Tanzania (Taifa Stars) vs Morocco

Tanzania (Taifa Stars) vs Morocco

Kama kawaida nishafika uwanjani, timu zote zishaingia na zinapiga jaramba hawa Wamorocco wanaonyesha wako fiti na wepesi na wazee wa touch sana inabidi tutulie kama twahitaji kuondoka na chochote...JK bado hajaingia na mashabiki ni wengi kiasi...

Ngassa tupe rahaa mwana

Ngasa alishahama Yanga. Umesahau?
 
Stars wanacheza vizuri sana katikati mpaka sasa, tatizo ni umaliziaji ninavyohisi
 
Nina wasiwasi kama wewe ni Mexence kweli. Mimi siwezi kukupigia simu. Laini yangu nimesajili. hahaha!
Ni mimi mkuu. Mimi pia nimesajili hahahahaha

Morocco wanaanza kushambulia sasa, dakika ya 5
 
Dakika ya 8 inakwenda, bado mambo ni Tanzania 0 - 0 Morocco
 
Ahasnteni... endeleeni kutuhabarisha. Tupeni na full lineup.
 
Vipi fulana za Chama zipo hapo?
JK hajavaa fulana hizo, sidhani kama watanzania wanaweza kuigeuza mechi hii ya chama.

Nizar kafanya shambulizi la kwanza zuri kiasi chake.

Tumebanwa, dakika ya 13 Morocco wanapata kona
 
Ahasnteni... endeleeni kutuhabarisha. Tupeni na full lineup.
Ntajitahidi kusaidia nikiweza. Kuna Nditi, Mrwanda, Joseph, Nsajigwa, Kaseja, Nizar n.k

Nikiwaona naandika maana wengi siwajui kusema ukweli.

Dakika ya 16 inaenda hiyo
 
JK hajavaa fulana hizo, sidhani kama watanzania wanaweza kuigeuza mechi hii ya chama.

Nizar kafanya shambulizi la kwanza zuri kiasi chake.

Tumebanwa, dakika ya 13 Morocco wanapata kona

wacha niwe mzalendo kwa dakika 70 zilizobaki.

naenda baa kuchek mechi.
 
Aisee pamoja na kwamba link zenyewe inaumiza macho, lakini naona wachezaji wetu wanakimbiakimbia tu bila malengo.
 
Huyu Ngassa tangu asifiwe na Wenger basi imekuwa tabu, kila wakati anataka a-dribble..
 
Back
Top Bottom