Tanzania SGR inajengwa Usiku na Mchana.

Tanzania SGR inajengwa Usiku na Mchana.

Mwanzi1

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2016
Posts
6,000
Reaction score
4,589
Wakati majirani zetu Kenya wanahangaika na changamoto za kisiasa, Tanzania inajikita kwenye uchumi wa Massa 24.

f06955e0d0b65c8e78a9b18a2848764d.jpg

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa (wa pili kulia) akiongozwa na Meneja Mradi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge kutoka RAHCO, Maizo Mgedzi (kushoto) pamoja na Meneja mradi huo kutoka kampuni inayotekeleza mradi huo ya YAPI Merkezi kutoka Uturuki, Abdullah Milk mara baada ya kufika eneo la Soga – Kibaha jumamosi usiku kuona endapo wakandarasi wa mradi huo wanafanya kazi usiku na mchana kama walivyosema katika mkataba wao na serikali.

6960cb2f1a3ed48015c983105cb764e5.jpg

Meneja Mradi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge kutoka RAHCO, Maizo Mgedzi akitoa ufafanuzi juu ya mradi.

d562c0e401fc0c0999b3336e98b2bbc1.jpg

bd57fb15d60d0823f685601203317024.jpg

Ujumbe huo aliutoa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa wakati alipofanya ziara ya kushtukiza usiku wa jumamosi katika kambi mbalimbali za mradi huo zilizopo Pugu mpaka eneo la Soga Kibaha ili kuona endapo wakandarasi wa mradi huo wanafanya kazi usiku na mchana kama walivyosema katika mkataba wao na serikali.

Kadogosa alisema mradi huo unatakiwa kwenda kwa kasi na kukamilika haraka hata kabla ya muda husika hivyo kila mtu atakayefanya kazi katika mradi huo ahakikishe anafanya kazi na sio ubabaishaji utakaopelekea mradi huo kuchelewa.

Aidha Kadogosa alisema wamefikia makubaliano ya kufanya kazi usiku na mchana ili kuharakisha mradii huo na wakandarasi wanafanya haraka na kwa ukubwa wa mradi huu ni lazima tufanye kazi usiku na mchana.

“Kama mnakumbuka wakati Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Makame Mbarawa alipokuja hapa alisema ni lazima twende kasi na wakandarasi wetu wameamua kwenda na kasi na sasa mnaona tuta linaendelea vizuri ni lazima mradi huu ufanywe usiku na mchana kutokana na ukubwa wake,”alisema.

Msafara huo ulipofika eneo la mradi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge Soga – Pwani.

b0c881cd3fb01e594937326e27ed460d.jpg
bc06dd84beb0534fdec18fd07c6fd9fc.jpg

Shughuli ya ujenzi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge Soga – Pwani ikiendelea.

3205a847b891ef4c784b44026a9e5fc5.jpg
e7d60e18fbbd0832b279c20b68cd6377.jpg

5546eb355bca5f368c24c74b99a30909.jpg

fd5a46e170faeb0a3f0cfdc242d1f135.jpg

Meneja Mradi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge kutoka RAHCO, Maizo Mgedzi akitoa ufafanuzi juu ya mradi.

Kwa upande wake Meneja Mradi huo kutoka RAHCO, Maizo Mgedzi alisema kazi inayoendelea kwa sasa ni kuendelea kusawazisha tuta ikiwa ni pamoja na kukata na kujaza, kujenga mifereji na madaraja ya reli pamoja na kuweka miundombinu ya umeme pamoja na vifaa vya kuongozea reli.

760bf0645c122c4f5eb2abfd12f750e3.jpg

Kwa upande wake Meneja mradi kutoka kampuni inayotekeleza mradi huo ya YAPI Merkezi kutoka Uturuki, Abdullah Milk alisema kampuni hiyo imejipanga kuhakikisha mradi huo unatekelezwa usiku na mchana ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati.
 
PR at it's best...kweli wajinga ndio waliwao.
 
Sasa hapo mbona hatuoni zege ikikorogwa, ni mapicha mapicha tu ya jamaa wamevaa mavazi ya kazi usiku ambao hatujui saa ngapi, inawezekana mida ya saa moja usiku.
Tatizo Waswahili maneno mengiii kabla ya kuanza kazi yenyewe.

Sisi wakati tunajenga SGR tuliwajazia huku picha za wanaume wakiwa kazini, sio huu urembo mnatuonyesha hapa. Halafu mkumbuke mambo ya SGR kwetu sio habari tena kwetu, kwenu sawa maana ndio bado mnaanza kushangaa shangaa, naskia hata fly over bado mnashangaa wakati sisi tulishachoka nazo.

SGR+2.jpg
 
Mbona unapitiliza kuweka maelezo bila kusoma yaliyomo, zege itawekwa kwa wakati wake, kinachofanyika sasa ni kusawazisha maeneo yote. Cha msingi ni kazi itafanyika USIKU NA MCHANA kama mkataba ulivyosema na muda utafupishwa. Yani ni usiku na mchana kwa hela nusu ya Kenya SGR, sijuwi kama umeliwaza hilo au lilikupita. [emoji23]
 
Hadi mlete picha za zege ikikorogwa, hayo mengine yatabaki kuwa stori, nakumbuka mlituzungusha sana na mapicha ya kihivi ya kuonyesha sura kipindi kile cha bandari ya Bagamoyo.

Halafu SGR yenu gharama yake sio nusu ya Kenya, haya tuliyajadili huku kwa kina na mahesabu yakadadavuliwa balaa, lakini kwa jinsi huwa mlivyo, mkikaririshwa huwa hamuachi.
 
Sasa hapo mbona hatuoni zege ikikorogwa, ni mapicha mapicha tu ya jamaa wamevaa mavazi ya kazi usiku ambao hatujui saa ngapi, inawezekana mida ya saa moja usiku.
Tatizo Waswahili maneno mengiii kabla ya kuanza kazi yenyewe.

Sisi wakati tunajenga SGR tuliwajazia huku picha za wanaume wakiwa kazini, sio huu urembo mnatuonyesha hapa. Halafu mkumbuke mambo ya SGR kwetu sio habari tena kwetu, kwenu sawa maana ndio bado mnaanza kushangaa shangaa, naskia hata fly over bado mnashangaa wakati sisi tulishachoka nazo.

SGR+2.jpg
Hiyo yenu tulishaijengaga 1960's huko,
In fact this have to be news to you as well,
Sababu SGR Tz is the Modern in the entire region.
 
Back
Top Bottom