Tanzania (Taifa Stars) vs Morocco

Tanzania (Taifa Stars) vs Morocco

Sisi tuna matatizo sana .. tunacheza mechi sana kwenye magazeti na Radio , uwanjani hatuna kitu..
kweli kabisa kaka,tunacheza mpira wa jukwaa wachezaji wetu,wakishangiliwa badala kutoa pasi anataka kufinya kanzu yani wanaona wasipopiga chenga wataonekana hawajui mpira,wanajua mpira ni kujua kupiga chenga na kukaa nao,hakuna hivyo tutaisha kila siku chenga twawala lakini twafungwa,hakuna kitu kabisa,kwa mtaji huu sijaona hata mchezaji mmoja mwenye sifa za kucheza ulaya hususan timu kubwa,tutaishia kucheza uarabuni tu ulaya wakijaribiwa watashindwa maana hawakuonyesha hata akili ya kutafuta goli,shambulizi ni moja tu shuti la mrwanda.
 
Hapa kwetu tanzania tatizo kubwa tulilonalo katika soka ni kukosekana kwa wachezaji wenye vipaji!Hata tufanyeje swala litabaki palepale,vipaji ni kitu muhimu katika soka!
 
Hapa kwetu tanzania tatizo kubwa tulilonalo katika soka ni kukosekana kwa wachezaji wenye vipaji!Hata tufanyeje swala litabaki palepale,vipaji ni kitu muhimu katika soka!
kaka ngoja nikujibu kidogo,kuhusu vipaji kila nchi dunia kuna watu wenye vipaji vyao,tz wenye vipaji wapo kuanzia michezo hadi ktk elimu,tatizo ni wa kuviendeleza,naweza sema tumekosa msimamizi mzuri wa michezo hususan ktk sekta ya soka,hapo namaanisha makocha wanoujua mpira wa ushindi na wenye kubadilisha timu na wachezaji hususan wenye vipaji kuwa balaa zaidi,wapo wenye vipaji vya kina messi,ronaldo nk sema wamekosa muendelezaji wa vipaji vyao ndio hata ktk elimu wapo wenye vipaji vya kuvumbua vitu ila wamekosa muendelezo hasahasa kutokana na sera zetu mbovu ukijumlisha na umaskini,mimi nakuambia hata kama ulikuwa hujui mpira kabisa hata kuunyanya kupiga danadana na hata kupiga kulenga goli,ukipata mapromota niwaite utajua tu,nchi za ulaya hususan england wachezaji wake wengi ni mpira wa darasani,na hawataki masihara na kufunga wao wanataka bora goli sio goli bora,goli bora litakuja baadae kama kutakuwa na mazingira ya kutengeneza goli bora,ila kwetu tunapenda magoli ya video sana ndio tatizo letu kubwa,kifupi management bongo ni mbovu sekta zote,yani somo la uongozi,usimamizi bongo bado kwa kweli,umeona hata kabla kuanza mpira nyimbo za taifa zimepigwa kuanza kwa 2nd half,yani hatupo nikiazima kamusi wanasema organized yaani hatujiandai mapema.
 
Hapa kwetu tanzania tatizo kubwa tulilonalo katika soka ni kukosekana kwa wachezaji wenye vipaji!Hata tufanyeje swala litabaki palepale,vipaji ni kitu muhimu katika soka!
Wachezaji wenye vipaji wapo,tatizo hatuko serious na tumeichukulia soka kama burudani na ndiyo maana hata sisi mashabiki tukishaona mchezaji kapiga chenga tunaridhika nae na kumpamba sana.

Bado tumegubikwa na kuchomeka vijeba kwenye timu za vijana ili kupata ushindi rahisi na ndo maana hata ile Serengeti boys ya Gambia(Nurdin Saga) wachezaji wake wengi ni vijeba kuliko Hussein Masha na wakati wakati huu ndo walitakiwa wawe wamejaa Stars,mbona Nizar na Nurdin bado wapo!

Na hata falsafa ya kocha wa stars si nzuri kwa sababu anataka timu ikabe sana na ikashambulie kwa counter attack,hapa ni vigumu kwa aina ya wachezaji tulionao. Kocha kama anataka ushindi awatumie washambuliaji asilia wa kati, kama Tegete na John Boko ili wazoee kucheza na waweze kujiamini zaidi.
 
Dar es Salaam - TAIFA Stars coach Jan Poulsen admitted that Tanzania now faces an arduous task in their 2012 African Cup of Nations (Afcon) qualifying campaign following 1-0 loss against Morocco, but believes his side performed well and has bright future.
Stars Danish tactician Poulsen was left frustrated after his players failed to take advantage of long periods of territorial dominance at the National Stadium in Dar es Salaam on Saturday.

"Our chances (of qualifying for the 2012 finals) have gone down a little bit because we have lost the match of course, that is how it is," conceded Poulsen after the match.
And Poulsen lamented his team's lack of cutting edge as the reason behind their failure to capitalize on the home ground advantage, but couldn't complain losing against a team of Morocco's stature.
"We had a lot of possession but we didn't create so many chances, my players worked very well, they showed commitment but we need to create chances and score goals. I must say congratulation to Morocco, they have a good team, I don't think you can say anything to Morocco winning one nil.

"I think we gave Morocco a good match, we enjoyed a lot of possession," said Poulsen who conceded that his team came up against tough opponents; "There are some aspects of the game where you can see that we played against players at a high level."
Poulsen held that Taifa Stars' lack of cutting was a reflection of the problem of creative players and attackers also seen in the premier league.
"It is the problem you also see in the league that we had difficulties of creating the chances, of course you had to say that Morocco's defence was big and strong and played very well."
However he challenged his players to increase the tempo of their attacks when in opponents' area, "We need to play a faster game in order to get into the box most often and maximize our scoring chances."

He said Stars need to have one or two players who can make difference up front by creating and scoring goals against any strong defence, "That is what we have to look for."
Most soccer analysts who watched the match beamed live on SuperSport said Tanzania have little chance of ending its 30-year wait for a place in the continental finals unless they improve on the quality of finishing they showed against Morocco.
The Dane defended his tactics of deploying Mrisho Ngasa upfront with Danny Mrwanda playing as second striker and refuted suggestions that the Azam striker lacked support for most of the game.

"If you look, Danny was very close to him all the time, so I don't think he was a lone striker, like Nigeria play the same way, Danny is striker, we have Nizar (Khalfan) can go forward, but I must agree that we need to be more compact upfront."
In the end Poulsen believes that the future is still bright for Tanzanian team, "If we can keep this team together and if we can get some of these young players improving their game, the future looks okay for Tanzania."
Morocco's attacking midfielder Houssine Kharja who plays for Serie A club Genoa and the team's caretaker coach Dominique Cuperly hailed Stars' performance and conceded that the hosts gave them a torrid afternoon.
Kharja said: "I think that they are very good, it was very difficult game because Tanzania is a team that plays good in defence and they have very good counter attacks, I'm so happy that we won."
Kharja believes Morocco are making good progress after a slow start to their campaign following a goalless draw against Central Africa republic.
"Now we're better because we had a lot of players injured, but now the guys are coming back and I think that we can play better and we can make a very good qualification and now we have to take on Algeria it is a very difficult game."
The loss, Tanzania's first of the campaign, leaves Poulsen's men on one point after two games while Morocco improved to four points in Group D. The other teams in the group, Algeria and Central Africa Republic met yesterday.
 
Wachezaji wenye vipaji wapo,tatizo hatuko serious na tumeichukulia soka kama burudani na ndiyo maana hata sisi mashabiki tukishaona mchezaji kapiga chenga tunaridhika nae na kumpamba sana.

Bado tumegubikwa na kuchomeka vijeba kwenye timu za vijana ili kupata ushindi rahisi na ndo maana hata ile Serengeti boys ya Gambia(Nurdin Saga) wachezaji wake wengi ni vijeba kuliko Hussein Masha na wakati wakati huu ndo walitakiwa wawe wamejaa Stars,mbona Nizar na Nurdin bado wapo!

Na hata falsafa ya kocha wa stars si nzuri kwa sababu anataka timu ikabe sana na ikashambulie kwa counter attack,hapa ni vigumu kwa aina ya wachezaji tulionao. Kocha kama anataka ushindi awatumie washambuliaji asilia wa kati, kama Tegete na John Boko ili wazoee kucheza na waweze kujiamini zaidi.

Huyu Nizar ukienda website ya Vancouver Whitecaps ambao next year wanacheza ligi kuu ya USA ama MSL eti ana 23 years old kazaliwa 1988!?>
 
Wachezaji bado kabisa wanakosa vitu vya msingi hapa hata akija kocha gani kazi ipo.Makocha wa klabu wanapaswa kumrahisihia kocha wa timu ya Taifa kazi
 
Timu yenyewe hajakaa kama ya Muungano! Safi sana Algeria Nadhani Kikwete aliweka mkosi
 
Huyu Nizar ukienda website ya Vancouver Whitecaps ambao next year wanacheza ligi kuu ya USA ama MSL eti ana 23 years old kazaliwa 1988!?>
Hapa ni utata mtupu,japo siwezi kuthibitisha,lakini tatizo hili ambalo ni kama donda ndugu, lilikuwepo tangu enzi za UMITASHUMTA,ambapo wachezaji, hasa wa soka na riadha hawakuwa halali, walikuwa ni mamluki wakawa wanachomekwa ili mradi mkoa uchukue medali na si uhalali wa medali zenyewe.

Sasa vijeba hawa, baada ya UMITASHUMTA kwisha wakawa wanachukuliwa na Kipingu kwenda pale Makongo,wengine wakafaidika kwa vile walirudi shule ila kuna wale ambao waliona kama shule inawapotezea muda wakarudi kuendelea na shughuli zao,sasa miongoni mwa walioendelea kusoma wakaunda Serengeti boys huku wakiwa vijeba.

Kama kuna mtu ana kumbukumbu nzuri kuna timu halisi ya U17 iliundwa mwaka 1992, ikacheza na Guinea U17 pale Taifa ,miongoni mwa wachezaji waliounda timu ile ni pamoja na Masumbuko Hassan, Juma Waziri,Jmanne Ahmed,Ally Abdallah Saleh,Odo Nombo nk.Baada ya kutoa droo na Guinea,tukenda kwao tukapigwa 2-0, ile FAT ya Alhaj ikaamini tulifungwa kwa sababu wachezaji wetu wana miili midogo kwa hivyo suluhisho ikawa ni kuchukua wachezaji wa ligi kuu na tena wenye miaka 24 na kuwarudisha umri mpaka miaka 17. Na ndipo tulipopotea na kuendelea na mtindo huu wa kufoji umri mpaka leo.So hatujui umri halisi wa ukweli wa wachezaji hata tulionao sasa,na ndo maana timu ya taifa inaundwa na wachezaji walioibuka juu kwa juu,kwani hata mbuyu ulianza kama mchicha!
 
kwa upande mwengine naona bora turudi kuanza kwenye sifuri, ukiangalia miaka yote timu zile zinazoingia fainali ya mashindano haya ama kombe la dunia basi zinakuwa na wachezaji wa kulipwa kwenye vilabu vikubwa bara la ulaya,(Ghana, Nigeria, Ivory coast, Egypt, Algeria, Morroco, S. Africa nk. wote hawa wachezaji wao wamesambaa ulaya) tusijidanganye katu haitatokea miujiza ya timu yetu hii kwenda fainali kwenye major competition yoyote.
Kwa hivo ni muhimu tukaelekeza nguvu zetu kwenye academies, na tuanze kuunda system na kuwaandaa vijana kuanzia miaka 7,(under7, 10, 13, 16, 18 na 21) badala ya kupoteza fedha kwenye makocha nk na tutumie hela tujenge academies za uhakika, pengine baada ya miaka 10-15 tutaanza kuvuna matunda.
Mpira hivi sasa uko level nyengine, haiwezekani wachezaji wetu akina Ngasa waweze kushindana na wachezaji kama akina Charmakh, Essien, Drogba Boetang etc. Hawa wameanza kuandaliwa mapema na wamewazidi mno wachezaji wetu kwa kila nyanja, huku kwenye academies huwa wanafunzwa mengi tokea bado wadogo sana kuanzia Discipline, Technical coaching, sports science, education and welfare, life skills vilevile wanazo 1st class facilities (Gyms, trainning gears, Classes, medical etc.)
Kama kweli kama tunataka mafanikio na tuanze huku venginevyo tutaendelea kuwa wasindikizaji.
 
Back
Top Bottom