Siyo mfumo wa Kijamaa ndugu yangu, ni sheria za nchi. Hata Marekani kwa baba wa ubepari kuna sheria za madini, kwa mfano huwezi kuuza madini ya uranium bila kupata kibali cha serikali, na huwezi kuuza baadhi ya products unazotengeza mwenyewe kwa mfano electronic components, infra red sensors, na optical gryoscpes bila kupata kibali cha serikali.
Urusi na China ndiyo basi kabisa, madini yote ya rare earth minerals yaliyoko China ni mali ya serikali tu. Halafu pia madini yote yaliyoko kwenye ardhi ya Urusi, pamoja na kuwa kuna makampuni binafsi yanayochimba, lakini lazima mauzo yake yarekodiwe serikalini. Sasa wewe sijui unataka system ipi hiyo isisyosimamiwa na serikali kuhusu raslimali za nchi.
Sikiliza hii kuhusu madini ya Uranium Marekani