Tanzania "Shamba la bibi" hadi lini? Hii Ruby ni yetu. Iweje iko sokoni Dubai na serikali yetu haijui? Nasaidia, mchimbaji huyu, anzieni hapa!

Ona jizi hili!

Hata shimo la choo huwezi kuchimba, utaweza wapi kuzama mgodini mtoto mchele wewe?

Ati tunafia kwenye mashimo! We utakuwa bwa-bwa sio bure!

Mashimo gani unayozungumzia?
Linufaika la mfumo uliopo madarakani awamu hii hilo, wakati mwingine unayapuuzia tu maana yanatamba kuwa ni awamu yao kula keki ya Taifa [emoji851]
 
Bro P SNR
Umeandika Kwa uchungu na emotions, hizo ifs & whys utajipa stress bure!
Wewe lea Tu, forgery nchi hii ni kawaida!
BoT wafanyakazi wanashika mikasi wanakatakata note za msimbazi kisha wanajilipa!
Immigration wanafoji visa na permits so ni kawaida kabisa!

Pop a chill pill!
 
Winza ilikuwa 2006 nakumbuka
2007 mwanzoni hata mm nkikuwa winza

Na ruby ya winza nakumbuka kuna mzee mmoja pale alikuwa anajishugulisha na uchimbaj alikuwa anaitwa mzee mturuchie (marehem sahv)baba Ben yeye ndiyo aliigumia
Ndani kwake walimkuta nayo kama debe 2 aliambulia kupewa fuso na kirolaa
Ndipo mlio ukaitika huko watu tukajazana huko
Ila kwa baday winza mawe yalikata kabisa,sasa najiuliza hii ruby imetokatoka vp huko au iliwekwa
Maana mlio mbona watu hawakuusikia
Kingine nikiangaliaaaaa hiyo ruby mbona inafanana kama ruby ya longido,miamba yake
Maana nakumbuka ruby ya winza ilikuwa ya sensa
Inafanana kdg kama ya mahenge,marombo au mtopwesh

Ova
 
Hata tusijifanye tunashtuka.

Tuliibiwa, tunaibiwa na tutaendelea kuibiwa sana tu nchi hii mpaka siku tutakapoamua kuitoa madarakani.
 
Tunashangaa jiwe moja la ruby ilhali watu walishasaini mkataba wa mgodi mzima wa dhahabu Hotelini huko ughaibuni ?? Au tumesahau ?? Hiyo ndio inayoitwa KAZI NA BATA !! Mmesahau tulikuwa tunagawiwa asilimia tatu kwenye migodi wenyewe wazungu wanachukua asilimia 97% ?? Ndio maana mkiambiwa hii nchi ni tajiri msibishe !! Mwalimu kipindi chake alikataa madini yasichimbwe kwa kuogopa kutapeliwa na mikataba yao ya kinyonyaji akasema yaacheni hayo madini yakae huko chini ya ardhi mpaka wenyewe watakapojua kuyachimba na thamani yake ndio watayachimba bila kunyonywa !! Matokeo yake ndio haya sasa waliokuwa wanasubiriwa waelimike kwanza Ndio wamekuwa wakiingia mikataba ya ajabu ajabu ya madini !! Na kuhusu hilo jiwe ruby haiwezekani Hao jamaa wadai kwamba limechimbwa Tanzania kama hawana documents za ku- surport madai yao !! Je ni akina nani waliotoa hizo documents ?? Iko kazi bandugu !!
 
Hiloo jiwe sijui imekuaje likawa na thamani kubwa hivyoo.


Mama atulie nyumbani.

na kauli za kula kwa urefu wa kamba achane nazo.
Kuna uhusiano gani kati ya jiwe na mama kukaa nyumbani....


Kama wizara zinazohusika na serikali kwa ujumla zimeshtuka baada ya kupata taarifa hizi kwenye mitandao ya kijamii.
Jua jiwe limetoroshwa wakati/Huenda likitoroshwa mama alikuepo.
 
Wee msaka tonge unaya jua machungu aliyo yapata aliyeichimba? Leo hii unadai hilo jiwe ni lako / lenu na angekuuzia wewe ungempa shilingi ngapi kama usinge mdhulumu??? Laiti ungeyajua mateso wanayo pata ‘wachoji’ pindi wanapo tafuta sijui kama unfekuja na ki hzi kama hiki…,
 
Paskali anajiuliza "hadi lini".wakat jibu analo.ni hadi tuondoe tamaa binafsi na kueka maslahi mapana mbele.
Lini tutaweza ndio hatujui.
Lingepita njia halali, njia hiyo ingepindishwa tu ili watu wajinufaishe binafsi. (Huenda ndio ilivokuwa.nan ajuae)?
 
Kwani kati ya hela zinazoripotiwa na CAG kuwa zinapotea/tumiwa vibaya /fisadiwa,na mrabaha ambao tungeupata. Lipi tungekipa kipaumbele.
80/20 rule.
 
Uzalendo wa kweli utaonekana pale ambapo serikali itaonekana inawasaidia wananchi badala ya kuwazuia, nyang'anya, toza Kodi isiyoeleweka n.k.
Lazima ifike wakati ambao wachimbaji watasimamia na kuamua kuhusu uuzajji wa madini yao, wakulima mazao yao, wavuvi samaki wao na hata wafugaji mifugo yao.
Watumishi wa serikali ambao hawajui gharama na mateso ya uchimbaji na taasisi zao hawaaminiki kwa wachimbaji.
Umasikini wa Afrika una misingi katika fikra za viongozi na taasisi za serikali dhidi ya raia hasa wale asilia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…