Mleta mada mm naamini hujui unachoandika au imejawa na kujipendekeza na uchawa pro.
Any way ngoja nikueleze kwa uchache sana.
Royal tour imekuwa released mwezi Aprili 2022.
Hao watalii wa nje unao waona wamekuja au wanaokuja katika miezi hii miwili hadi mwishoni mwa mwaka huu walifanya maandalizi ya safari zao tangu 2021.
Unajua mtu anavyosafiri kwenye mapumziko nje ya nchi lazima ajiandae kwa ratiba yake ya kazi kuomba ruhusa makazini kwao,kuwa na pesa za kutosha,kuchagua wapi anataka kwenda halikadhalika afanye bookings za ndege hoteli na activities.
Sasa ww unavyodhani mwezi wa nne baada ya released ya Royal tour immediately mtu kachukua begi na kuja Tanzania?
Kumbuka watalii hupanga na kubook safari zao mapema zaidi ya mwaka mmoja na wale wa last minute sio chini ya miezi miwili/mitatu kabla ya kusafiri.
Njoo tukufundishe namna watalii wanavyosafiri na kuja Tz,usidhani wanakurupuka kama vile wanakwenda msibani.
Acha uchawa andika facts.