Nasikitika kuona logic ya Mzee ES imekuwa tena ya wasiwasi. Tunataka kuvutia watalii wengi
kwa faida yetu, sio kwa
faida ya hao watalii. Mwaka jana, tulipata watalii
laki sita, na waliingiza fedha za kigeni
$700 million. Mazao ya kilimo yaliingiza chini ya $500 million.
Mzee ES, iweje ukemee watu kuishi na mbuzi na kuku na huku unataka tuendelee kukazania majiko ya mafuta ya taa? Inabidi kukumbatia mabadiliko ya kuleta maendeleo moja kwa moja, sio nusu nusu
. You cannot be a little bit pregnant.
Mzee wa kijiji anasema haiwezekani kuleta maendeleo kwa kutegemea utalii na madini. Mbona Misri imeleta maendeleo (relatively) kwa kutegemea utalii? Nguvu ya uchumi wa Kenya ni utalii. Mwaka huu, Kenya wanatarajia watalii 1.8 mil. That should bring in about $2.5 billion. Yaani Kenya itaweza kuingiza zaidi ya nusu ya fedha za bajeti yote ya tanzania kwa njia ya utalii peke yake.
Inabidi tulime, kwani kama alivyosema Mwalimu,
tusipolima tutakufa. Lakini, ili kupata fedha nyingi za kigeni, inabidi kukazania zaidi utalii.
Utalii ndiyo sekta yenye uwezo mkubwa kuliko zote Tanzania, wa kuingiza fedha nyingi za kigeni.
Nashauri msome vile vile hii paper kuhusu bajeti ya kilimo (2006) ambayo imeandikwa na mtaalamu wa SUA.
Iko hapa:
Augustine Moshi