Tanzania(Taifa Stars) yanyolewa bila wembe na Algeria goli 4 kwa 1

..... HAKUNA KITU AMBACHO SIKIWEZI MAISHANI MWANGU KWA MIAKA YA HIVI KARIBUNI KAMA KUTAZAMA MECHI YOYOTE YA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA.
 
Hee, lini hiyo tena timu ya taifa tz imepigwa goli nne?
 
Tatizo ni TFF maana ndiyo wenye jukumu la kusimamia mpira nchini. mbaya zaidi FIFA hawataki serikali iingilie mpira vinginevyo jiwe angeshawatumbua na angekuwa kafanya kazi nzuri sana. TFF wanawaza matumbo ma si mpira wetu.
Hapa kama serikali ingeruhusiwa kuingilia huoni kama yule naniliu angeshaingilia na KUWAFUNGIA baadhi ya wachezaji?
 
Kipigo cha goli 4 kwa Timu yetu ya Taifa dhidi ya Algeria Tatizo la msingi ni nin hasa...? Lakini nini kifanyike tutoke hapa tulipofikia

Comrade, yaani unataka kusema hujui tatizo au matatizo ya soka ya Tanzania???!!! Matatizo yako wazi kabisa...Kwanza ni uongozi wa soka kutoka kwenye uongozi wa juu kwa maana ya TFF mpaka kwenye klabu...kote huko ni vichaka vya wezi na wababaishaji wakubwa...wanajiita watu wampira lakini siyo wa mpira hata kidogo....rushwa, hongo vimegubika ligi zetu zote za soka...marefani rushwa mtindo mmoja...makocha wanachaguliwa kwa upendeleo...ni hovyo kabisa...Mayanja ana kitu gani cha kujivunia hata awe kocha wa timu ya taifa...hao viongozi ndani ya TFF wana lipi la kujivunia hata wachukue nafasi hizo kwa uchaguzi uliogubikwa kwa rushwa? Mimi ni mwanafamilia ya soka na najua ninachozungumza hapa, na nimewahi kuongoza soka....
 
Hatuna wachezaji, club haziandai wachezaji kuwa na uwezo wakimataifa.
Mchezaji anandaliwa kwenye club kuanzia akiwa mdogo, sasa uku kwetu club hazina academy zitakazo kuza wachezaji kuwa na uwezo mzuri.
Wachezaji wa Tanzania hawana:-
Agility
Match fitness
Technic
Tactical awareness
Sharpness
Passing
Positioning

Hauwezi ukawa na wachezaji wa namna hiyo halafu unategemea watakua na uwezo wa kupambana na wachezaji wenye levo za kimataifa.

Tunatakiwa kuandaa wachezaji kuanzia kwenye grassroot ndio tutaweza kuipeleka Taifa stars afcon.
 
Kipigo cha goli 4 kwa Timu yetu ya Taifa dhidi ya Algeria Tatizo la msingi ni nin hasa...? Lakini nini kifanyike tutoke hapa tulipofikia
Tunaekeza kwenye viwanda na kununua madiwani, tukimaliza tutalitafuta tatizo
 
Tatizo ni TFF maana ndiyo wenye jukumu la kusimamia mpira nchini. mbaya zaidi FIFA hawataki serikali iingilie mpira vinginevyo jiwe angeshawatumbua na angekuwa kafanya kazi nzuri sana. TFF wanawaza matumbo ma si mpira wetu.
TFF ndo wanacheza MPIRA UWANJANI?
kiufupi hatujui kucheza mpira.
acha kumsifia MTU kiboya.
 
Ukweli Ni Kwamba Waarabu Wana Allergy na Hili Jina Tanzania That is why Kuanzia Ngazi Ya Vilabu Mpaka Taifa Wamekuwa Wakitufanya Watakavyo!
Ukweli Ndiyo Huu! Tunahitaji Miaka 300 mbele ili Tanzania tufikie at least Nusu ya Uwezo Wa Waarabu.
Kwa Sasa tuendelee Kupokea Vipigo Kutoka Kwao.
 
Mbona watu tunakuwa wanafiki sana!
Si ni sisi sisi tunaoshangiliaga Simba yetu na Yanga yetu mpaka tunafia uwanjani?

Hizo timu zenu mbili ni mbovu balaa na ndiyo timu yenu ya Taifa.

CCM hawawezi kujinasua kwenye lawama hii. Viwanja vyote wameving'ang'ania wao, haviendelezwi havina taa.

Viwanja vya wazi vilivyokuwa vinatumika kuchezea mpira vingi vimejengwa majengo ya shule, si msingi si sekondari leo wakati wa mapumziko watoto hawana mahali pa kuchezea mpira. Mfano Mwanza hakuna kabisa viwanja vya wazi.

Udhamini uliopo katika ligi kuu na daraja la kwanza ni mdogo sana kiasi vilabu vingi vinashindwa kabisa kujiendesha.

Mimi huwa ninajiuliza, hivi serikali ikitenga walau hata billion 2 kila mwaka kudhamini vilabu vyetu vya ligi kuu itapungukiwa nini, hiyo si inakuwa ni namna nyingine ya kutoa ajira kwa vijana!

Leo Simba na Yanga zinazotoaga wachezaji wa Taifa eti ubora wao ni kuzifunga timu kama Mbao na Toto. Yaani uzifunge timu zenye wachezaji wa kuokoteleza na wenye njaa alafu ndiyo iwe qualification ya kupampana na Aly Misry? Masihara hayo.

Simba ile iliyokuwa inapata nafasi ya kutuwakilisha CAF na kufika hadi fainali ilikuwa kwanza inapitia kwenye tanuru la moto kwa kuzishinda Pamba, Sigara, Reli na Ushirika timu zilizokuwa hazina njaa chini ya udhamini wa serikali ya Mwinyi.

Uimara wa ligi yetu ndiyo uimara wa timu yetu ya taifa.
 
Mpira wa bongo hauna tofauti na siasa ya kujenga viwanda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…