Tanzania "Shamba la bibi" hadi lini? Hii Ruby ni yetu. Iweje iko sokoni Dubai na serikali yetu haijui? Nasaidia, mchimbaji huyu, anzieni hapa!

Nimemwona mzalendo wa kweli mmoja aliyeutoa uhai wake kuitetea nchi yake, ila kwa sababu kunguru ni wengi, wanajitaidi kumzushia mabaya kila siku, akalipwa majungu na kila aina ya kelele

Acha ikae hivo hivo hata kama watahamisha ardhi yote kupeleka kwao tuishi angani kwa nini shida???

Wakupiga apige tu
 
Sasa ndugu yangu,uchimbaji wa madini ni biashara huria kama biashara zingine..

Serikali imeweka masoko sasa kama wachimbaji hawapeleki wanatorosha lazima kuna shida..

By the way pesa zikiingia Serikalini wanasiasa wanachezea so hata huo uzalendo kama wa awamu ile ni shida..

Well done lakini.
 
... serikali ilikuwa na mchango gani kumwezesha huyo dogo kufikia malengo aliyofikia? Mjikalie kwenye maviyoyozi; mtutimulie mavumbi na ma-V8 yenu; adha tunazopata kama wachimbaji si kitu kwenu; tunafia kwenye mashimo kila siku halafu tukibahatisha ndio mnataka uzalendo? Be serious Pascal Mayalla.
 
Uhuni tu hapo hamna jiwe LA thamani hiyo,dhahabu tu 1Kg ni $ 50,000 sasa ruby ndio itauzwa bill hizo 240 kwa 2.8Kg??
Kwa akili zako tu za kuvukia barabara unadhani dhahabu ina thamani ghali sana kifedha kuliko ruby [emoji848]

Hivi mbona sisi wa-TZ tuna ujinga ujinga mwingi sana vichwani [emoji848][emoji34]
 
Mnakaza mafuvu weeee kuwa Jamaa alikuwa Fisadi, haya wekeni hapa ushahidi ufisadi wake ulifanyika vipi [emoji848] hamna hata majibu sahihi [emoji849]

Basi tajeni hata akaunti yake 1 aliyokuwa akificha hizo fedha pia hakuna chochote.

Kawadanganyeni watoto ili muendelee kulipwa posho zenu za kuichafua legacy ya JPM [emoji2]
 
Jibu ni hadi pale tutakapopata viongozi wazalendo wapenda Nchi ka ulivyoelezea namna ya kupenda Nchi yako kua ni kua tayari kuipambania kwa namna yoyote ile.
 
Hizi kauli kuna watu hawataki kuzisikia ila kadri siku zinavyo enda zinazidi kuwa kubwa. Kaka subiria matusi kwa watu walio hifadhi mimba za chuki za Mwendazake kwenye mawazo yao.
Wanakuja akina Omusolopagas, Belt, Stuxnet, Mmawia, Allancy, Tindo, Dudus na wengineo [emoji87]

Cha kushangaza zaidi inshu kama hizi wapinzani wameuchuna tu nakati wanadai wana democracy chini ya utawala huu wa awamu ya 6 kuliko enzi za JPM walikuwa hawawezi kuongelea [emoji16]

TZ hakuna cha upinzani zaidi ya ndumilakuwili tu wanaokula kote kote ilimradi matumbo yao yanenepe [emoji23]
 
Paskali umemsagia kunguni kaflag umeona haitoshi unamsagia na dogo
 
Kuna hali ilitulemaza Afrika hasa Tanzania ya kufuata upepo wa viongozi wanaokuwa madarakani ili kulinda maslahi yetu binafsi, hali hii imepatiwa jina siku hizi inaitwa UCHAWA.

Uchawa unamfanya mtu awe kipofu kwa mambo mtambuka, awe barubaru kwa mambo yasiyo na faida kwake wala kwa UMMA mradi tu amejihakikishia kula yake
 
TZ ukipiga hakikisha unakuwa na connection kama akina Rugemarila na upige kingi haswaa, maana waliopo jela wana kesi za wizi wa vitu vidogo vidogo tu tofauti na wale wazee wa Richmond company ni mahela bin mapene [emoji4]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…