Tanzania orders 1305 cows from Kenya sold

Huyo hakimu aliyetoa hii hukumu ANAJUA SHERIA ILA HANA BUSARA! That's all I can say for now. Unahukumuje Wakenya watatu kwa kuvuka mpaka kinyemela ihali kuna Watanzania elfu tano ambao wamevuka mpaka kinyemela (on the very same day) na wakati unatoa hukumu yako unajua kabisa kuwa raia wako elfu tano na ushehe wametenda kosa kama hilo unalolihukumu?
All in all tusijijengee chuki baina yetu na majirani zetu. Tusilifanye taifa letu lichukiwe na mtaifa mengine mithili ya North Korea. Tanzania imejijengea heshima kama nchi iliyopigania uhuru wa mataifa mengine barani Afrika. We have to treasure that... Isn't it?
 
Kila mtu anatakiwa kuwa na identity. Kuwa mpakani hakumaanishi identity is not something of a concern. Kwa upande mwingine kufuga kwa aina yao kwa sasa hailipi
 
Ndio maana Mwl. Nyerere alihimiza kuunganishwa kwa EA tuwe na nchi moja lakini Kenya mkaona ni heri kuheshimu matakwa ya wazungu.
 
Reactions: Oii
Mkuu unazeeka na kumbukumbu kupoteza.
Issue ya juzijuzi ya
Wasomali wa Loliondo, leo imekuwa issue ya miaka ya 80 kweli!
 
Reactions: Oii
Nina imani pande zote mbili zitatumia busara kulimaliza swala hili pasipo kuzua taharuki .....!
 
Busara ni muhimu zaidi kuuza hakuleti mahusiano mema hela wapigwe faini kesho zetu zimekamatwa kwao hapo vip. Pia muunganiko wa mipakani ni wa asili kutenganisha kisiasa ni ngumu.
 
Hii ni kulazimisha ubaya bila sababu.

Hivi hakuna suluhu nyingine zaidi ya kuuza ng'ombe wa jirani zetu kibabe?

Siungi mkono suala hili.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] saiyo jeshi litakua limeweka mikono mfukoni au kiunoni? Kawaite waje kuwasaidia wenzao waone fire
 
Kweli hata mimi Nakumbuka sana wale wasomali walikua wakisumbua sana mpaka Mabasi ya abiria wanawaibia ila sijui waliyeyukia wapi baada ya jwtz kutuma vijana wake?

Ni kama kibiti wanavyouwawa mpaka jana waarabu watatu wamekula shaba walikua na mabom na silaha police wamewaulia mbali
 
Reactions: Oii
Maneno matupu hayavunji mfupa kama nyie wamewashinda waambie wajichanganye Tanzania, we do not entertain none
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] those are just toys and we have them in tons
 
Sasa huwezi halalisha kosa kisa kuna mwingine ametenda kosa na hatua hazikuchukuliwa, haya mambo yapo kisheria ndio mana mahakamani imeamua sio swala la mitaani
 
Kaka kwasababu umeingiza neno busara, kwamba unadhani hakimu hakutumia busara, hapo umetumia uhuru wako wa kutoa maoni kama raia wengine, hupaswi kushutumiwa wala kulaumiwa, swali ni je sheria inasemaje katika hilo?, kwa sababu hakimu lazima atumie sheria katika kutoa maamuzi yake, ili kesho na keshokutwa akiulizwa kwanini alifikia maamuzi hayo, aweze kuwa na kimbilio, akisema alitumia busara tu na kupindisha sheria, sijui kama wanasheria walio wengi watamuelewa, kwa sababu busara au si busara inategemeana na mambo mengi sana
 
Busara ni muhimu zaidi kuuza hakuleti mahusiano mema hela wapigwe faini kesho zetu zimekamatwa kwao hapo vip. Pia muunganiko wa mipakani ni wa asili kutenganisha kisiasa ni ngumu.
Mipaka ipo kisheria sio kiasili huwezi kuingiza mifugo yako Kenya na Kenya wakakuchekea tu soma sheria za mipaka
 
Hii ni kulazimisha ubaya bila sababu.

Hivi hakuna suluhu nyingine zaidi ya kuuza ng'ombe wa jirani zetu kibabe?

Siungi mkono suala hili.
Hata hivyo huna nafasi kwenye hili ndio mana wakapeleka mahakamani hawakuleta kwako hiyo sio kazi yako
 
Mkuu, nakuelewa. Sources ya sheria za Tanzania zimegawanyika katika mafungu kadhaa. Moja ni zile ordinances, yani sheria tulizorithi kutoka kwa Muingereza za kabla ya mwaka 1920. Lakini pia kuna sheria zinaitwa customary laws. Hizi ni sheria zilizojengeka kutokana na mazoea fulani.
Sasa kama kumekuwa na mazoea ya watu wa mipakani kuvuka mipaka bila kufuata taratibu na hakuna mtu ambaye aliwahi kushtakiwa kwa kosa hilo, ina maana customary laws zinaruhusu watu wa mipakani kuvuka mipaka bila kufuata formality.
Muulize huyo 'hakimu wako' kuhusu customary laws naye atakuhadithia maana wanasheria wooote wanafahamu juu ya uwepo wa 'customary laws'...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…