joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Kaka tunazungumza vitu tofauti sana, wewe unazungumzia katika level ya watu mmoja mmoja wakati serikali inazungumzia katika National level, hebu niambie vitunguu vinachangia kiasi gani katika pato la taifa?, mwisho utasema biashara ya mikungu ya ndizi na kuku wanaovushwa huko mipakani, hiyo biashara ya vitunguu wala serikali hizi mbili haijui ni kiasi gani inachangia katika pato la taifa, ni ndogo mno kuumiza vichwa vyetu.Vitunguu Bila Wakenya vyaoza, Mahindi bila wao bei unaiona sasa
Kuhusu mahindi, Kenya sio mnunuzi mkuu wa mahindi ya Tanzania, japo Kenya anategemea sana mahindi toka Tanzania, kumbuka mikoa inayozalisha mahindi kwa wingi Tanzania ipo kusini mwa Tanzania, mahindi mengi yanavuka mipaka ya nchi za kusini kama DRC, Malawi, Zambia, Msumbiji na zimbabwe, bei inashuka kama serikali inapiga marufuku kusafirisha chakula nje ya nchi, hasa nchi za kusini na DRC lakini sio Kenya