Tanzania Prisons na Singida Big Stars zafungiwa kusajili Ligi Kuu

Tanzania Prisons na Singida Big Stars zafungiwa kusajili Ligi Kuu

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imezifungia kusajili klabu za Ligi Kuu ya NBC za Tanzania Prisons na Singida Big Stars kwa kosa la kusajili wachezaji wenye mikataba na klabu zingine.

Uamuzi wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji umefanywa kwa kuzingatia Kanuni ya 47(21) ya Ligi Kuu baada ya kuzikuta na kosa hilo. Adhabu hiyo ni kwa dirisha moja la usajili.

Tanzania Prisons ilimsajili kipa Musa Mbise wa Coastal Union wakati ikifahamu kuwa bado ana mkataba na klabu hiyo. Nayo Singida Big Stars ilimsainisha mkataba kipa Metacha Mnata huku akiwa bado ana mkataba na klabu ya Polisi Tanzania.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imezikumbusha klabu zote nchini kuwa usajili wa wachezaji unafanywa kwa kuzingatia kanuni, na ambazo zitakiuka kanuni zitachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni.

1E92643B-97D6-448E-8868-99A4D844D7CC.jpeg
 
Je, iliyomchukua Kocha wa Coastal Union?

Au Kocha hakua na mkataba?
 
Sasa TFF waliwapaje leseni za kucheza timu zao mpya huku wakijua wana mikataba?
TFF ya awamu hii ni majanga!! Yaani mtu anaweza kufikiri hao walinda mlango labda walitoroka nchini Somalia, na kuja kusajiliwa na hivyo vilabu kwa njia ya mkato/kughushi!

Kumbe ni walinda mlango wa hapa hapa Bongi!
 
TFF ya awamu hii ni majanga!! Yaani mtu anaweza kufikiri hao walinda mlango labda walitoroka nchini Somalia, na kuja kusajiliwa na hivyo vilabu kwa njia ya mkato/kughushi!

Kumbe ni walinda mlango wa hapa hapa Bongi!
Kufungiwa kumezidi (ingawa Manara anastahili). Nafikiri vilabu viungane kukataa huu ujinga. Hata kugomea ligi
 
Hivi Simba na Yanga zinaweza fungiwa kwa kosa kama hili? Nawaza
Simba walimchukua Kyombo lakini baadae singida wakaenda kupewa hela ili yaishe,,,

Hapo nyuma iliwahi kutokea kwa busuita alisain Simba halafu akajiunga yanga,, Utopolo wakaamuriwa wailipe Simba.

Pia Kuna usajili wa marehm jeba kutoka Azam kwenda Simba
Pia Ramadan singano toka Simba kwenda yanga..

Kuna Mubarak Yusufu toka Simba kwenda Kagera....

Kiufupi hapo Tff huwa wanaangalia upepo tu
 
Back
Top Bottom