Tanzania second largest producer of RICE in Africa

Njowepo

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Posts
9,710
Reaction score
2,240
Tanzania currently produces more than 1mn tonnes of rice, which makes it the second largest rice producer in Africa after Madagascar, which produces about 2.5mn tonnes. However, local authorities see growth potential for the country mainly as a result...
Madagascar: total area: 587,041 sq km (land: 581,540 sq km & water: 5,501 sq km )
with the population of 22,599,098 (July 2013 est.)
Tanzania: total: 947,300 sq km (land: 885,800 sq km & water: 61,500 sq km )
Population 48,261,942 (July 2013 est.)
Ivi kwa nini hatunaga wivu wa maendeleo hawa jamaa tumewazidi idadi ya watu(implies huge labour force) na ata ukubwa wa ardhi tumeashinda yet wanatuongoza kwenye uzalishaji wa mpunga.
I know with government intervention kwenye kilimo cha zao hili kwa kuwawezesha wakulima wa kamsamba,shinyanga,kyela,mahenge,mbalali etc
 

Hapo kwenye blue,
Unashangaa nini ??
Wewe mgeni nchi hii ?? au uko nje ya nchi kwa muda mrefu saaana !!
 

Mimi nilifikiri ungeanza angalau kwa kusifu badala ya kulaumu tu kila siku, Kutokana na maelezo yako sisi ni wa Pili ktk Bara la Afrika, hauoni kama tumejitahidi sana, sisi tuko chini ya watu milioni 44 na niwa pili Afrika kwa kulima Mpunga, huuu Hongera zetu!

 
Hapo kwenye blue,
Unashangaa nini ??
Wewe mgeni nchi hii ?? au uko nje ya nchi kwa muda mrefu saaana !!

Niwe mgeni au mwenyeji niwe nje au ndani ya inchi Tanzania deserves to be the first producer given the land and the labour force we have.
 

We have a room to improve and become the number one producer and rank our self worldwide
Think big ndugu izi sio zama za kulizika
 
mh hiyo rice inalimwa wapi? Maana juzi tu hapa serikali imeagiza au kuruhusu wafanyabiashara kuagiza mchele toka nje. Naona km kuna walakini hapo
 
Niwe mgeni au mwenyeji niwe nje au ndani ya inchi Tanzania deserves to be the first producer given the land and the labour force we have.

Agreed, Tanzania ikijikita kwenye kilimo, inaweza kulisha Africa nzima.
Kwa raslimali ya ardhi tuliyonayo, hatutakiwi kuagiza chakula toka nje ya nchi.
Lakini, kama kawaida yetu, raslimali ipo imekaa bure tu.
Aaaaaaghh !!!!
 
We have a room to improve and become the number one producer and rank our self worldwide
Think big ndugu izi sio zama za kulizika

Sio swala la kuridhika au kutokuridhika, ni swala la kwanza kutambua jitihada za watu wengine na kuwapa hongera pale wanapojitahidi halafu mapendekezo ndiyo yanafwata baadae, kwangu mimi kama hiyo Habari ni ya kweli basi nasema HONGERA KWETU tena sana tu, kwani kuwa wa 2 (kama ni kweli) ktk Bara lenye watu bilioni 1 na sisi tuko chini ya milioni 44, tunastahili pongezi kwanza, halafu baadaye ndio kuanza kuangalia kwa nini tusiwe wa 1
 
Kuna kale ka nchi wapo watu 500,000 waliingia AFCAN, sisi 48,000,000 hakuna kitu.pamoja na kuwa wa 2 bado tuna import mchele toka thailand,na mafuta ya kula toka malaysia
 
kuwa wa pili in rice production ni jambo jema sana na la kujivunia ,,,ila mjue hapa tunaongelea mchele tu!!!,,,huo mchele unapika wali(ubwabwa),ila mkumbuke wali hauliwi mkavu,tujitahidi na mboga basi....wat abt mahindi na vyakula vingine ambavyo watumiaji wake wengi ni wale wa kipato cha chini?
pongezi za dhati kwa JICA...they are behind this success
 
Niwe mgeni au mwenyeji niwe nje au ndani ya inchi Tanzania deserves to be the first producer given the land and the labour force we have.

Ukubwa unaozungumzwa hapo sio ukubwa wa kulima mpunga/mchele, ni ukubwa wa nchi, japo Tanzania ni kubwa kuliko Madagascar, lakini matumizi ya Ardhi ya Tanzania yapo tofauti sana na Madagascar, zaidi ya mpunga, Madagascar haina umaarufu kwa kilimo cha kitu kingine Tanzania inalima mahindi sana, ina mashamba makubwa sana ya miwa, katani, Tanzania ina maeneo mengi yaliyotengwa, yasiyofanya shughuli za kilimo (mbuga za wanyama, misitu ya mbao na karatasi pamoja na misitu ya hifadhi, kama Biharamulo, Lushoto nk),

Nadhani point ya muhimu ni kuwa kilimo tunacholima Tanzania ni cha kizamani, lakini kama kilimo cha kisasa kikitumika kwa eneo hilohilo linalotumika sasa kulimia mpunga/mchele kuna uwezekano wa kuwazidi Madagascar kwa mbali sana
 

Naona taarifa hii kwamba Tanzania ni nchi ya pili Africa kuzalisha mpunga mwingi ni mpya imetoa jikoni leo, labda ni nchi ya pili kwa zile zilizoko kusini mwa Ikweta. Nashangaa ni lini Tanzania tumevuka nafasi yetu ya nne na kuwapita Misri na Nigeria!? Siku hizi ubishi sipendi maana lolote linawezekana ninachoomba ni source ya hizi taarifa! Hatuna jeuri ya kuwapita Misri na Nigeria kwa muda huu! Msilete siasa kwenye facts! Watanzania ndani ya nchi huwa tunajifagilia sana na kupandishana chat sana kwamba mambo ni mazuri sana lakini ukishaenda kwenye level ya kimataifa ndiyo utagundua jinsi tulivyo nyuma kwenye mambo mengi tu ikiwamo kilimo, asikudanganye mtu! Subirini Kenya wanajipanga na serikali ya Jubilei muone kama tutawauzia mpunga tena, tutaishia kuhesabu mito, maziwa na mabonde tuliyonayo tumesahau tatizo letu kubwa ni quality of human resource!!
 
Agreed, Tanzania ikijikita kwenye kilimo, inaweza kulisha Africa nzima.
Kwa raslimali ya ardhi tuliyonayo, hatutakiwi kuagiza chakula toka nje ya nchi.
Lakini, kama kawaida yetu, raslimali ipo imekaa bure tu.
Aaaaaaghh !!!!

Hatuna upekee wowote hapa Afrika, hizo sifa ulizozitaja nchi nzingi tu za Afrika inazo na zaidi, hivyo karibu kila nchi inaweza kusema hivyo hivyo hapa Afrika siyo sisi tu!

 

Nigeria ni top importer sio producer. Get your fact.
 

Mkuu asilimia 60 ya mpunga unaozalishwa Tanzania unatoka kwenye kilimo cha kutegemea mvua (rainfed lowland rice ecosystem). Kanda ya ziwa ndiyo kinara wa uzalishaji. JICA wamejikita zaidi kwenye kilimo cha mpunga maeneo yenye umwagiliaji ambako ukweli ndiyo huo kwamba mchango wake ni asilimia kidogo tu ukilinganisha na maeneo yanayotegemea mvua! Harakati zilizopo hivi sasa za kujenga skimu za umwagiliaji ni usanii tu, wanatengeneza mabanio ya maji tu (intake) na mifereji kiasi lakini mashamba mengi ya umwagiliaji hayaingiliki kwa mashine za kufanyia kazi! Hayajapangwa na hayana miundo mbinu kama farm roads. Kuingiza mashine ziwe za kulimia au kuvunia au kubebea mazao mashambani haiwezekani, kuvuna mazao unayatoa shambani kwa kubeba mazao kichwani umbali mrefu hadi utoke nje ya shamba, hakuna mashine inaweza kuingia kirahisi mashambani! Mashamba ambayo yangeleta maendeleo ni kama yangetengenezwa mfano wa yale ya umwagiliaji kule Dakawa, Ruvu, Mbarali, Ndungu, Lower Moshi na mengine machache ambako ni rahisi sana kuingiza mashine za kuharakisha na kurahisisha uzalishaji. Tz bado sana kwa hilo ni siasa kwa sanaa na kelele kibao kwamba mambo yanakwenda safi huku njaa haiishi!
 

Fascinating findings and pretty useful piece of information! Would u mind to provide the source?
 
Nigeria ni top importer sio producer. Get your fact.

Subiri nitaweka published document, fact hatupeani kwa maneno tu! Mnacheza na Nigeria eenh!! Being the top importer does not mean it produces less than Tanzania!!
 
Tafadhari pekua pekua linki hii FAOSTAT ! Hizi facts on fingertips siyo za kutafuta kwa darubini, nikitu bayana, Nigeria iko juu kiuzalishaji hata kama wanaimport sana.Pia fungua na hii Milled Rice Production by Country in 1000 MT - Country Rankings uone kuwa Tz si nchi ya pili labda iwe imepanda juu kwa mwendo wa vodafasta!

Kwa wale ambao hamtaweza kufungua link hizi kifupi ni kwamba uzalishaji kwa nchi vinara Africa uko hivi:

1. Misri tani Million 4.7 mchele
2. Nigeria tani Million 2.8 mchele
3. Madagascar tani Million 2.6 mchele
4.Mali tani Million 1.4 mchele
5.Guinea tani Million 1.1 mchele
6.Tanzania tani Million 0.9 (approximately 1 million ton)

Hapo mjue sasa mchele halisi ni upi na na pumba ni zipi chambueni wenyewe wadau!!
 

Attachments


Nimekubali mkuu lakini tukijaribu kwenda mbele zaidi kulinganisha na population ya nigeria ya 162+m...vs 44m ya tz...tunaona relative to population bado tz inazalisha zaidi ya Nigeria.

ratios za kawaida tu TZ 1/44m = 0.023
NG 2.8/162M = 0.017.

Kwa context hiyo Tz inazalisha zaidi ya Nigeria....Wasalaam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…