Rev, Kishoka,
' Uchumi mnao mmeukalia' Mtu wa kwanza kusema maneno haya alikuwa Rashid Kawawa, Mwinyi amekuwa akiurudia mara nyingi ila nakuimbuka kuna moja hii kali sana ya Mwinyi akiwahutubia wananchi wa Mtwara - Alisema:- Humo humo katika Mikorosho kazaneni!.... eeeh bwana wee wamachnga walifanya matusi vibaya sana mikoroshoni..wakidai kuwa - Nzee kasemaaaa.
Pundit,
Mimi ni mmoja wa watu ninaokubaliana kabisa na msemo wa Nyani Ngabu na inabidi utazame tulikotoka, tulipo na tuendako ili upate kuelewa msemo huo una maana gani na uzito gani
Kumbuka wakati wa mkoloni Waarabu wawili wenye gobole la kushindiria baruti za risasi waliweza kuchukua Waafrika (Miafika) Elfu nzima wakapigwa minyororo na kuongoza toka Zaire, Tabora hadi Bagamoyo, tena basi minyapara ilikuwa Miafrika vile vile!..Na Spy wanaopeleka habari kwa walowezi walikuwa Miafrika mienzetu.
Ukitazama Wazungu toka Mjarumani na Muingereza walikuwa hawana majeshi makubwa kulinda koloni zao Afrika isipokuwa walitumia Miafrika kuendesha Ukoloni, tena kuna wengi kibao walikwenda kupigana vita Burma, North Afrika kulinda himaya za wazungu...Adui wa Mwafrika ni Mwafrika mwenzake, vita yote ya mwafrika ni mwafrika mwenzake -Tazama historia ya nchi zote za Afrika tulipigana sisi wenyewe kwa wenyewe kwa makabila yetu kuliko vita dhidi ya Mwarabu ama mzungu mkoloni. Tena tuliwalinda sisi wenyewe wakaweza kututawala kwa karne..
Haya tulipo leo tazama hizo nchi Zaire, Rwanda, Burundi, Ivory Coast, Nigeria, Zimbabwe na kadhalika...Kote tunapigana sisi wenyewe waafrika Utafikiri tumepagawa.. wakoloni walitubebesha Bunduki tukaua ndugu zetu wakati sisi wenyewe bado tumo ndani ya Utumwa. I mean mkuu just imagine wewe POW unapewa Bunduki na risasi lakini bado unakuwa royal kwa bwana wako unaenda kumwinda ndugu yako...South Afrika! Mtume wamefikia hadi kutufukuza waafrika wote kuwa tunamaliza kazi zao (utumwa) lakini sio mzungu ambaye anachukua all high post zenye kulipa mishahara mizuri.
Kuna mfano wa mzee Bundalla aliokota pande la Almasi akampelekea mzungu (Williamson) ambaye kawa mvumbuzi na tajiri (Mwadui Diamonds) hadi wajukuu wake wanafaidika na mali ile lakini familia ya Bundalla hadi leo inabangaiza...No action taken!
Ni katika kutazama tulikotoka, na wapi tumesimama leo hii - Viongoizi wachafu CCM ndio wameshika madaraka tena wabaya kuliko Mkoloni kwa sababu ni ndugu zetu sisi wenyewe, ni kati yetu sisi wanatuibia mali zetu lakini kipi wananchi wanakifanya tofauti na Mkoloni?.... HAKUNA...talk the talk sawa na zile poem zilizokuwa zikiandikwa wakati wa Kina Kunta Kinte...
Mimi nafikiri Ujumbe huu ni mzito sana na tusiuchukulie mzaha ama tusi isipokuwa ni La mgambo kwetu!...Hivi unafikiria kuna watu wangapi ktk Mtandao?...iweje hawa watu wachache sana waweze kutuburuza sisi sote pamoja na rais mliyemchagua...
Tutaendelea kuwa NDIVYO TULIVYO hadi lini?..