Tanzania "Shamba la bibi" hadi lini? Hii Ruby ni yetu. Iweje iko sokoni Dubai na serikali yetu haijui? Nasaidia, mchimbaji huyu, anzieni hapa!

Mkuu umemaliza yote hii issue haiko sawa haijulikani limechimbwa wapi,pili ruby ya longido haina bei na rangi haijaiva...ruby ua winza sijui rangi ila bado haiwezi kua na hiyo thamani waliosema,tunalishwa matango pori
 
Hili jiwe liliibwa kipindi cha JK miaka kumi nyuma. Sasa hivi JK anazunguka USA, ulaya kama Hana akili nzuri, kuna mambo mazito yanakuja kuangamiza taifa kwa kupitia huyu jamaa stay alert. Especially kwenye madini.

 
imelipwa kodi sh ngapi? unadhani madini yanauzwa kama maandazi? lazima kodi ilipwe kabla ya kuuzwa!
 
Tulieni yule mmarekani wa Dubai kakubali kutoa kishika uchumba cha dola 20m, mazuri yanafuata
 

Hii Rubi ilitoroshwa nchini kabla ya 2005, hata JK hajawa rais.
P
Kuna thread moja niliyi iona leo JF kwa mujibu wa Waziri Biteko anadai likitoroshwa miaka 11 (2011) iliyopita na wanayo majiwe mengine 25 yenye uzito tofauti na yote yametokea Tanzania.


Tuwe wapole kwani hayo mawe ndio Baba Jen.
 
kama kitengo cha uhamiaji wanatoa stika feki kuna tass gani ambayo haipg dili tatizo wafanyakazi wa serikal wana ubinafsi
 
Paskali nimekupa like hapo umeiona!!??? Watu kama nyie ndio hasa wanatakiwa ktk nchi hii ila bahati mbaya mmezaliwa katika nchi ambayo trending stories ni Masha love,Juma Lokole stories,Mange kimambi na upuuzi kama huo...Lakini kitu ambacho kilitakiwa kiwe mjadala kama hilo jiwe hapo ni habari isiyopewa kipaumbele kabisa kwenye nchi hii
 
Tumefika hapa,na tunaendelea kufanyiwa ujanja ujanja sababu ya CCM, acha tuendelee kufanyiwa tunayofanyiwa kama vipofu
 
imelipwa kodi sh ngapi? unadhani madini yanauzwa kama maandazi? lazima kodi ilipwe kabla ya kuuzwa!
How do you issue a certificate without valuation? Kodi hulipwa on the basis of the value of the gemstones. Utaratibu ikoje wa kutoa certificate? Certificate hutolewa baada ya kodi kulipwa.
 
Mkuu pascal Mayala kama twiga aliweza kupanda ndege na kutoroshwa inakuwaje unashangaa jiwe la kilo mbili kutoroshwa?
Mkuu The lost , nikurekebishe, wale Twiga, hawakutoroshwa!, kuna mtu alipewa zawadi hao Twiga, ila ilikuwa iwe discreet, ndio maana wakabebwa usiku wa manane. Kwa bahati mbaya kuna wambea waliona ndio wakapiga kelele, sasa ili kuzima soo ya mtu kutoa zawadi ya nyara, ikabidi maofisa wazuge hao twiga wameibiwa!. Ukweli ni kuwa hao twiga wawili, jike na dume,hawakuibiwa, kuna mtu alipewa zawadi, aliyewatoa zawadi tunamjua, walipokwenda tunapajua. Ili kuthibitisha Twiga hao hawakuibiwa, ndio maana hapo walipo, wako mpaka sasa tena habari njema, wameisha zaa mara mbili!. Hapo walipo, Watanzania tunakwenda sana, na kuwafurahia!.

Kwa vile kina ndege kabla haijatua uwanja wowote, lazima itoe flight data na manifest, ni ngega gani, ya nani, inaendeshwa na nani, na imetoka wapi, imebaba nini, ina crew wangapi, ina abiria wangapi etc. Ikiisha tua, hizo taarifa zinathibitishwa, kama imeleta mzigigo inapokelewa inagaguliwa, kama ni abiria wanakaguliwa ndio wanaruhusiwa kuondoka nchini.

Vivyo hivyo, ndege ikiondoka, kabla haijapewa clearance, flight details zinakuwepo, haiwezekani twiga wameibiwe hatujui!, ndege hiyo tunaijua ni ya nani, inaendeshwa na nani, imekwenda wapi, hivyo twiga wangeibiwa tungeripoti interpoli, walipofika kule walikopelekwa wangekamatwa na aliyewaiba kulazimishwa kugharimia kuwarejesha, lakini hatujafuatilia popote!. Hivyo amini twiga wetu hawakuibiwa bali walitolewa zawadi, atoa zawadi anafahamika, mpokea zawadi anafahamika, walipo panafahamika, ila naombo tuu usiniulize mimi nikutajie, kwasababu, kuna taarifa nyingine sisi waandishi tunazipata as prileged information, yaani unapa taarifa kwa taarifa yako tuu, FYE only na sio kuzitangaza, kama ile siku nilipopata taarifa hii Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Hapa sijashangaa jiwe kutoroshwa!, nimeshangaa serikali kutokuwa na taarifa!.
P
 
Naona jamaa wanaraise doubt kama kweli hiyo ndio thamani yake.
Mkuu Statesman , doubt zao ni za kweli, lile jiwe ni ruby ya Longido, rubby ile haina thamani kivile, kwasababu ni mjiwe mkubwa tuu lakini ruby halisi ni kidogo sana. Sasa matapeli wakacheza dili, wakaichukua ruby ya Longido na kuitengenezea a face certificate of orgin ili kuonyesha imetoka Winza, Dodoma!, kisha wakaitengenezea a fake waluation certificate ionekana ina thamani kubwa, wakati its not true. Mnunuzi akadanganyika kuinunua, alipogundua amedanyangwa, na yeye akaiuza kwa tajiri wa Kiarabu kwa utapeli vile vile, tajiri wa Kiarabu bila kujua jiwe ni fake, ndio kaingiza nzigo sokoni.
P
 
Hao uliowataja, hoja zao, ndicho Watanzania wanapenda kusikia. Mfano angalia bandiko hili kuhusu hii ruby, lilibandikwa lini humu jf, angalia lilibandikwa lini na lilichangiwa na watu wangapi Rubi ya Tanzania ya thamani kubwa Duniani ilienda UK Kihalali au Iliporwa?
Leta habari za Daimond na Wema, Zari etc uone jinsi michango ikimiminika.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…