Watanzania poleni sana kwa msiba huu mkubwa uliotuelemea. Wengi tulimpenda sana rais wetu kutokana na mazuri mengi aliyotufanyia.
Mengi yamesemwa na sina lengo la kuyarudia. Lengo la hii thread ni kuhoji ukimya wa kwaya ya TOT ambapo nakumbuka wakati wa msiba wa mzee wetu Rais Mstaafu Mkapa walitoa wimbo maalumu tena muda mfupi baada ya tangazo la kifo chake.
Kwenye msiba wa Baba Magufuli naona Msechu ndiye amejikongoja na kutoa wimbo dakika chache baada ya Rais Samia Suluhu kutangazia Taifa kifo cha JPM.
Kulikoni?
Mlioko karibu na TOT tujuzeni kinachojiri au kwaya imesambaratika?
Mara ya mwisho nawasikia wanaongelewa kabla ya wewe kuwaulizia Dr. Bashiru alisema watawatumia kwenye kampeni pamoja na nyimbo za mazumari na ngoma sema sijui nini kiliwakuta hatukuwaona
Dah! Ile TOT ya Captain John Komba (RIP) enzi zile ilikuwa ni nyoko! Jamaa alikuwa na kipaji cha uimbaji aisee! Hasa wa nyimbo zenye maudhui ya kwaya!!!
Yaani ule mwaka 1999 wakati wa kifo cha mwalimu Nyerere, unaweza ukadhani labda alijulishwa mapema kama kuna kifo! Maana nyimbo zake zote zilienda shule na zilikuwa zinasikilizika! Achilia mbali zile alizo zitunga kwa ajili ya kampeni za chama chake cha CCM!