Ushauri wa Zitto ufuate, pesa yote ya michezo ya kubahatisha ipelekwe kwenye michezo. Huwezi kufanikiwa bila kuwekeza. Jk alianzisha uwanja bora kabisa lakini umekua wakupigia selfie. Tatizo bajet hakuna.
Lakini pia watanzania tunapenda mawaziri wa chache wenye majukumu mengi bila kujua athari zake, utasikia mtu anaitwa waziri wa Habari, sanaa, utamaduni na michezo. Kwa bajeti gani na kichwa gani abebe hayo mambo yote? Ona sasa week hii TFF walikua bize kufungiana wizara nayo ilikua bize kupambana na wasanii matokeo yake tumepigwa tobo.