Tanzania (Taifa Stars) vs Morocco

Tanzania (Taifa Stars) vs Morocco

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2009
Posts
5,471
Reaction score
752
Kama kawaida nishafika uwanjani, timu zote zishaingia na zinapiga jaramba hawa Wamorocco wanaonyesha wako fiti na wepesi na wazee wa touch sana inabidi tutulie kama twahitaji kuondoka na chochote...JK bado hajaingia na mashabiki ni wengi kiasi...

Ngassa tupe rahaa mwana


=========
======================
HABARI PICHA ZA MCHEZO HUO


Wapenzi wa soka kutoka ndani na nje ya Dar es Salaam na hata nje ya mipaka yetu walihudhuria kwa wingi.Ilikuwa ni mwendo wa VUVUZELA kama soccer city vile.


Kikosi cha timu ya Taifa Morocco kikiingia uwanjani kwa ajili ya mazoezi madogo madogo yajulikanayo kama Warm Up.


Kikosi cha Timu ya Taifa Stars kikingia kwa mbwembwe uwanjani kwa ajili ya mazoezi ya Warm Up huku wakishangaliwa kwa nguvu zote.

Mrisho Ngasa (kulia) akiwa na Nadir Haroub Canavaro (kushoto) wakionyesha ufundi katika kuchezea mpira kabla ya mchezo kuanza.

Pamoja na washabiki wengi kuja kushangilia Taifa Stars lakini pia macho yao yalielekezwa kwa kijana mwenye jezi namba 17 Marouane Chamakh ambaye anakipiga kule katika ligi kuu ya Uingereza ndani ya Club ya Arsenal.hapa akiwa anapasha na wachezaji wenzake.

Walinda mlango wa Timu ya Taifa wakionyoosha viungo kabla ya mpambano.

Timu zikiingia uwanjani tayari kwa mtanange hapo ilikuwa nimwendo wa VUVUZELA.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akielekea katika kukagua vikosi vya timu zote mbili huku akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa TFF.

"Vijana leo fanyeni kweli sioni kwa nini tushindwe kama Algeria tulitoa nao suluhu na tulikuwa kwao"


Juma K. Juma (katikati) akiwa na Stephano Mwasika(3) pamoja na Shadrak Nsajigwa (13) wakiimbia wimbo wa Taifa.


Rais JK akipungia mashabiki waliohudhuria baada ya kukagua vikosi.

Makapteni wa timu zote mbili pamoja na marefarii wa mchezo huo wakiwa katika hatua za mwisho tayari kuanza kwa mechi hiyo.

Kocha mkuu wa timu ya Taifa Jan Paulsen akiwa na benchi lake la ufundi.

Benchi la ufundi la Morocco.

Suleimani Rashid(3) Morocco akimkaba Shadrak Nsajigwa (13) wakati Taifa Stars bikipeleka mashambulizi.


Danny Mrwanda (7) akijaribu kumtoka Kantari Ahmed (15) wa Morocco.

"Tunajua uko nyumbani na sisi tunahakikisha hampati upenyo"

Lamyaghri Nadir ambaye ni mlinda mlanggo wa Morocco akiwa katika pilika pilika ndani ya mchezo huo.

Wachezaji wa Morocco wakiwa wamejipanga tayari kuzia mpira wa kona uliokuwa ukielekezwa langoni kwao.
 
Supwersport wako kikazi zaidi kwa haraka haraka naona wameset kamera kama 12 hivi si mchezo
 
Supersport wako kikazi zaidi kwa haraka haraka naona wameset kamera kama 12 hivi si mchezo
 
Kama kawaida nishafika uwanjani, timu zote zishaingia na zinapiga jaramba hawa Wamorocco wanaonyesha wako fiti na wepesi na wazee wa touch sana inabidi tutulie kama twahitaji kuondoka na chochote...JK bado hajaingia na mashabiki ni wengi kiasi...

Ngassa tupe rahaa mwana

Angalia usiripoti umbea kuhusu JK. Utanyang'anywa kitendea kazi.
 
Angalia usiripoti umbea kuhusu JK. Utanyang'anywa kitendea kazi.
Mheshimiwa rais kawapungia mashabiki na alikuwa anasalimiana na wachezaji kwa kugongeshana mabega (ushkaji?) na anatabasamu muda wote
 
Stars wanafanya shambulizi la kwanza zuri lakini umaliziaji (kama kawaida) ni tatizo sana. Kaseja ndiye kaanza golini
 
Stars wanajitahidi, wanaanza vizuri na kutia moyo. Dakika ya tatu inakwenda hiyo
 
Vijana wameaanza kwa kasi hapa hadi golini kwa Morocco, TFF wametia aibuu nyimbo za taifa hazijapigwa JK kammind Tenga sana hata hivyo big screen ya uwanjani inaonyesha live thanks to SS3
 
Back
Top Bottom