Tanzania Premier League: Simba SC 0 - 0 Lipuli FC zatoshana nguvu

Dakika 90' za mchezo wa ligi kuu TPL kuanza hivi punde.

Naaaaaaaam mpira umeanza uwanja wa Taifa.

Simba SC 0-0 Lipuli FC
 
04' Shuti la John Bocco lapanguliwa na golikipa wa Lipuli..ilikuwa hatari sana
 
07' Jonh Bocco kwa mara nyingine anakosa bao baada ya shuti lake kudakwa na golikipa..
 
Paul anaingia kwenye lango la Simba anapiga..Lakini mpira unatoka nje na kuwa gooal kick

18' Simba SC 0-0 Lipuli FC
 
25' Simba wanajaribu kujenga mashambulizi lakini bado hawajaweza kuona lango
 
28' Lipuli wanakosa bao la wazi, ilikuwa ni nafasi nzuri kuandika bao baada beki Bukaba kupokonywa mpira na shuti la mchezaji wa Lipuli kupanguliwa na Manula
 
30' Nafasi tena kwa Lipuli..goo laaaaa, golikipa Aishi anafanya kazi ya ziada kuokoa bao
 
Bocoo lakini golikipa anafika na kuucheza mpira nje ya 18

Ni faulo kuelekea Lipuli
 
Kichuyaa anapiga...Kagereeee anapiga kichwa lakini mpira unaokolewa.
 
40' Paul Bukaba anakwenda kwenye benchi anaingia James Kotei upande wa Simba

Simba SC 0-0 Lipuli FC
 
45+3' Wakati wowote mpira utakuwa ni mapumziko

Naaaaaaaam kipindi cha kwanza mpira kati ya Simba na Lipuli zimekamilika ambapo timu zote zinatoka bila kwa bila

Simba SC 0-0 Lipuli FC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…