Dunia ina umafia mwingi saaana..
Biashara ya madini inamilikiwa na cartels fulani ambazo zina matawi kila mahala na zipo kuhakikisha maslahi ya mabwanyenye yanastawi.. Kudeal na huu umafia kunahitaji akili kubwa zaidi ya hizi akili za kina Joti na Mpoki...
DRC ni nchi kubwa sana yenye madini kila mahala lakini ukiwa pale Lubumbashi aka Katanga province utakuta raia wana njaa na umasikini japo huko polini mamafia wa dunia wanakamua watakavyo midege ikitua na kuruka
Kifupi nchi imetekwa na wahuni ndio wanaimiliki.
Tanzania iko mikononi mwa wahuni toka enzi za uhuru, madalali wa hao wahuni tuko nao tunaishi nao na wengine tunaamini kama ndugu zetu but they are here purposely, Kupitia hao madalali ndio hata uongozi wa juu na maeneo nyeti wanapatikana watu.... Kuvuka hiki kikwazo na kuukata mnyororo wa wahuni huhitaji demokrasia bali unahitaji kiburi, unyama, kutojali na ukatili mwingi, ukiwavuruga ndipo utapata nafasi ya kuset na kuokoa maslahi ya Taifa...
Watanzania kwa kupenda maisha mazuri mepesi wamegeuka maagent wa cartels na kusaidia ustawi wao pale penye ugumu, Cartels hizi zimejipenyeza Kanisani, misikitini, Kwenye vyama vya siasa na kila penye influence ili kulinda maslahi yao kila yanapoingiliwa..