kuna kitu lazima tuwe sensitive, haya mambo ya mikataba sio mambo ya siasa ni mambo ya kitaalamu kwanza na siasa inafata baadaye, naomba nizungumzie kama ifuatavyo
tunavyozungumzia natural resources formation yake si mara zote iko hivyohivyo kwa maana hiyo hata dhahabu iliyopo ardhini haifanani kwa jinsi ilivyoform na pia haiwezi kufanana jinsi ya kuichukua (Mining)
sasa katika mikataba lazima uwashirikishe wataalamu waangalie ile dhahabu ni ya aina gani na kuna tonnage( reserve) kiasi gani, na njia gani ya ku-mine (underground/open cast)
baada ya kupata gharama iliyopo plus gharama ya utafiti (Exploration) ndio watu wanakaa mezani na kuangalia serikali ipate ngapi kwani kwa sababu kama madini yapo Tanzania automatically serikali inakuwa na 50%, sasa hii 50% ya serikali inapungua taratibu kutokana na gharama za utafiti na uendeshaji wa mgodi, lakini pamoja na hayo yote serikali aiwezi kuwa chini ya 35%
mfano ni huu
kuna mgodi mmoja wa barrick unaitwa Tulawaka Gold mine Upo Biharamulo/Chato Disrtict, kilichotokea hapo ni kwamba kulikuwa na kampuni (MDN) inahodhi hayo maeneo lakini fungu lao lilikuwa dogo, barrick walivyokuja na kuona potential ya area wakaingia ubiya na na hao Jamaa(MDN) , MDN 30% na Barrick 70%, sasa angalia jamaa kuhodhi maeneo tu wanapata 30% na walikuwa wanalipa serikalini 2500$ kwa kuhodhi hivyo viwanja kwa mwaka,
swali inakuaje mtu aliyehodhi viwanja aweze kupata 30% na serikali mwenye maeneo hayupo kaibsa kwenye share,
mfano wa pili angalia hii kampuni ya almasi De Beers, hii kampuni ipo kusini mwa afrika, Bot,Nab,Swazi. Leth, RSA, lakini kote huko wanafanya mining na hizo nchi zote zinapata more than30% na kweli inalipwa lakini kampuni hiyohiyo hapa Tanzania hawezi kufanya kama hivyo pale Williamson Diamond, habari za pale NI WIZI MTUPU
hapa point inakuja palepale kwamba huwezi kuweka mikataba bila kuwashirikisha wataalamu