Tanzania "Shamba la bibi" hadi lini? Hii Ruby ni yetu. Iweje iko sokoni Dubai na serikali yetu haijui? Nasaidia, mchimbaji huyu, anzieni hapa!

Hata kwenye huu mjadala wa ubinashishaji wa Bandari yetu kwa kampuni ya DPW ya Mwarabu wa Dubai, tunaendeleza uzalendo ili tusiendelee kufanywa shamba la bibi Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!

Hakuna. Mtanzania yeyote mwenye akili zake timamu anapinga maendeleo ya nchi yake, kinachotakiwa ni tumefanywa sana shamba la bibi, tusiendelee kufanywa shamba la bibi, let's negotiate a good deal
P
 
Hivi P ibara ya 6 na 13 unaionaje wewe kama wewe?? Ni deal nzuri au??
 
Na huo ndio ukweli mchungu. !!
 
Tuwe kama China. Adhabu kifo. Uone kama watu wataiba mali ya umma..
Na huo ndio ukweli mchungu. ! Lakini kwanza Kabisa ni Katiba mpya bora ambayo itaifumua mifumo yote inayotakiwa itende haki kwa watu wote ili kusiwepo na uonevu au upendeleo wowote kwa yeyote yule !

Kisha mifumo isukwe ipasavyo !! Hata hao wachina mpaka wamefikia hapo wameshapitia changa moto nyingi kama zetu na kushinda zetu !!

Panapo na nia na njia ipo !! It can be done play your part !
In Mwalimu’s voice R.I.P 🙏🙏🙏
 


Tanzania tuna waandika habari na si waandishi wa habari.kuna jiwe la rubi limenadiwa uarabuni kwa dola 120m sawa na b288 lkn hakuna chombo cha habari hata kimoja kilichoandika bali ni Askofu Bandukile ndoa kaibua na kuposti facebook
Hututendei haki, wandika habari wapo, waandishi wa habari wapo, na wahandisi wa habari pia wapo ambao ni watunga habari.

Kuhusu hiyo Ruby, karibu mitaa hii Tanzania "Shamba la bibi" hadi lini? Hii Ruby ni yetu. Iweje iko sokoni Dubai na serikali yetu haijui? Nasaidia, mchimbaji huyu, anzieni hapa!

Na hii Rubi kutoka Tanzania yavunja rekodi Dubai hivyo usiseme hatujaandika, sometimes mnatuonea sana.

P​

 
Mkuu pascal Mayala kama twiga aliweza kupanda ndege na kutoroshwa inakuwaje unashangaa jiwe la kilo mbili kutoroshwa?
Twiga alifanya boarding pale airport moja nchi ya kufikirika akapanda ndege bila kuonekana na mamlaka zinazo husika.
 
Ndugu Mayalla, ukishatoa kibali cha uchimbaji kwa mwekezaji (mgeni au mwenyeji) at what point mali anayopata inaweza kumilikiwa kinguvu na serikali, refer ishu ya yule Mamba
 
Waoman na Dubai wamefanikiwa sana kutuletea wageni kututawala kisiasa na kiuchumi.

Wamefanikiwa vile vile kuchukua mpaka ardhi ya Tanganyika.

Watabeba kila kitu.
Kwa sasa wachina wanavuna miti kama vichaa.

Wageni Wanaupigawingi!!

Mfukuzeni wakala wa Waarabu Tanganyika ili nchi iwe salama.
Vinginevyo Tanganyika tutabaki na madeni na mashimo ya migodi.
Pascal Mayalla 2025 Msimpigie kampeni Mgombea atakayekwepa midahallo. Tunataka Wagombea wote wawekwe kwenye mdahalo ili watuonyeshe uzalendo wao na maono yao kwa taifa hili kwa vizazi vijavyo. Hata wagombea wenza waitwe kwenye midahalo.
Hii nchi tusipokua makini tutakua na vyombo vya dola vinavyolinda ufisadi wa watawala kwa kutumia mamlaka makubwa ya mtu na marafiki zake
 
Mambo kama haya yasingetokea laiti kama JPM angekua Hai.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajiliwaza tu. Kwani wakati wake kulikuwa hakutokei upigani na hapakuwa kabisa na ripoti za kila mwaka za CAG kuonyesha fedha zinazopigwa? Mungu amwtujalia binadamu akili sana na ndiyo maana tunafanya maendeleo makubwa na kwa akili hiyo hiyo tuna uwezo wa kufanya uharibufu mkubwa (regression). Hivyo, katika Kila awamu kuna potential ya kufanya maendeleo makubwa na kuna potential pia ya kufanya blunder kubwa (coexistence of good and evil). Cha kufanya ni kuendelea kuwa responsible and law-abiding citizens and at the same time be able to prevent as much as we can some evil such as mismanagement or depletion of our resources.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…