifa zimwendee Rais Benjamin Mkapa aliepambana na Wamisri waliokuwa hawataki tuchukue maji ziwa Victoria na kuzunguka dunia nzima tusipate mkopo wa kujenga. Na Rais Benjamin Mkapa akaamua kuujenga kwa fedha za ndani. Hongera Hayati Mkapa.
 
Kumbe siyo mbowe aliyeukamilisha? Nilijua ni mbowe
 
Kuna wa kumsahau JPM basi....! Ni lini wachawi umekuta wakiwa wanapendana mchana bana?

Unachokiona kwa baadhi ya watanzania kinaendana tu walivyo wachawi kutopendana mchana, lakini usiku wanacheza pamoja

Asiyesema Mchana kwamba JPM kafanya makubwa katika nchi hii, atasema usiku,

kilichopo ni unafiki tupu, na unafiki haudumu
 
Akili yako ndogo sana mkuu...kuwa na wazo ni moja, kitekeleza ni 100
 
Kwani sisi ndio tulisema tumeingia uchumi wa kati? Si ni World Bank? Ungewauliza hao world bank, nadhani ungepata majibu sahihi
 
Utekelezaji ulikuwa unaendelea, awamu ya kwanza maji yamefika Shinyanga na Kahama awamu ya pili yamefika Tabora, Nzega na Igunga awamu ya tatu yatafika Singida na Dodoma.
Singida Maji yalikuwepo kabla ya Tabora...usikariri mkuu
 
Mwaka gani mradi wa maji Tabora umejengwa...acha roporopo mkuu.
 
Miaka 60 ya utawala wa chama chake watu hawana maji. Na yanapoletwa hawana 2000 za kila wiki ili waunganishiwe maji.
Miaka 60 ya kujitawala mwananchi anaona ni ajabu kupata maji.
Tatizo ni kubwa kuliko tunavyofikiria.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…