Tanzania "Shamba la bibi" hadi lini? Hii Ruby ni yetu. Iweje iko sokoni Dubai na serikali yetu haijui? Nasaidia, mchimbaji huyu, anzieni hapa!

Tanzania "Shamba la bibi" hadi lini? Hii Ruby ni yetu. Iweje iko sokoni Dubai na serikali yetu haijui? Nasaidia, mchimbaji huyu, anzieni hapa!

Ona jizi hili!

Hata shimo la choo huwezi kuchimba, utaweza wapi kuzama mgodini mtoto mchele wewe?

Ati tunafia kwenye mashimo! We utakuwa bwa-bwa sio bure!

Mashimo gani unayozungumzia?
Linufaika la mfumo uliopo madarakani awamu hii hilo, wakati mwingine unayapuuzia tu maana yanatamba kuwa ni awamu yao kula keki ya Taifa [emoji851]
 
Wanabodi

Naendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", na Leo ni kuhusu uzalendo wa kujitolea kuisaidia serikali yako na nchi yako, pale unapoona imeshindwa na inahitaji msaada, je tutaendelea kufanywa Shamba la Bibi Hadi Lini?.

Hili ni bandiko la kuisaidia serikali yetu kuhusu hii Ruby, Swali ni Tanzania tutaendelea kufanywa ni "Shamba la Bibi" hadi lini?!. Hii Burj Alhamal Ruby ni Yetu!, Iweje Iko Sokoni Dubai, lakini serikali yetu haijui chochote?!.

Uzalendo ni kuipenda nchi yako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote na kwa nafsi yako yote na kuilinda na kuitetea kwa moyo wako wote, kwa nguvu zako zote, na kwa uwezo wako wote, na ikibidi kuipigania, uwe tayari kuutoa uhai wako kuifia nchi yako!.

Uzalendo wa kweli hukaa ndani ya mtu, hauonekani kwa macho, bali hukaa moyoni, hivyo kuna watu ukiwaangalia kwa juu juu at face value kwa jinsi wanavyo onekana, wanaonekana kama ni wazalendo, lakini in reality sio wazalendo lolote wala uzalendo chochote, bali ni wapigaji, na baadhi yao ndio mafisadi wakubwa!. Wamejivisha ngozi ya kondoo ya uzalendo,Ila kwa ndani ni mbwa mwitu, fisi, Chui. Na kuna watu ni hohe hahe, masikini wa kutupwa, wanaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, lakini ndio wazalendo wa kweli wa taifa hili, Mimi ni mmoja wa wazalendo hawa.
Ukiona kuna kitu serikali yako imeshindwa na wewe unaweza kusaidia, saidia tuu usingoje uombwe.
Kwenye ulinzi wa Rasilimali zetu, kwa muda mrefu Tanzania tumekuwa na kilio cha kufanywa shamba la bibi kwa manyang'au kutuibia Rasilimali zetu as if hazina mwenyewe!.

Hivi ninavyoandika hapa, kuna jiwe la kito cha thamani aina ruby kutoka mgodi wa ruby wa Winza kule Dodoma, lenye uzito wa kilo 2.8, ambalo limechimbwa na Mchimbaji mdogo, serikali haijui, Mchimbaji huyo haijui thamani yake hivyo ameuza bei ya kutupa, serikali haijui. Mnunuzi kaliondoa nchini kinyemela serikali haijui. limeuzwa serikali haijui, mnunuzi kaliuza kwa tajiri wa Kiarabu, serikali haijui. Tajiri wa Kiarabu kalibatiza jina la Burj Alhamal Ruby, serikali haijui.

Sasa Burj Alhamal Ruby liko sokoni Dubai, likisubiria mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan uishe, lipigwe mnada, serikali haijui!.
Mbunge Mhe. Danstan Kitandula, anauliza Bungeni kumuuliza Waziri wa Madini kuhusu jiwe hili, Waziri wa Madini anashanga na yeye kusema serikali haijui Ila na wao wamesikia mitandaoni!.
Serikali sio mtu ni Taasisi, ina jicho kali linaona kila mahali, ina mkono mrefu unafika kila kona, hivyo katika hali ya kawaida, haiwekani haya yote yatokee Tanzania!, tutaendelea kufanywa Shamba la Bibi Hadi Lini?. Kwa vile sasa tunaishi kwenye ulimwengu wa "the world of information world" kila kitu ni kwenye ncha za vidole vyako, kuisaidia serikali yetu ipate PA kuanzia, hizi ni data zote za jiwe hili akiwemo mmiliki.
View attachment 2196654
Huyu dogo ndie Mchimbaji WA jiwe, na huyu jamaa Steve Ulatowski with a miner in Tanzania, ndie mtaalamu wa Madini aliyepima properties za jiwe hili, sasa analisagia kunguni ili mnada usifanyike kwasababu hilo jiwe limepigwa!.

Haya kazi kwenu serikali yetu. Anzieni na Mchimbaji, ila hala hala msi mu harass.
Burj-Alhamal-1024x891.png

Buyer Beware: Closer Examination of the Burj Alhamal Ruby Casts Doubt on its $120 Million Valuation​

by Jeffery Bergman, AGA ASG, BDC-BGC SSEF
April 21, 2022
An astonishing record-breaking rough ruby of 8,400 carats, weighing 2.8 kilograms, from Winza, Tanzania has gone on display at the Waldorf Astoria Dubai International Financial Centre. According to Patrick Pilati, a director of the company that owns the ruby, SJ Gold & Diamonds of Dubai, said it is one of the largest rubies in the world and is valued at approximately $120 million. As the company’s crown jewel, they have named it ‘Burj Alhamal’.

Is the Burj Alhamal really worth $120 million? Photo attribution: The National.
However, a closer examination of the stone casts doubt on its estimated valuation. A closer look at the details reveals the stone may not be what it seems. For example, a 5.00 carat stone weighs about 1.00 gram. Therefore, a 8,400 carat stone would weigh approximately 1.68kg, not 2.8 kilograms. Second, several rough ruby-in-zoisite specimens 5 to 10 times larger have been documented. Third, rubies from Winza are not found in zoisite. The stone is likely from Longido, Tanzania. Finally – and most importantly – current valuations for ruby-in-zoisite specimens do not support the estimated $120 million valuation for the Burj Alhamal.
So, what could the Burj Alhamal really be worth? Steve Ulatowski of New Era Gems is an expert in ruby-in-zoisite specimens. He has sold a substantial amount of this material at the going rate of around US$350 per kilogram, including the approximately 3kg specimen he is holding in the photo below. “Maybe US$1200 if we were lucky…wholesale, most likely [this would sell for] $750.”
Steve Ulatowski with a miner in Tanzania. ©Travis Lejman

New Era Gem’s table at Tucson 2022 selling ruby-in-zoisite specimens from Longido, Tanzania for $350 per kilogram.
Another example that undermines the extraordinary valuation of the Burj Alhamal is the 2 kg ruby-in-zoisite specimen named the “Gem of Tanzania.” It was initially valued at £11m (US$14.35m) and owned by UK Wrekin Construction. The company used the valuation of the stone to help prop up its balance sheet. Forced into bankruptcy, the court-appointed administrators Ernst & Young declared the 2kg stone’s £11m valuation and its accompanying documents as forgery. With 60 offers, it was eventually auctioned for a mere £8,000 (US$10,400), leaving creditors with massive losses exceeding £45m (US$58.7m).
But there’s still more evidence that points to an inflated valuation for the Burj Alhamal. A 228,000 carat (45.6kg) ruby-in-zoisite specimen offered by Bonhams in Los Angeles on 20 May 2014 carried an estimated value of US$100,000-$150,000. This enormous ruby specimen is 16 times larger than the “Burj Alhamal.” It failed to sell at the Bonhams auction. In other words, bidding did not reach the minimum estimated value of US$100,000 (or US$2,200 per kilogram).
Instead, the Bonhams stone, which the listing states was carved from a “single specimen of Tanzanian ruby rough” by a famous Idar-Oberstein carver, had a finished weight of 0.85kg and sold at auction for $13,200 or $15,500/kg. This is another great price/value comparison to the Burj Alhamal which, from its photos, is likely of similar or lesser quality. The National photo of Burj Alhamal shows that the stone may only be about 25% ruby and 75% zoisite. This means the actual ruby content is about 0.7kg – considerably less than the 0.85kg of the Bonhams carved toad.
Several other Bonhams auction records demonstrate that you can purchase ruby-in-zoisite specimens for a few hundred dollars.

New Era Gems website offers a 2.92KGS ruby-in-zoisite specimen for US$700.
The 2.8kg (or 1.68kg?) “Burj Alhamal” is only one of the gems in the SJ Gold & Diamonds Callisto collection, which includes 12 rough rubies that weigh a total of “an astonishing 236,000 carats” according to Tariq Saeed, writing for Dubai’s Periodical Today news website.
SJ Gold & Diamonds should pay closer attention to auction records when publishing any eye-popping valuation of the stones in its collection. Otherwise, experience from the likes of the Gem of Tanzania will dictate the obvious next question: “Why?”
Kwa kuwasaidia wenzangu na mimi ambao hizi lugha ni lugha za watu.

Kwa mujibu wa mtaalamu wa miamba ya madini, anasema japo hili jiwe la hii Ruby limeingizwa soko la kimataifa Kwa makaratasi ya kuonyesha limechimbwa mgodi wa Winza Dodoma, hizo karatasi ni forgery, hili jiwe limechimbwa Longido Arusha, na Mchimbaji mdogo, ambaye hajui thamani ya jiwe hilo, hivyo alishikishwa kidogo dogo cha pesa mbuzi , kwake akaziona nyingi. Jiwe likaondoka Longido.

Ili jiwe liweze kuingia masoko ya kimataifa, ni lazima lisajiliwe na kupatiwa certificate of origin, hivyo ukatafutwa mgodi wa ruby ambao uko tayari ku issue that certificate, and that where mgodi Winza huko Dodoma ulipoingia ukatoa face certification ili mzigo uingie Sokoni. Jamaa wakalipwa chao, wakaingia front kuwa jiwe ni Lao, wakaliandikia certification, na sijui kama kodi za serikali zilipwe ndio maana serikali haijui!.

Hawa mgodi wa Winza, walifanya kosa moja tuu, walipima uzito bila kupima properties na kulisajiji kuwa wamelichimba wao. Hilo jiwe lina properties za kitu kinachoitwa zoisite, ambacho kinapatikana Longido tuu!, iweje ruby ya zoisite ipatikane Dodoma?.

Ni kama jiwe la Tanzanite kinapatikana Mererani pekee, lakini muuzaji mkubwa number 1 wa Tanzanite ni India akifuatiwa na Africa Kusini, Tanzanite inapatikana Mererani pekee nchini Tanzania, hiyo Tanzanite ya India inayoongoza Duniani na Africa Kusini, inatoka wapi?.

Tanzania tunaendelea kufanywa Shamba la Bibi Hadi Lini?.
Wasalaam

Paskali​


Bro P SNR
Umeandika Kwa uchungu na emotions, hizo ifs & whys utajipa stress bure!
Wewe lea Tu, forgery nchi hii ni kawaida!
BoT wafanyakazi wanashika mikasi wanakatakata note za msimbazi kisha wanajilipa!
Immigration wanafoji visa na permits so ni kawaida kabisa!

Pop a chill pill!
 
Katika bandiko lako sijaona ni mwaka gani lilichibwa. Shida kwangu ni kwamba chini ya 2016. (Nikiamanisha kabla ya Magufuli), Market ya madini ilikuwa black market. Hivyo madini mengi yalichimbwa na kuuzwa bila mifumo ya serikalini kujihusisha . Maduka mengi ya wanunuzi wa gemstone ( madini ya Vito) kwa dar yalikuwa Kinondoni na hakuna Uthibiti wa serikali dodoma yalikuwa mpwapwa kwa wingi na kusini yalikuwa Tunduru na Songea sehemu zote za ununuzi serikali ilikuwa imesinzia. Ukizungumuzia Winza mining area uchimbaji wa Ruby ilifanyika Kati ya 2007 Hadi 2013 diyo pakawaka zaidi baada ya hapo pakawa kawaida. Kipindi hiki chote serikali ilikuwa imesinzia.
Kunamadini mengi serikali haikunufaika mfano mwingine ni Spinel from Empanko Mahenge Morogoro hili ni jiwe la 52kg lilinunuliwa tsh16billion na mlanguzi wa kiisilaeri Malapa hapa dar na kwenda kuuzwa tsh21billion serikali haikupata chochote pia Soma hapo kwa maelezo zaidi Gem Hunting in Mahenge & Tunduru Tanzania • Downtown.
Mambo ni mengi wakati mchache.
Magufuli alifaulu kututoa kwenye black market na kutuleta kwenye open market but it seems we are going back again.View attachment 2196686
Winza ilikuwa 2006 nakumbuka
2007 mwanzoni hata mm nkikuwa winza

Na ruby ya winza nakumbuka kuna mzee mmoja pale alikuwa anajishugulisha na uchimbaj alikuwa anaitwa mzee mturuchie (marehem sahv)baba Ben yeye ndiyo aliigumia
Ndani kwake walimkuta nayo kama debe 2 aliambulia kupewa fuso na kirolaa
Ndipo mlio ukaitika huko watu tukajazana huko
Ila kwa baday winza mawe yalikata kabisa,sasa najiuliza hii ruby imetokatoka vp huko au iliwekwa
Maana mlio mbona watu hawakuusikia
Kingine nikiangaliaaaaa hiyo ruby mbona inafanana kama ruby ya longido,miamba yake
Maana nakumbuka ruby ya winza ilikuwa ya sensa
Inafanana kdg kama ya mahenge,marombo au mtopwesh

Ova
 
Hata tusijifanye tunashtuka.

Tuliibiwa, tunaibiwa na tutaendelea kuibiwa sana tu nchi hii mpaka siku tutakapoamua kuitoa madarakani.
 
Serikali inakuwa taasisi pale tu kila mmoja kwenye taasisi hiyo ya serikali anapotimiza wajibu kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi na kwa maslahi ya nchi.......Kinyume chake na hapo hiyo serikali haina tofauti na kikundi cha wahuni.........

Hili tukio la Rubi ni muendelezo matukio yanayodhihirisha udhaifu kama sio uzembe wa taasisi tunayoiita serikali.........

Na kwa namna ilivyo credibility za watawala wetu Kuna asilimia kubwa kuwa hii ni inside job ndani ya serikali kupitia kwa tuliowapa mamlaka ya kutuangalizia rasilimali zetu......

Huu ni mfumo mbaya kwenye serikali au nchi ambayo inajipambanua kuwa inapigana kujitegemea.......


SHAME.....SHAME......SHAME.....SHAME.....
Tunashangaa jiwe moja la ruby ilhali watu walishasaini mkataba wa mgodi mzima wa dhahabu Hotelini huko ughaibuni ?? Au tumesahau ?? Hiyo ndio inayoitwa KAZI NA BATA !! Mmesahau tulikuwa tunagawiwa asilimia tatu kwenye migodi wenyewe wazungu wanachukua asilimia 97% ?? Ndio maana mkiambiwa hii nchi ni tajiri msibishe !! Mwalimu kipindi chake alikataa madini yasichimbwe kwa kuogopa kutapeliwa na mikataba yao ya kinyonyaji akasema yaacheni hayo madini yakae huko chini ya ardhi mpaka wenyewe watakapojua kuyachimba na thamani yake ndio watayachimba bila kunyonywa !! Matokeo yake ndio haya sasa waliokuwa wanasubiriwa waelimike kwanza Ndio wamekuwa wakiingia mikataba ya ajabu ajabu ya madini !! Na kuhusu hilo jiwe ruby haiwezekani Hao jamaa wadai kwamba limechimbwa Tanzania kama hawana documents za ku- surport madai yao !! Je ni akina nani waliotoa hizo documents ?? Iko kazi bandugu !!
 
Hiloo jiwe sijui imekuaje likawa na thamani kubwa hivyoo.


Mama atulie nyumbani.

na kauli za kula kwa urefu wa kamba achane nazo.
Kuna uhusiano gani kati ya jiwe na mama kukaa nyumbani....


Kama wizara zinazohusika na serikali kwa ujumla zimeshtuka baada ya kupata taarifa hizi kwenye mitandao ya kijamii.
Jua jiwe limetoroshwa wakati/Huenda likitoroshwa mama alikuepo.
 
Wee msaka tonge unaya jua machungu aliyo yapata aliyeichimba? Leo hii unadai hilo jiwe ni lako / lenu na angekuuzia wewe ungempa shilingi ngapi kama usinge mdhulumu??? Laiti ungeyajua mateso wanayo pata ‘wachoji’ pindi wanapo tafuta sijui kama unfekuja na ki hzi kama hiki…,
 
Paskali anajiuliza "hadi lini".wakat jibu analo.ni hadi tuondoe tamaa binafsi na kueka maslahi mapana mbele.
Lini tutaweza ndio hatujui.
Lingepita njia halali, njia hiyo ingepindishwa tu ili watu wajinufaishe binafsi. (Huenda ndio ilivokuwa.nan ajuae)?
 
Kwani kati ya hela zinazoripotiwa na CAG kuwa zinapotea/tumiwa vibaya /fisadiwa,na mrabaha ambao tungeupata. Lipi tungekipa kipaumbele.
80/20 rule.
 
Uzalendo wa kweli utaonekana pale ambapo serikali itaonekana inawasaidia wananchi badala ya kuwazuia, nyang'anya, toza Kodi isiyoeleweka n.k.
Lazima ifike wakati ambao wachimbaji watasimamia na kuamua kuhusu uuzajji wa madini yao, wakulima mazao yao, wavuvi samaki wao na hata wafugaji mifugo yao.
Watumishi wa serikali ambao hawajui gharama na mateso ya uchimbaji na taasisi zao hawaaminiki kwa wachimbaji.
Umasikini wa Afrika una misingi katika fikra za viongozi na taasisi za serikali dhidi ya raia hasa wale asilia.
 
Back
Top Bottom