Tanzania Premier League 'TPL' : Mabingwa watetezi Simba waichapa Prisons kwa goli 1 - 0 katika uwanja wa Sokoine Mbeya

Tanzania Premier League 'TPL' : Mabingwa watetezi Simba waichapa Prisons kwa goli 1 - 0 katika uwanja wa Sokoine Mbeya

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania TPL kuendelea kupigwa leo Mei 5, 2019 kunako dimba la Sokoine mkoani Mbeya ambapo Tanzania Prisons wanatarajia kupepetana na Simba SC.

Mechi inatarajia kuwa kali na ya vuta nikuvute kwa muda wote wa dakika tisini, hasa ukizingatia Tanzania Prisons wametoka kupoteza mchezo wao uliopita huku Simba SC wakiibuka na ushindi katika mchezo wao uliopita.

Je Tanzania Prisons watakubali kupoteza michezo miwili mfululizo au Simba ndio watakubali kuziacha alama tatu muhimu ambazo zitaweza kuongeza mbio zake za kutetea ubingwa.?

Kumbuka mechi ni saa kumi kamili jioni

••••••=====•••

Wakati wowote mpira utaanza uwanja wa Sokoine...!

Naaaaaam mpira umeanza kunako uwanja Sokoine mjini Mbeya dakika tisini za mchezo wa Ligi Kuu Tanzania.

Tanzania Prisons 0-0 Simba SC

IMG_20190505_144239_608.jpeg
IMG_20190505_144334_980.jpeg


Mpira uko sawa kwa pande zote kwa mashambulizi ya zamu..Lakini Simba wana nafasi zaidi kuona lango mapema..!

5' Tanzania Prisons 0-1 Simba uwanja wa Sokoine..!

Simba wazidisha mashambulizi lakini Prisons wanakaa sawa kwa kuokoa

11' Gooooooooooooal gooooooooal Emmanuel Okwii anaipatia Simba bao la kwanza.

Baada kuwa nyuma kwa bao moja Prisons wanajitahi kutafuta bao la kusawazisha.

20' Tanzania Prisons 0-1 Simba SC

Kutoka uwanja wa Sokoine, Mbeya mchezo wa TPL, timu zinapambana kutafuta matokeo ya ushindi..Simba wanashambulia kuliko Prisons

30' Tanzania Prisons 0-1 Simba SC

Zimebakia dakika 15' kuelekea mapumziko ambapo Simba wako mbele ya bao moja.

Naaaam dakika 45 za awali zimekamilika ambapo Simba wanatoka wakiwa mbele ya bao moja

Tanzania Prisons 0-1 Simba SC

•••••Kipindi cha pili mchezo wa TPL kimeanza uwanja Sokoine..

••••Mpira umemalizika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya ambapo Simba wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao moja kwa yai.

Bao la Simba liliwekwa kimiani na Emmanuel Okwiii

Tanzania Prisons 0-1 Simba SC
 
Naaaaam mpira umeanza kwa mashambulizi ya pande zote za timu..TPL na sasa ni muda wa dakika ya

5' Tanzania Prisons 0-0 Simba SC
 
Back
Top Bottom