Naona kama huielewi dunia hii bali unaongea nadharia tupu ya kujitungia tu. Usidhani kama China eti ilifungua nchi yao wakawaachia wawekezaji wajifanyie wanavyotaka kama unavyodhani. Jinsi China ilivyofungua kuwaita wawekezaji ndiyo hivyo Tanzania pia tuliwata wawekezaji. Ila China ilibaki na mashirika yake ya umma umma, na mojawapo ya masharti kwa wawekeaji kuruhusiwa kufanya biashara zao ndani ya China ilikuwa ni lazima washirikiane na wawafundishe wachina. Tofauti yake Tanzania tukauza mashirika yote ya umma wala hatukuwa na mpango wa kufanya wawekezaji hao walisadie Taifa; tuliwapa tax holidays za ajabu. Baada ya miaka kama kumi tu, wachina wakaanza kuendeleza mashirika yao kwa kutumia technology waliyojifunza kutoka kwa wawekezaji na kuanza kukataa bidhaa zilizozalishwa na wawekezaji hao. Sisi baada ya muda mfupi tu mashirika yote ya umma yakafa tukawa wategemeaji zaidi wa nje, na mpaka leo tunaendelea kubembeleza wawekezaji miaka yote 35 iliyopia tunalia na ujamaa tu.
Makampuni na mashirika yote makubwa unayoyajua kutokea China ni ya serikali; mifano michache ni kama vile kampuni ya TV ya Hisense, kampuni ya kutengeza ndege ya COMAC, Benki kubwa sana inaylipia miradi mingi ya ujenzi wa majumba na miundoa mbinu ya CCB ni mali ya serikali, Kampuni ya reli ambayo ndiyo imetengeza zile high speed train ya CR ni mali ya serikali, Migodi yote ya madini China ni mali ya serikali. Makampuni yote makubwa ya kutengeza magari kama SAIC, Dongfeng, FAW, Chang'an, BAIC,GAC na mengine mengi sana ni mali ya serikali, China bado wanaendelea na ukomunist twao tu, hakuna chama cha upinzani China, bali ni chama cha kikomunist tu, kuipinga serikali au kum[pinga rais China ni kosa la jinai.Sasa sijui undhani tofauti yao na ujamaa ni ipi.
Kwa nini hutaki kukubali kuwa Tanzania hatuna kisingizio bali ni sisi wenyewe? Hata Rwanda sasa hivi wanatupita standard of living wakati walichinjana sana miaka 28 tu iliyopita. Tunataka vya ulaini mno, tukisimamiwa kufanya inavyotakiwa tunalia na udikteta, tukiachiwa tujifanyie bila kusimamiwa tunaharabu hadi kukwama na wengine kama wewe kuanza kulaumu ujamaa uliokufa miaka 38 iliyopita; solutiona yetu ya haraka huwa ni kutembeza bakuli duniani na kutafuta mikop[o. China mtu akishikwa kwa rushwa, wizi wa mali ya umma, au madawa ya kulevya anayongwa; sisi kwetu tutamchekea tu na kumwona "mtu wa misheni town."
Wachina waliokufa kipindi cha mao hawana uhisnao wowote na kuendelea kwa china au kutokuendelea kwa Tanzania.