Tanzania "Shamba la bibi" hadi lini? Hii Ruby ni yetu. Iweje iko sokoni Dubai na serikali yetu haijui? Nasaidia, mchimbaji huyu, anzieni hapa!

Good Analysis 🙌
 
Kwanza huyu mchimbaji atabaki na nini baada ya kuliuza.
Isije kuwa akapewa vi milioni wakati jiwe limeuzwa mabilioni
 
Hiyo ndio BABA JEN tena kama yule Twiga aliyekwea pipa bila passport hii ndio TZ yetu tuliyo izoea,mwingi unapigwa, asali zinalambwa na milango inafunguka mpaka Dubai.Sijui ndio ile misafara ya kipindi kile ya Dubai EXPO ya mzee wa Schedule Maintenance.

Na mama kishasema yy sio Simba wa Yuda.
 
yasingetokea au Taarifa zake zisingetokea?

JPM alikuwa Mchapakazi sana lakin moja ya udhaifu wake ni kuminya habari ambazo pengine zingekuwa zinamsaidia kujua Wasaidizi wake wanayoyafanya nyuma ya kivuli chake


Jakaya alikuwa mjanja mjanja lakin bado aliruhusu habari za ufisadi kutoka kwa kuwa zilimsaidia kujua Wasaidizi wake wakimzunguka

Wasaidizi na Rafiki zake walipomruka kwny Richmond nae 'akawaruka ' mazima

Mambo kama haya yasingetokea laiti kama JPM angekua Hai.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeisoma hiyo article ya Kiingereza?
 
Mfano Mimi mfanyabiara yenu wapi?

Mfano niliinunua 1980 kihalali kwa dola 200 nikaondoka na hayo Madini nikaihifadhi kusubiri bei ipande leo imepanda nikauza

Tanzania utasemaje yenu? Chako dola mia 200 nilikulipa Miaka hiyo unanifuata kwa chako kipi?
 
Katika bandiko lako sijaona ni mwaka gani lilichibwa. Shida kwangu ni kwamba chini ya 2016. (Nikiamanisha kabla ya Magufuli), Market ya madini ilikuwa black market. Hivyo madini mengi yalichimbwa na kuuzwa bila mifumo ya serikalini kujihusisha . Maduka mengi ya wanunuzi wa gemstone ( madini ya Vito) kwa dar yalikuwa Kinondoni na hakuna Uthibiti wa serikali dodoma yalikuwa mpwapwa kwa wingi na kusini yalikuwa Tunduru na Songea sehemu zote za ununuzi serikali ilikuwa imesinzia. Ukizungumuzia Winza mining area uchimbaji wa Ruby ilifanyika Kati ya 2007 Hadi 2013 diyo pakawaka zaidi baada ya hapo pakawa kawaida. Kipindi hiki chote serikali ilikuwa imesinzia.
Kunamadini mengi serikali haikunufaika mfano mwingine ni Spinel from Empanko Mahenge Morogoro hili ni jiwe la 52kg lilinunuliwa tsh16billion na mlanguzi wa kiisilaeri Malapa hapa dar na kwenda kuuzwa tsh21billion serikali haikupata chochote pia Soma hapo kwa maelezo zaidi Gem Hunting in Mahenge & Tunduru Tanzania • Downtown.
Mambo ni mengi wakati mchache.
Magufuli alifaulu kututoa kwenye black market na kutuleta kwenye open market but it seems we are going back again.
 
Jeffrey Bergman anataka kuwekea kitumbua cha watu mchanga. Kwa hiyo Burj Alhamal linaweza kuwa around $10,000!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…