Hadi mlete picha za zege ikikorogwa, hayo mengine yatabaki kuwa stori, nakumbuka mlituzungusha sana na mapicha ya kihivi ya kuonyesha sura kipindi kile cha bandari ya Bagamoyo.
Halafu SGR yenu gharama yake sio nusu ya Kenya, haya tuliyajadili huku kwa kina na mahesabu yakadadavuliwa balaa, lakini kwa jinsi huwa mlivyo, mkikaririshwa huwa hamuachi.
Tunawapongeza sana wenzetu wa Kenya kwa kutangulia, mmetuonesha njia kwenye SGR na sisi ndugu zenu tunafuata, tupo slow kuliko ninyi lakini tutafika tu. However, we have to keep in mind that the most important thing is not only the SGR but the type of SGR in terms of cargo carrying capacity, speed, cost as well as type of energy used to run locomotives and the negative impact of the energy used to the environment/society. Sina uhakika kwakuwa sijafanya utafiti ila nimesikia kuwa SGR yenu Wakenya kuwa ni ya kizamani kwa maana kuwa inatumia diesel kitu ambacho kimepitwa na wakati, maximum speed ni 90km/hr, uwezo wake wa kubeba mzigo ni mdogo na gharama yake ni zadi ya SGR inayoendeshwa na umeme, hivyo vyote ni opposite to theone that TZ is constructing. Vipi ndugu yangu mpendwa umeshawahi kufanya utafiti juu ya hili na kupata majibu kuwa ni kweli au si kweli, tueleze basi tuelewe. Asente jirani.