Shirika la Fedha Ulimwenguni(IMF) limedai kwamba bajeti ya Tanzania ya Trilioni 31 ni "changa la macho" na kwamba Tanzania haina vyanzo vya fedha kukusanya mapato yanayofikia trilioni 31
Kwa maana hiyo shirika hilo linasema watanzania tumepewa matumaini yaliyopita kuliko cha uwezo wetu!
Binafsi ninaona kuna ukweli asilimia kubwa sana,ukiangalia bajeti ya mwaka 2016/2017 ilitekelezwa kwa asilimia 38,ikashindwa kutekelezwa kwa asilimia 62
Bajeti ya 2016/2017 ilikuwa trilioni 29, lakini pesa iliyotoka ni trilioni 15,bajeti ya mwaka huu 2017/2018 ni trilioni 31,sasa kama ya mwaka 2016/2017 ilitushinda kufikia hata nusu,tulikuwa na vigezo vipi vya kuipandisha bajeti yetu mpaka ifikie trilioni 31?
View attachment 531778 View attachment 531779 View attachment 531780
Yaani tulishindwa hata kuikaribia nusu!
Sasa tumeongeza makadirio ya bajeti mpaka trilioni 31 wakati vyanzo vya mapato ni vilevile,na serikali inasema kumekuwa na wimbi la kufunga biashara,makampuni yanapunguza wafanyakazi
Mapato watayakusanya kutoka wapi!???
IMF ndio moja kati ya mashirika makubwa yanayoongoza na kutoa mwelekeo wa uchumi wa dunia,lakini wanakiri kwamba bajeti yetu ni "changa la macho"